Said Mwema - Kuwa shemeji ya Rais ni leseni?

Said Mwema - Kuwa shemeji ya Rais ni leseni?

Sijui mpaka lini na kwanini...
Sijui kwanini CDM hadi leo hii hawajaanzisha maandamano ya kumshinikiza Mwema aondoke au aondolewe; hata Bungeni hakunyoshewa kidole yeye mwenyewe na kutaka aondoke.. sijui mpaka nani wa CDM auawe ndio watajua kuwa Mwema na Chagonja ni hatari kwa demokrasia!!! Kutokana na rekodi zao wenyewe inaonekana wamejifanya kuwa ni maadui wa kudumu wa haki za kiraia na haki za binadamu. Wazo kuwa wananchi wana haki ya kuandamana kuipinga serikali yao au uongozi wa walio madarakani halijawaingia kabisa kichwani! Wako kama maafisa wa kizungu wa wakati wa mkoloni ambao walijaribu kuzima maandamano yaliyoongozwa na Mwalimu Nyerere au wale waliowafunga kina Makange! Hawana tofauti!

Kha! kumbe Mwema ni Bwa'she wa mkuu wa kaya!! Huyu Ndiye mjomba wa Riz1? ama kweli inji hii ni ya Kaka, dada, mjomba, mabwa'she na washikaji wa Mkuu wa kaya. Ndo maana hatuendi mbali.
 
Nasikia una usongo wa kila mwenye cheo Serikalini kwani ulikuwa na hamu ya kurithi kazi ya baba'ko na umpite kwa cheo kwani yeye aliishia u rpc tu lakini kimo ndio kikawa tatizo kwako na ukashindwa kukubalika jeshini na uraiani ukaamuwa kuzamia USA na kuishi mafichoni. Pole sana na ahsante aliyegunduwa intaneti, angalau unaweza kujificha nyuma ya pazia na ukasambaza ***** bila ya kujulikana ni nani.

Sitaki kuamini kuwa ni kile kisa cha Tanga!

ZOMBA Bwana! lini ukaungana na wapenda ukweli?
 
Kwenye fujo lazima Polisi waende kutuliza ghasia.

Nakumbuka Said Mwema alipochaguliwa wewe mwanakijiji ndio ulikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumfagilia tukiwa kule Youngafrican na ulisema amekusaidia kwenye mambo yako kadha wa kadha. Sasa iweje leo ugeuke tena?
 
Hapo naomba nipingane na wewe, toka mwema ameingia jeshi la polisi limekuwa la hovyo haijapata kutokea. Rushwa inachukuliwa njenje, mtu ukiibIwa huwezi kufikiria kwenda polisi kwani ni kupoteza hela bure. Utendaji wa polisi umekuwa kama wa waganga wa kienyeji baada ya Mwema kuingia na sasa anataka akumbukwe kwa mauaji ya raia

You are not serious, unataka kusema kipindi cha Mahita kilikuwa afadhali?
 
Eti anapotoa kikatili roho ya mtu mwingine Mungu hapendi, je mauaji ya Arusha, mwanza, Morogoro jana na shm nyingine kibao Mungu ndo anayoyapenda? Mkuki kwa nguruwe mtamuhee!
 
Sijui mpaka lini na kwanini...
Sijui kwanini CDM hadi leo hii hawajaanzisha maandamano ya kumshinikiza Mwema aondoke au aondolewe; hata Bungeni hakunyoshewa kidole yeye mwenyewe na kutaka aondoke.. sijui mpaka nani wa CDM auawe ndio watajua kuwa Mwema na Chagonja ni hatari kwa demokrasia!!! Kutokana na rekodi zao wenyewe inaonekana wamejifanya kuwa ni maadui wa kudumu wa haki za kiraia na haki za binadamu. Wazo kuwa wananchi wana haki ya kuandamana kuipinga serikali yao au uongozi wa walio madarakani halijawaingia kabisa kichwani! Wako kama maafisa wa kizungu wa wakati wa mkoloni ambao walijaribu kuzima maandamano yaliyoongozwa na Mwalimu Nyerere au wale waliowafunga kina Makange! Hawana tofauti!



Wanafuata ushauri wa brother wao (Kikwete). Mtu incopetent siku zote hapendi ushindani, yaani atajitahidi kukuzima hata kwa uchawi ili mradi tu asipate washindani.
 
Huyu chagonja kwanza kabisa sio mtanzania,ni mnyarwanda,juzi tu hapa katoka kumzka baba yake uko Rwanda,na pia cjui kama ni mtu muelewa kwa sababu hata familia yake mwenye ameshndwa kuilea,watoto wake wanashnda kwnye mabar hasa pale silver town pale karibu na uhamiaji kurasini wanapga maznga,.tuanze na uraia wake razima ni wakimagumashi tu.
 
Tutafika tu, yana mwisho haya, ni uthubutu tu ndo unahitajika!
 
lazima watambue nchi hii si mali ya ccm peke yao,na watu wana demokrasia ya kupinga chochote kulingana na utashi wao.

Hivi huko ktk siku za mbeleni hawawezi kuwajibishwa? uzuri wa historia kamwe huwa haifutiki
 
Ndugu wana JF na Watanzania wote wapenda amani,
Naandika hii thread nikiwa na huzuni na uchungu sana moyoni kuhusiana na kile kilichotokea Mkoani Morogoro jana tarehe 27/08/2012. Kwa mara nyingine tena damu isiyo na hatia imemwagika kwasababu za kishenzi,kijinga,kizembe na chuki za kisiasa dhidi ya Upinzani!

Nasikitika kusema kuwa mauaji haya yamesababishwa na Rais Kikwete akisaidiana na Mkuu wake wa Jeshi la Polisi-IGP Mwema. Hawa jamaa 2 wako nyuma ya mipango yote hii ya kuzuia maandamano kwa kupiga watu mabomu,risasi za moto na maji ya washawasha! Kile walichofanya Polisi wa Morogoro chini ya usimamizi wa Kamanda Shilogile ni maelekezo maalumu ya Rais Kiwete na IGP Mwema. Wakubali,wasikubali huo ndiyo ukweli!

Napenda tu niwape salamu Rais Kikwete na IGP Mwema kwamba ile damu iliyomwagika jana pale Msamvu Morogoro na damu nyingine ambayo ilishamwagika huko Arusha,Mbeya,Mwanza,Mara(Tarime),Tabora(Igunga),Arusha(Arumeru East) na itakayoendelea kumwagika jueni kwamba ni chachu ya ukombozi kwa Watanzania! Inasikitisha kuona kwamba watu wasio na hatia wanaendelea kuuawa na Jeshi la Polisi huku Rais na IGP wake wamekaaa pembeni wakichekelea! Kwanini viongozi wa Taifa hili hawataki kujifunza hata kutoka kwa majirani zetu?

Ni hivi karibuni tu Rais wa Malawi Bingu wa Msarika aliaga dunia. Kilichofuatia ni kwamba Rais aliyechukua nafasi Bi Joyce Banda alimtimua kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kwa vile Polisi wa Malawi walihusika katika mauaji ya raia wa Malawi waliokuwa wakiandamana. Juzi kule South Afrika kumetokea mauaji ya Wafanyakazi wa Migodi ya Marikana inayoshughulika na uchimbaji wa madini ya Platinum. Rais Zuma ameunda tume haraka sana kuchunguza chanzo cha mauaji hayo ya wafanyakazi wasio na hatia.

Tunataka Rais Kiwete na IGP Mwema waunde tume haraka ya kuchunguza mauaji na vurugu hizi za Morogoro. Tunataka RPC mkoa wa Morogoro Bwana Shilogile na askari waliohusika na mauaji hayo wasimamishwe kazi mara moja kupisha uchunguzi huo. Kama Rais Kiwete na IGP Mwema hawataweza kufanya hivyo basi watakuwa wanaendelea tu kuwathibitishia Watanzania kuwa wako nyuma ya mpango mzima wa vurugu na mauaji haya ya kipuuzi.

Namaliza kwa kusema kwamba haya matukio yanayochochewa na wanasiasa uchwara wa chama Twawala CCM yanaendelea kukidhalilisha chama cha CCM na serikali yake na hivyo kuzidi kujenga chuki kati ya Watanzania na serikali hii ambayo nathubutu kuiita ni ya kidikteta. CCM hamwezi kutawala nchi hii milele hilo liko wazi. Ni bora tu mkaacha demokrasia ya kweli ikachukua mkondo wake na watu wakaamua kuchagua kile wanachoona kinawafaa kwa maisha yao ya baadaye. Siasa za kulazimishana zilishapitwa na wakti!

Wasalaam.
 
.....[/QUOTE]
Huna hoja ya msingi kawaambie walioanzisha maandamano ndo chanzo cha vurugu na kuwaga damu, kwa sababu bila wao kuandamano pasipo kufuata taratibu na sheria haya yote yasingetokea, na wananchi wanaakili, ondoa propaganda zako.
 
Nasikia una usongo wa kila mwenye cheo Serikalini kwani ulikuwa na hamu ya kurithi kazi ya baba'ko na umpite kwa cheo kwani yeye aliishia u rpc tu lakini kimo ndio kikawa tatizo kwako na ukashindwa kukubalika jeshini na uraiani ukaamuwa kuzamia USA na kuishi mafichoni. Pole sana na ahsante aliyegunduwa intaneti, angalau unaweza kujificha nyuma ya pazia na ukasambaza ***** bila ya kujulikana ni nani.

Sitaki kuamini kuwa ni kile kisa cha Tanga!
Baba yake Mwanakjiji kumbe alikuwa RPC?
 
Jamani,
Bunduki za Polisi, Jeshi ni kwa ajili kuua watu. Tena zile za Polisi ni ajili RAIA wetu wenyewe. Wameuawa raia wengi sana kipindi hiki cha Jakaya na Mkapa pengine kuliko wakati mwingine wowote ule tangu turudishiwe uhuru wetu na wakoloni.

Suala hili linaigusa KATIBA yetu ya JMT ambayo mlinzi wake mkuu ni Rais wa JMT. Amekaa kimya akiona haya yote yanaendelea. Wabunge na Bunge letu wako kimya.

Ungetegemea CHADEMA yenye wanasheria na wasomi wengine wazuri kabisa wangechukua hatua angalau tukio kama lile la Morogoro lifike tu mahakamani. Lakini wapi? Zimebaki tu sinema za Nape na Mnyika ambao kwa sura ni warembo sana hasa kwenye sikirini za TV.
 
Back
Top Bottom