Naziona dalili za kujirudi kwa mbunge huyu, labda baada ya kusoma upepo kwa kuaangalia mwitikio wa wananchi baada ya mwanasiasa wa tanzania anyetumia cheo kama cha --------- wa Iran au yule mwenzake wa Korea kaskazini.
Arfi amekuwa kiongozi wa ngazi za juu wa CDM, hivyo ni matarajiao yangu kuwa anafahamu na kanuni, taratibu na sheria za chama na pia alihusika kupitisha katiba anayopinga hii leo. hili sio tatizo kwani hutokea mtu akapata wazo la pili baada ya kutoea kwa kitu fulani. Ninachojiuliza ni vipi makamu mwenyekiti alalamike ubovu wa katiba? hakuna utaratibu wa ndani ya chama wa kuwasilisha mapendekezo ya kufanyika kwa mabadiliko ya katiba?
kadhalika sio sahihi kusema kuwa katiba ya chadema inapingana na katiba ya nchi kwa kuwazuia wananchama wake kupeleka migogoro yao mahakamani. Ingetokea vipi kama mahakama kuu ingeamua kwa upande wa kiongozi mkuu? Hivi Pale TTF wanaruhusu migogoro yao kupelekwa mahakamani?
Wakati tunaona ni vibaya kwa jaji moja wa mahakama kutengua ubunge wa anayedaiwa kuchaguliwa na mamia kama sio maelfu ya wanannchi, vipi leo tuone ni sahihi migogoro ya ndani ya chama kupelekwa huko?