Saikolojia: Hatua tano za kuukubali ukweli/uhalisia

Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
8,295
19,195
Ulishawahi kuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye mnapendana kwa dhati? Mmeweka mipango ya pamoja na mnapambana kuitimiza. Labda mmeshatambulishana hadi kwa jamii inayowazunguka - ndugu, jamaa na marafiki. Ukiangalia mipango na maisha yako ya baadaye yote imejawa na huyo mtu. Unamuamini kupita kiasi. Pengine hata unawaza bila yeye maisha yako hayana thamani yoyote, hayawezekani.

Halafu ghafla inatokea mwenzako anageuka ghafla, anataka kuondoka. Pengine mmekoseana, mmetofautiana kidogo au sana, na au hata hakuna sababu yoyote ila mwenzio anakuambia safari yake kwenye maisha yako imefikia tamati. Pengine anakueleza upungufu na udhaifu wako, au anaweza asikuelezee. Pengine anakuambia wewe ni mtu mwema sana kuliko yeye, hivyo anaona hastahili kuwa na wewe au akakuambia wewe siyo type yake.

Vyovyote iwavyo; mtu ambaye yupo mbele yako amekuletea ukweli mpya mbele yako ambao unapaswa kuupokea hata kama hautaki au haupendi - anapaswa kuondoka. Wewe haupo tayari kuupokea ukweli huu; Wanasaikolojia wanakuambia ili upate uponyaji wa kweli ni lazima upitie hatua tano zifuatazo:

1. Denial (Kuukataa)
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambapo utaukataa ukweli/uhalisia huo mpya. Unakuwa unawaza hawezi kuniacha tumetoka mbali sana, tumefanya mambo mengi sana pamoja, huwa tunatofautiana tu tunayamaliza, ananipenda sana, ninampenda sana na yeye anajua, hawezi kuniacha na tuna watoto, hawezi kuniacha na pesa zote hizi nilizonazo au urembo huu, hawezi kuniacha kwa anavyonitegemea, n.k.

Mkuu, hakuna cha mmefanya mangapi au mlipendana kiasi gani; hakuna cha mali wala urembo, hakuna cha watoto wala eti wazazi, hakuna cha alishajitambulisha kwenu na au umetoa/kutolewa mahari. Kama ameamua kwenda, ujue tu ndio imetoka hiyo.

Kitu kizuri cha kufanya kwenye hatua hii ni kuanza kujiandaa kuupokea ukweli wowote uliopo mbele yako.

2. Anger (Hasira)
Hii ni hatua inayofuata baada ya ile ya kwanza. Katika hatua hii unakuwa na hasira sana. Unamchukia aliyekuacha na au hata watu au vitu unavyohisi vimesabisha. Hapa ndio unakuwa kwenye hali ya kumchukia mtu ila bado unampenda. Unakuwa unajifariji na maneno kama "anaringa sana ila ndio hivyo ninampenda sina jinsi", "ananifanyia hivi kwa kuwa anajua ninampenda", "pamoja na yote tuliyoyafanya pamoja leo ndio ananifanyia hivi kweli!!?"; mara unausingizia moyo wakati wewe mwenyewe hautaki kusikiliza ubongo unaokuambia ukweli, hahaha...

Hapa unaweza hata kujichukia wewe mwenyewe kwa kumpenda mtu kupitiliza. Unamchukia mhusika kuwa hajali hisia zako, hajali jinsi unavyojitoa kwake, jinsi ulivyomthamini. Unamchukia kuwa amekuchezea tu na sasa umempa mzigo anakukimbia. Unawachukia wanaume au wanawake wote. Unakuwa unapatwa na uchungu mkali na usioelezeka, mara nyingine hata unashinda unalia, unakonda wakati mwenzio anazidi kunenepa, hahaha...

Namna nzuri ya kushughulika na hatua hii ni kulia kwelikweli kama unahisi kulia, kuwashirikisha watu wako wa karibu - ndugu, jamaa na marafiki - ambao unahisi watakuwa na wewe, unaowaamini. Achilia huo uchungu, ndio unapona hivyo.

3. Bargaining/compromising (Kutafuta maelewano)
Baada ya hasira kuwa nyingi, na kutafuta faraja huku na kule utashauriwa na moyo au pengine na watu wako wa karibu kuwa mtayamaliza tu, mkae chini muongee. Basi na wewe unajidanganya eti mtayamaliza kweli. Unamtafuta mwenzio unaanza kumbembeleza mrudiane, asiondoke. Unamshawishi kuwa bila yeye wewe siyo kitu, maisha yako bila yake yatakuwa na ni sawa na gari bila konda, hahaha... Unampenda sana.

Unaweza hata kumkumbusha mambo aliyokuahidi, moments nzuri mlizozipitia, na kwamba wewe ni mwanadamu tu. Hapa ndio watu huomba msamaha hata kama hawakukosa na kutoa ahadi hata wasizoweza kuzitimiza ili tu watu hao wabaki katika maisha yao. Hapa ndio watu wanakuwa tayari hata kutoa mahari wakati waligoma kwa miaka kadhaa, hapa watu ndio huwa tayari hata kutoa mbususu walizozibania kwa miongo kadhaa, hapa watu huwa tayari kufanya chochote ili tu wasiuruhusu uhalisia au ukweli mpya kuchukua nafasi. Ndugu yangu, mtoto wa mtu kama ameamua kwenda hata uahidi kumpa dunia yote hawezi kukuelewa. Kwahiyo hata ufanyaje, mwenzio ameamua kwenda muache tu aende. Ukiachwa achika. Hahaha...

Ndugu, kitu kizuri cha kufanya hapa ni kusikiliza tu ushauri na uzoefu wa watu waliowahi kupitia hali kama hii - ambao watakushauri umuache tu aende.

4. Depression (Msongo wa mawazo)
Baada ya kupambana kadiri uwezavyo, kujishusha mpaka chini kabisa na kufanya kila kitu ndani ya uwezo wako na unaona mambo yamegoma kabisa, ndio unapata msongo wa mawazo. Unajutia hisia na muda uliouwekeza ambao mwisho wa siku umepotea. Ukiwaza namna ulivyojitoa, unapata stress ya kufa mtu. Utawaambia nini watu ambao pengine uliwaoshea? Hahaha... Hapa ndio watu hukasirikia kila mtu.

Hata hivyo habari njema ni kuwa unakaribia kuukubali ukweli. Hivyo njia nzuri ni kuanza tu kujiandaa kuipokea hatua ya tano na ya mwisho.

5. Acceptance (Kuukubali)
Baada ya yote sasa inafikia kipindi mtu unaamua tu kuukubali ukweli - unamuacha aende au unaupokea ukweli. Hapa sasa ndio mtu anaanza kurudia hali yake ya kawaida. Hapa hata walioapa hawatakuja kupenda ndio unaona sasa wanapenda tena. Waliosema wanaume wote ni mbwa ndio hapa wanakuwa tayari kubwekewa na mbwa mwingine tena, hahaha...

Note:
  • Tunapokushauri kuwa utapona baada ya muda na kila kitu kitakuwa sawa, huwa tunamaanisha kukupa muda ili uzipitie hatua hizi vizuri na kwa ukamilifu. Hii ndio maana halisi ya time heals.
  • Tujue kabisa kuwa break up zinaumiza. Hakuna kabisa (au kama ipo ni mara chache sana) kuachana kwa amani. Ukiachwa ni lazima uumie. Hata ndugu zangu Sukuma Gang muda utatuponya na tutaukubali ukweli kuwa hii nchi imerudi kwa wenye nao - wapigaji - baadaya kupitia hatua hizi zote. Hahaha...
Ninawatakia kipindi chema cha Pasaka.. Mlioachwa achikeni. Hahahaa...
 
Atakaeshindwa kuukubali ukweli anitafute nina namba za mganga maumivi ni yako na maamuzi ni yako kupanga ni kuchagua!,kwanini akuache wakati njia za asili zipo za kumrudisha!
#wemakeitsimple.. Nipe hizo namba mkuu.
 
Atakaeshindwa kuukubali ukweli anitafute nina namba za mganga maumivi ni yako na maamuzi ni yako kupanga ni kuchagua!,kwanini akuache wakati njia za asili zipo za kumrudisha!
#wemakeitsimple..😁
Hahaha... Waganga wanapiga pesa za bure.
 
Nimekuja mbio mbio nikijua kuna njia ya shortcut ya kuponya maumivu ya kuachwa, kumbe ni yaleyale ya kuteseka na maumivu kwa muda mrefu
Hahaha... Hakuna shortcut mkuu, haya mambo ni lazima uteseke.
 
Ulishawahi kuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye mnapendana kwa dhati? Mmeweka mipango ya pamoja na mnapambana kuitimiza. Labda mmeshatambulishana hadi kwa jamii inayowazunguka - ndugu, jamaa na marafiki. Ukiangalia mipango na maisha yako ya baadaye yote imejawa na huyo mtu. Unamuamini kupita kiasi. Pengine hata unawaza bila yeye maisha yako hayana thamani yoyote, hayawezekani.

Halafu ghafla inatokea mwenzako anageuka ghafla, anataka kuondoka. Pengine mmekoseana, mmetofautiana kidogo au sana, na au hata hakuna sababu yoyote ila mwenzio anakuambia safari yake kwenye maisha yako imefikia tamati. Pengine anakueleza upungufu na udhaifu wako, au anaweza asikuelezee. Pengine anakuambia wewe ni mtu mwema sana kuliko yeye, hivyo anaona hastahili kuwa na wewe au akakuambia wewe siyo type yake.

Vyovyote iwavyo; mtu ambaye yupo mbele yako amekuletea ukweli mpya mbele yako ambao unapaswa kuupokea hata kama hautaki au haupendi - anapaswa kuondoka. Wewe haupo tayari kuupokea ukweli huu; Wanasaikolojia wanakuambia ili upate uponyaji wa kweli ni lazima upitie hatua tano zifuatazo:

1. Denial (Kuukataa)
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambapo utaukataa ukweli/uhalisia huo mpya. Unakuwa unawaza hawezi kuniacha tumetoka mbali sana, tumefanya mambo mengi sana pamoja, huwa tunatofautiana tu tunayamaliza, ananipenda sana, ninampenda sana na yeye anajua, hawezi kuniacha na tuna watoto, hawezi kuniacha na pesa zote hizi nilizonazo au urembo huu, hawezi kuniacha kwa anavyonitegemea, n.k.

Mkuu, hakuna cha mmefanya mangapi au mlipendana kiasi gani; hakuna cha mali wala urembo, hakuna cha watoto wala eti wazazi, hakuna cha alishajitambulisha kwenu na au umetoa/kutolewa mahari. Kama ameamua kwenda, ujue tu ndio imetoka hiyo.

Kitu kizuri cha kufanya kwenye hatua hii ni kuanza kujiandaa kuupokea ukweli wowote uliopo mbele yako.

2. Anger (Hasira)
Hii ni hatua inayofuata baada ya ile ya kwanza. Katika hatua hii unakuwa na hasira sana. Unamchukia aliyekuacha na au hata watu au vitu unavyohisi vimesabisha. Hapa ndio unakuwa kwenye hali ya kumchukia mtu ila bado unampenda. Unakuwa unajifariji na maneno kama "anaringa sana ila ndio hivyo ninampenda sina jinsi", "ananifanyia hivi kwa kuwa anajua ninampenda", "pamoja na yote tuliyoyafanya pamoja leo ndio ananifanyia hivi kweli!!?"; mara unausingizia moyo wakati wewe mwenyewe hautaki kusikiliza ubongo unaokuambia ukweli, hahaha...

Hapa unaweza hata kujichukia wewe mwenyewe kwa kumpenda mtu kupitiliza. Unamchukia mhusika kuwa hajali hisia zako, hajali jinsi unavyojitoa kwake, jinsi ulivyomthamini. Unamchukia kuwa amekuchezea tu na sasa umempa mzigo anakukimbia. Unawachukia wanaume au wanawake wote. Unakuwa unapatwa na uchungu mkali na usioelezeka, mara nyingine hata unashinda unalia, unakonda wakati mwenzio anazidi kunenepa, hahaha...

Namna nzuri ya kushughulika na hatua hii ni kulia kwelikweli kama unahisi kulia, kuwashirikisha watu wako wa karibu - ndugu, jamaa na marafiki - ambao unahisi watakuwa na wewe, unaowaamini. Achilia huo uchungu, ndio unapona hivyo.

3. Bargaining/compromising (Kutafuta maelewano)
Baada ya hasira kuwa nyingi, na kutafuta faraja huku na kule utashauriwa na moyo au pengine na watu wako wa karibu kuwa mtayamaliza tu, mkae chini muongee. Basi na wewe unajidanganya eti mtayamaliza kweli. Unamtafuta mwenzio unaanza kumbembeleza mrudiane, asiondoke. Unamshawishi kuwa bila yeye wewe siyo kitu, maisha yako bila yake yatakuwa na ni sawa na gari bila konda, hahaha... Unampenda sana.

Unaweza hata kumkumbusha mambo aliyokuahidi, moments nzuri mlizozipitia, na kwamba wewe ni mwanadamu tu. Hapa ndio watu huomba msamaha hata kama hawakukosa na kutoa ahadi hata wasizoweza kuzitimiza ili tu watu hao wabaki katika maisha yao. Hapa ndio watu wanakuwa tayari hata kutoa mahari wakati waligoma kwa miaka kadhaa, hapa watu ndio huwa tayari hata kutoa mbususu walizozibania kwa miongo kadhaa, hapa watu huwa tayari kufanya chochote ili tu wasiuruhusu uhalisia au ukweli mpya kuchukua nafasi. Ndugu yangu, mtoto wa mtu kama ameamua kwenda hata uahidi kumpa dunia yote hawezi kukuelewa. Kwahiyo hata ufanyaje, mwenzio ameamua kwenda muache tu aende. Ukiachwa achika. Hahaha...

Ndugu, kitu kizuri cha kufanya hapa ni kusikiliza tu ushauri na uzoefu wa watu waliowahi kupitia hali kama hii - ambao watakushauri umuache tu aende.

4. Depression (Msongo wa mawazo)
Baada ya kupambana kadiri uwezavyo, kujishusha mpaka chini kabisa na kufanya kila kitu ndani ya uwezo wako na unaona mambo yamegoma kabisa, ndio unapata msongo wa mawazo. Unajutia hisia na muda uliouwekeza ambao mwisho wa siku umepotea. Ukiwaza namna ulivyojitoa, unapata stress ya kufa mtu. Utawaambia nini watu ambao pengine uliwaoshea? Hahaha... Hapa ndio watu hukasirikia kila mtu.

Hata hivyo habari njema ni kuwa unakaribia kuukubali ukweli. Hivyo njia nzuri ni kuanza tu kujiandaa kuipokea hatua ya tano na ya mwisho.

5. Acceptance (Kuukubali)
Baada ya yote sasa inafikia kipindi mtu unaamua tu kuukubali ukweli - unamuacha aende au unaupokea ukweli. Hapa sasa ndio mtu anaanza kurudia hali yake ya kawaida. Hapa hata walioapa hawatakuja kupenda ndio unaona sasa wanapenda tena. Waliosema wanaume wote ni mbwa ndio hapa wanakuwa tayari kubwekewa na mbwa mwingine tena, hahaha...

Note:
  • Tunapokushauri kuwa utapona baada ya muda na kila kitu kitakuwa sawa, huwa tunamaanisha kukupa muda ili uzipitie hatua hizi vizuri na kwa ukamilifu. Hii ndio maana halisi ya time heals.
  • Tujue kabisa kuwa break up zinaumiza. Hakuna kabisa (au kama ipo ni mara chache sana) kuachana kwa amani. Ukiachwa ni lazima uumie. Hata ndugu zangu Sukuma Gang muda utatuponya na tutaukubali ukweli kuwa hii nchi imerudi kwa wenye nao - wapigaji - baadaya kupitia hatua hizi zote. Hahaha...
Ninawatakia kipindi chema cha Pasaka.. Mlioachwa achikeni. Hahahaa...
Hizi kitaalamu zinaitwaga DABDA,,stage of death umenikumbusha mbalii## hongera
 
Ahsante umeniponya sana maana nami yamenikuta yooote uliyoyaongea ni mimi mtupu. Tokea siku ya ijumaa kuu hadi leo ijumaa mpenzi wangu ameniacha kimya kimya hajaongea chochote namba zake hapatikani, kaondoka dar anaishi na mtu aliemzalisha ambae walikuwa wameachana.
 
Saikolojia haidanganyi kaka.

Hata hivyo tumeonywa sana humu kuhusu single mamas.

Pole mkuu, utapona na utasahau.
 
You made my day!!🙏🙏🙏
 
Umeandika kama utani utani upuuzi upuuzi ila dah sijui kwa nini umeamua kuniongelea mimi indirect? Ahaaaaaaa hata hivyo nimeishia kucheka

Ahaaaa nimekumbuka ile kuachana kimia kimia, hakuna majibizano kama utani mwezi ukakatika bila hata sms.ikaisha hivyo.

Wewee kweriiiiii faraaa😂😂 upuuzi upuuzi ulouandika nikajikuta nacheka, watu tumegalagala juu ya kaburi lakini ndo hivyo tena harudi tena.

Aisee umenikumbusha faraaa mmoja kama utani nikamute nae si akamute ahaaaa hadi leo ikaisha hivyoooo.
 
Haha... Saikolojia ni nyoko sana. Mambo yanatokea kwa pattern ileile, hakuna jipya.
 
Back
Top Bottom