Saikolojia ya Nyani.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,025
Nenda katika msitu wenye nyani wengi.Msitu huo uwe na akina mama wanaokata kuni,kufunga mizigo ya kuni na kuibeba kichwani.Daima nyani huwaangalia kwa makini sana hawa akina mama wakidhani kwamba ile mizigo ya kuni inayoinuliwa na kuwekwa kichwani ni miti inang'olewa.Sasa jaribu kwenda chini ya mti wenye nyani juu,weka kata kichwani halafu jifanye kama unajitwisha ule mti.Kitakachotokea hapo,hata kama huo mti una urefu gani,nyani wote watajirusha mpaka chini wakihofu kupinduliwa pamoja na ule mti.
 
yah...hii nilishawahi kuona mahali.....
nyani aliiba sufuria akapanda nayo juu ya mti....
ikabidi mwenye sufuria atumie hii njia....
bwana nyani alishuka na sufuria huku hajiwezi kwa kupatwa na tumbo la ghafla......
 
Kama msitu una chui wengi,mida ya jioni nyani wakubwa hulala matawi ya chini na nyani wadogo wanalala matawi ya juu.Nyani wakubwa wanafanya unafiki huu wakijifanya wanawalinda nyani wadogo dhidi ya chui,lakini ikifika usiku mambo huwa vice-versa,nyani wakubwa kwa kunyata wanakwenda matawi ya juu zaidi na kuwaacha nyani wadogo kama chambo.
 
Na kwa taarifa yako kama nyani anajua anaishi msitu mmoja na chui,akibanwa na haja usiku,hujisaidia mkononi na kujipaka kinyesi kichwani.Hii yote ni kuogopa kinyesi kisidondoke chini kwa sababu chui atajua kwamba nyani yuko juu ya mti.
 
...na nyani akiona bunduki au mkuki huachia ushuzi usio wa kawaida!
 
kwa taarifa yako nyani wa hapa Udsm wadada wakipita ama wakikaa chini ya miti basi hawa nyani watajichezeshachezesha kwenye miti ama chini ngoja apite kaka sasa....
Malizia anayejua.
 
Ni nduki kali!
 
Nenda katika msitu wenye nyani wengi.Msitu huo uwe na akina mama wanaokata kuni,kufunga mizigo ya kuni na kuibeba kichwani.Daima nyani huwaangalia kwa makini sana hawa akina mama wakidhani kwamba ile mizigo ya kuni inayoinuliwa na kuwekwa kichwani ni miti inang'olewa.Sasa jaribu kwenda chini ya mti wenye nyani juu,weka kata kichwani halafu jifanye kama unajitwisha ule mti.Kitakachotokea hapo,hata kama huo mti una urefu gani,nyani wote watajirusha mpaka chini wakihofu kupinduliwa pamoja na ule mti.

Hii nitaifanyia majaribio leo hii hii.
 
kwa taarifa yako nyani wa hapa Udsm wadada wakipita ama wakikaa chini ya miti basi hawa nyani watajichezeshachezesha kwenye miti ama chini ngoja apite kaka sasa....
Malizia anayejua.

nawewe unasoma chuo?
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom