Sakata la Adamu Mchomvu na Mbasha

Sakata la Adamu Mchomvu na Mbasha

Sijasoma yotee
IMG_20200819_113516.jpg
 
Ukweli ni kuwa utani unategemea na uhalisia...ni vizuri sana watu watofautishe utani na uhalisia.

Utani usio na madhara ni ule ambao sio halisi mf. Ww sio mwizi katika utani ukiitwa mwizi huwez chukia wakati huo huo kama ni mwiz kweli lazma uchukie.

Kutana na albino mtanie hivi 'ngoz yako ni dili" utajikuta polisi siku hiyo hiyo.

Kama Adam Mchomvu asingekuwa mvuta bange asingempiga mtama ila angeona ni utani tu,lakini kwa sababu adam anapiga kisiri aliona kama anaaibishwa hata kama mbasha hakumaanisha vibaya.

Jaribu hii hapa hapa JF "wachaga ni wapiga dili tu"
"Wamakonde ni wapiga dili tu" angalia watakokuja juu ni kina nani?
 
SAKATA LA MITAMA YA ADAMU DHIDI YA MBASHA

Na, Robert Heriel

Tamasha la CCM lilikuwa la kuvutia sana, lilichangamsha washabiki wa sanaa waliohudhuria katika uwanja wa Uhuru na wale tuliokuwa tunafuatilia live kwenye onlineTv, na wengine waliokuwa wakifuatilia kwenye Channel Luningani.

Kama sikuwapongeza waandaji wa Tamasha hilo, na CCM basi nichukue nafasi hii kuwapongeza. Watu walifurahi, waliopata hela walipata, basi mambo yalienda sawa.

Lakini Dosari ilijitokeza pale ambapo Adamu Mchomvu alipombunda mtama Mbasha. Dooh! Ilikuwa ni aibu sana. Binafsi sikutegemea kama jambo lile lingefanyika.

Wapo waliomsifia Adamu Mchomvu na Kumponda Mbasha, lakini pia wapo walikuwa upande wa Mbasha wakimponda Adamu mchomvu. Basi kila mtu na mtazamo wake na ufikiriaji wake.

Mimi nitakuwa upande wa Mbasha, Kwa nini?

Mbasha na Adamu wote ni vijana wanaokaribia utu uzima.

Vijana sisi tunalugha zetu, tuna misemo yetu, tuna matani yetu, tuna namna tunavyoishi ili kusukuma maisha yaende.

Sikuona kosa la Mbasha kumuita Adamu ni "bange'' Tena hata mimi Taikon mtu akiniita Bange sioni shida ikiwa anachokisema sio kweli na hakina Madhara.


Neno "BANGE'' maana yake ya msingi ni mmea ambao majani yake hutumika kutengenezea madawa ya kulevya yaitwayo bange. Hiyo ndio maana ya msingi ya neno hilo.

Lakini kuna maana za ziada, kwa sisi wana lugha tunajua maneno huweza kuwa na maana zaidi ya moja mbali na maana ya msingi.

Kwa mfano Neno "Simba'' maana yake ya msingi ni mnyama jamii ya paka alaye nyama aishiye mwituni. Lakini Simba huweza kutumika kama mtu mtawala, mwenye nguvu, mfalme. Hata Yesu alijiita Simba wa Yuda bila shaka akirejelea Maana ya '' mfalme wa Yuda''

Mfano wa Pili ni "Jiwe'' ambalo maana ya msingi ni madini aina ya chuma yapatikanayo ardhini. Lakini maana ya ziada ni kuwa kitu kigumu, kitu kisicho yumbishwa wala kutetereshwa, kitu ambacho ni mhimili. Wapo watu wengi waliojiita Jiwe, Hata Yesu alijiita Jiwe Kuu la pembeni, pia kama sijakosea Mhe. Rais naye aliwahi kujiita Jiwe, akirejelea maana hizo nilizozitoa na nyinginezo ambazo sijazitoa.

Kila mfano una upande hasi na upande chanya. Hivyo inategemea na akili ya mtu atakavyotafsiri

Mifano ipo Mingi, mtu kuitwa jina fulani inategemea na matendo yako au unavyoonekana. Inaweza kuwa ni utani au kweli.

Kwa mazingira ya Adamu na Mbasha ni wazi kuwa yalikuwa mazingira ya furaha, burudani, mazingira ya utani, basi tuu watu wafurahi. Mbasha alimtania Adamu, kwa misingi ya matani lakini nafikiri kwa kadiri anavyomfahamu.

Kutumia neno Bange kwa muktadha wa siku ile, usingeleta athari yoyote kwa Adamu. Ilikuwa ishu ndogo mno. Kwani kila mmoja angejua ni masihara tuu.

Mtu akikuambia kichwa chako ni bange, au wewe nawe ni bange, atakuwa na maana zifuatazo; Mosi, wewe ni waruwaru, wewe umechangamka sana, mtu ambaye hujatulia, mtu mchapakazi, mtu jasiri asiye na aibu, mtu mwenye maamuzi pasipo kushirikisha akili yake n.k

Sasa inategemea umechukua maana ipi.

Mimi ningeweza kusema kuwa Mbasha alimtania Adamu akimaanisha, Adamu ni mtu aliyechangamka sana, na mtu mchapakazi.

Nipo upande wa Mbasha kwa sababu, Mbasha hakuwa na dhamira mbaya, na hii tunaiona hata baada ya kupigwa mitama alijikausha tuu, kama Mbasha angekuwa amedhamiria toka moyoni basi ule ungekuwa ugomvi mkubwa.

Adamu kakosea kwa sababu hakupaswa achukue maamuzi ya namna ile. Yale ni maamuzi makubwa sana. Kumpiga mtu hadharani kisa utani tuu ni jambo ambalo sio la kiungwana.

Adamu sio kwamba hajui maneno ya mtaani, maneno ya vijana, anajua lakini Alikosa utulivu na hakuipa akili yake nafasi ifanye kazi, aliruhusu mihemko.

Mbasha huenda alikosea lakini kiukweli hakukosea pakubwa kama watu wanavyotaka kuaminisha Umma.

Adamu ndiye kajiaibisha kwa kudhihirsha maneno hasi ya neno bange,Alichoonyesha ndio bange yenyewe, yaani upande hasi wa Bange.

Adamu kadhihirishia Wote waliopata kuangalia tukio lile kuwa yeye hana subira, hana hekima, hajui namna ya kutatua migogoro, anapenda kukuza mambo, hawezi kutawala hasira yake, wachache ndio watamsifu lakini wengi hasa wenye akili na wenye nafasi nzuri kimaisha watamuona kama mtu asiye mstaarabu.

Kama Adamu alitaka kulimaliza palepale asingepaswa kumpiga, angemuambia Mbasha aombe radhi palepale na akanushe maneno yake, au Mbasha ampe maana ya kile alichokuwa amemuambia. Lakini kumpiga haikuwa suluhu zaidi ya kuonyesha Bange zenyewe kwa upande hasi.

Mwisho niseme, Pongezi kwa Msemaji Mkuu wa Serikali Mkuu wa serikali kwa kuwapatanisha vijana hao. Ni jambo nzuri sana. Lakini nitoe wito kwa Watanzania kuwa, tuangalie namna tunavyotoa maamuzi yetu pale tunapokuwa na hasira. Lakini pia kwa wale wapenda utani, tuangalie watu wa kutania kwa maana wengine hawajui hata maana ya utani.

Robert Heriel
Taikon waFasihi
0693322300
20200818_140927.jpg
 
Ndio kina nani hao Adam Mchomvu na huyo Mbasha naona storiii ndefuu utadhani wote tunaishi huko dar.
Adam Mchomvu ni Mgombea wa Urais Zanzibar kupita Cuf.
Mbasha ni mme wa Hadija Koppa yani baba yake Zuchu.
 
Hapo kwenye CHADEMA umedanganya mkuu,

Huko yanapatikana matusi tu.
Ngoja nikutukane kidogo.

CCM na Mwenyekiti wao wamewavalisha Twiga mizula na kuwatoa Serengeti na kuwapeleka kijijini kwa mwenyekiti wao wa Chama.
 
Msemeji mkuu wa serikali amekwishalimaliza japo Mbasha ni wazi hakuridhika lakini the case is closed, anayebisha aka appeal.
Ni wapi ambapo sheria inampa mamlaka msemaji wa serikali kumaliza jambo kama hilo?
 
naungana na wewe mleta mada. tatizo Adam ni mvuta bangi ndio maana ilimuuma
 
We mtoa mada bange sana... Hii story si ya wiki ileeee.... Bado inatrend tu
 
Adam muoga kwa nini asimfuate faraghani wazichape huko huko!

Au apige risasi kabusa yaishe.
 
Mleta mada nae ni walewale bangi tupu . Sasa
Bange ndiyo nini?
 
Back
Top Bottom