Sahihi kusema CCM imelegalega au CHADEMA ni imara jimbo la Segerea?

Jun 21, 2021
34
29
Wanabodi,

Nashawishika kuamini kwamba kwa shughuli za kisiasa wanazozifanya CHADEMA kwa sasa katika jimbo la Segerea zinazotokana na mtaji mkubwa wa kisiasa ulichonacho chama hicho jimboni hapo.

Tumeshuhudia vuguvugu la kudai katiba mpya likianzishwa pale, na sasa ufunguzi wa ofisi ya chama huku kukiwa na mikakati mingi ya kusukuma agenda za kudai katiba mpya kutokea jimbo hilo.

Hii ni wazi kuwa chama hicho kinaungwa mkono na kinaamini kwamba kina wafuasi wa kutosha kuunga mkono juhudi hizo vinginevyo shughuli hizo zisingeelekezwa jimboni hapo.

Kwa upande mwingine, nauona udhaifu mkubwa wa CCM katika jimbo la Segerea ambao unabakia kuangalia tu michakato ya kujenga chama ikifanyikia kwenye uwanja wao.

Itoshe tu kusema CCM jimbo la Segera imelala usingizi wa pono tokea kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa karibu yote 2019 na uchaguzi wa ubunge mwaka 2020.

CCM haifanyi harakati zozote iwe za kisiasa au za maendeleo zaidi ya yale mambo ya lazima na yaliyoanza siku za nyuma kama ujenzi wa machinjio ya kisasa na barabara kuelekea machinjioni ambazo ni agenda zilizoanza kabla ya 2020.

Zaidi ya hapo miradi mingine ya kuliteka jimbo kama ujenzi wa barabara ya barakuda-maji chumvi, urudishaji wa maeneo yaliyoporwa kama soko la Liwiti, urasimishaji wa makazi yaliyoendelezwa n.k vikiwa havishughulikiwi kabisa.

Nikiri tu kwamba hata madiwani waliochaguliwa baadhi ya maeneo ya jimbo kama Liwiti hawafahamiki kwa wananchi, na hata mbunge Bonna Kamoli akiwa anaishi kama mbunge aliyeridhika huku akiwakimbia wananchi wake.

Ikumbukwe CHADEMA hawajawahi kushinda nafasi ya ubunge katika jimbo hilo ila walishinda kata zaidi ya asilimia 90%. Je, CHADEMA wana mtaji katika ngazi za chini ambayo inasababisha CCM kujikuta wakiwa watazamaji wa yanayofanyika?

Siku zote mambo ya harakati yakifanikiwa historia huandikwa, ni aibu kwa historia kuandikwa katika jimbo la Segerea. CCM amkeni.
 
CCM haijawahi kuwa na mikakati ya maana, wanategemea Tume ya uchaguzi kuwabeba, Chadema iko imara majimbo mengi Dsm, Kibamba, Ubungo, Kawe na kwingine.

Hiyo shughuli Chadema wangeenda kuifanyia Ubungo ungeshangaa, Kawe ungeshangaa, Kibamba ungeshangaa, hata Kinondoni kwa kile nilichokiona Salum Mwalimu alipogombea wakati ule, uchaguzi ukiwa fair CCM hawana chao.
 
Itoshe tu kusema CCM jimbo la Segera imelala usingizi wa pono tokea kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa karibu yote 2019 na uchaguzi wa ubunge mwaka 2020.
Nimeishia hapa kusoma mada yako. Umeanza vizuri lkn hapa umeharibu mada yako.

CCM ilishinda uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020??

Sema su! Kama kweli unaamini CCM ilishinda uchaguzi wa 2020, na kama ukidanganya Mungu akupeleke aliko Magufuli Sasa hivi.
 
Walioshinda ndio waliopo kwenye uongozi kwa sasa. Kama una fikra tofauti hilo ni lako, na kwakuwa hakuna kesi mahakamani, hoja yako inabaki kuwa ya kufikirika. Toa hoja na sio vitisho
 
Walioshinda ndio waliopo kwenye uongozi kwa sasa. Kama una fikra tofauti hilo ni lako, na kwakuwa hakuna kesi mahakamani, hoja yako inabaki kuwa ya kufikirika. Toa hoja na sio vitisho
Sema su! Ili kama ni uwongo ufe.

Mbona unambwela mbwela?? Sema Su,.....ufe sasa hivi.
 
Back
Top Bottom