SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,280
Wanawake wanapenda kuwa wasafi sana wataoga mara tatu au zaidi kwa siku, watadeki kila kona ya nyumba yao nk.nk Lakini kumbe katika mawazo yao ya usafi, wanadhani kwamba wasipofanya usafi huo watagundulika na watu yaani wageni watagundua kwamba sakafu iliyo chini ya kabati ni chafu. Dhana hii ilinigharimu sana mwaka 2008 nilipokuwa namalizia kujenga nyumba yangu.
Nyumba yangu hiyo ilifika hatua ya kupaka rangi. Nikanunua makopo kadhaa ya rangi za mafuta (Oil paint) na kuyaficha mvunguni mwa kitanda tunacholala mimi na mke wangu. Ikatokea kwamba kabla ya kutumika kwa rangi shemeji yangu aishiye ng'ambo akaleta habari kwamba alitaka kututembelea yeye, mkewe, na rafiki yao ambaye ni mwenyeji wa nchi waliyokuwa wanaishi (Denmark).Kwa hiyo tukajiandaa kupokea ugeni wa watu watatu.
Ona jinsi nyumba tulokuwa tumepanga ilivofanyiwa usafi! Wee bwanaeee! Nondo za madirisha zilioshwa na kung'aa sana. Kila kona ya nyumba ilisuguliwa na king'arishwa. Makopo yangu ya rangi (makopo 10) yaliondolewa mvunguni na kuwekwa kwenye kakibanda kamoja uani.Nilipomwuliza mke wangu kwa nini afanye hivyo ilhali wageni hawataingia chumbani kwetu alikataa katakata na kusema hayo makopo ni uchafu chumbani kwetu. Nikanyamaza kwa kujua kwamba hiyo ni saikolojia ya usafi inamsumbua.
Wageni wetu wakaja tukawakaribisha vizuri wakarudi zao siku hiyohiyo jioni.
Tukalala. Kesho yake asubuhi nilipoamka na kwenda uani, nilishangaa kuona mlango wa kibanda u wazi. Nilipoingia na kukagua, nikagundua kwamba makopo yote kumi ya rangi yameibwa! Nilihuzunika sana kwa kuwaza kwamba yangebaki chumbani yangekuwa salama ila yaliponzwa na saikolojia ya usafi wa mke wangu.
Unatakiwa kuwa mwangalifu mkeo anaposema anafanya usafi wa nyumba. Anaweza kabisa kuhamisha kifaa chako muhimu na kukiweka mahali pasipo na usalama mradi tu anafanya usafi!