Saga la Makonda: My Take

Saga la Makonda: My Take

Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Mkuu,kukuelewesha tuu,wanao pambana na magu sio upinzani,bali ni umma wa watanzania.

Chunguza ni mara ngapi viongozi wa upinzani wanatoa matamko katika matukio,ni mara chache sana
 
Kuna wakati ngozi nyeusi wanajifanya wajanja na wajuaji sana na kudhani wameyapatia maisha, kumbe sio akili zao-ni rangi ya ngozi yao inawasumbua. Ngozi nyeusi popote ilipo dunian haikubalikiwa na Mungu, kazi ya ngozi nyeusi ni kupiga marktime.
 
Unachosema ni cha kweli lakini mimi naona wapinzani hawana cha kupoteza kwa uamuzi huu wa Magufuli kumuacha Makonda pamoja na ushahidi wa maovu yake. Kwa maoni yangu hiki kitendo na hotuba ya leo ipo kwenye kumbukumbu na itazidi kumwandama na kumchafua Rais Magufuli. Makonda amekwisha chafuka kusema kweli na Rais kumkumbatia mchafu inamuondolea credibility ya kupambana na uovu wa aina hii hii ya makonda kama utatokea huko mbele kwani ameshaweka precedent it is a principle that similar facts are to be treated equal, Magufuli anaweza kumtumbua kiongozi mwingine yeyote kwa kufoji vyeti na ama kwa kituko kingine sawa na hiki cha kuvamia clouds? Na hata akifanya hivyo hata sifiwa bali rekodi ya Leo watu wataitumia kujaji utumbuaji husika.

Sababu nyingine kwanini wapinzani hawatadhurika ni kwamba wapo watu ndani ya ccm akiwemo waziri Nape na baadhi ya wabunge wameshaonesha kutofurahishwa na makonda hii inaleta bifu ndani ya serikali.

Swala la mwisho ni mahusiano ya Makonda na clouds media yamekwisha.

Nahitimisha kwa kuunga mkono premise yako lakini observation yangu iliyopo ni kwamba Maamuzi ya Rais bado yanawanufaisha wapinzani na sidhani kama alichokichagua Rais ni lessor evil Bali naona amechagua greater harm upande wake. Angemtumbua Makonda mbali na kwamba wapinzani wangejisifu kuwa wameshinda lakini angeokoa niliyoyataja huko juu na angeonekana msikivu na mtenda haki kuliko sasa waliokuwa hawaamini kwamba hashauriki wameshaanza kuamini
 
sidhani kama saga la makonda ni mtandaoni tu, magazeti na redio sasa zinasema na kujadili
 
We muache aweke pamba masikioni.... Mwenyekit wa kamat ya bunge na makam wake wa viwanda na biashara wamejiuzulu..... Atatuelewa tu
 
Approach nzima inayotumika dhidi ya Makonda si nzuri maana imekaa kiudaku udaki na kulipiza kisasi.

Halafu watu wanapoanza kudokeza kuwa Magufuli na Makonda ni mashoga...halafu hapo hapo wanamtegemea Magufuli eti amtumbue Makonda!

Mtu mnamtukana halafu hapo hapo mnamtegemea afanye jambo la kuwafurahisha...come on now.

Wrong approach.
Kwahiyo na Lugumi ni wrong aproach? nyinyi Wasukuma mnatuona wote ni kama maboya tu.

Mlevi anaweza kuongea kitu cha maana lakini katumbuliwa ila mhalifu kama Daud Bashite anakingiwa kifuwa hivi unategemea watu kama Mange wasemeje?
 
Kwanini Makonda Atumbuliwi....


Makonda kila tarehe 15 ana shughuri maalumu anaenda kuifanya pale kivukoni,

Makonda anawapeleka na kuwarudisha wataalaum

Makonda ndio anajua ufundi mzima Wa kumplease mkuu (Sio uhusiano Wa kimapenzi)

Mengine tuwek akiba
 
Swala si kutumbuliwa mtu, Daud Albert Bashite anapaswa kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kufoji, otherwise Rais awarudishe kazini wote waliopoteza kazi serikalini kwa sababu ya vyeti.

Hilo la mahakamani nani alikuwa wa kwanza kulizungumzia humu?

Lakini niliishia kubezwa na kuitwa kila aina ya majina.
 
Hamjuwi mnachoongea mtoa thread na hao wote mnaosupoport. Unapokuwa kiongozi, unaongoza kwa mujibu wa katiba na matakwa ya wananchi. Rais kikatiba anapaswa kufuata sheria. Akishindwa kufata sheria hapo ndipo wananchi huingilia kwa kupaza sauti kumshinikiza afate sheria. Kama kiongozi ni mvunjaji wa sheria, lazima atakuwa ni kiongozi wa kutumia ubabe. Ni kiongozi mbabe anaweza thamini mtu mmoja zaidi ya mamilion kwa sababu tu anaamini ananguvu na hakuna cha kumfanya.
Duniani kote chief informants wa information zozote ni wananchi ambao Rais anawabeza. Usalama wa taifa wanapata taarifa kutoka kwa wananchi. Hii inamaanisha kwamba sisi kama raia tupo sahihi kwa kile tunachokifanya. Lkn kwa kuwa tumempa nguvu zote Rais bila tukasahau kuwa tunawajibu wa kumdhibi, na yeye akajuwa kuwa hatujuwi Wajibu wetu, ndo maana anafanya anavyofanya. Anasahau kuwa kila siku anasema yeye ni Rais wa wanyonge, Rais wa watu, yupo kuwatumikia watu, kumbe anamtumikia Makonda.
Waingeleza wanasema, "birds of the same feather, flocks together" Kwa kuwa yeye manyoya yake hayafanani na yetu wananchi, wanyonge, ambao ndo kila siku hulalimika kwenye mitandao, ni ngumu kukubaliana nasi. Tuendelee kupaza sauti, siku moja tutayaona matunda ya sauti yetu.
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Si kwamba watu wanataka raisi afanye wao wanachotaka ila hivyo ndo raisi anatakiwa afanye

Ukimya wake ndo unaozua matusi,kejeli na kashfa zote hizo while wengine aliwatumbua hadharani tena ni ndani ya dkk tu baada ya kubaini makosa yao iweje bashite bado anaendelea kuyoyoma tu unataka watu wa react vp!!
 
Kwahiyo na Lugumi ni wrong aproach? nyinyi Wasukuma mnatuona wote ni kama maboya tu.

Usukuma unahusu nini sasa hapo?

Mimi ni Msukuma na si shabiki wa Magu, Makonda, wala Gwajima.

Halafu kama ishu ingekuwa Usukuma basi bifu na Gwaji na Mako wala lisingekuwepo.

Acheni kuingiza ukabila sehemu ambapo hata haupo.
 
kwa hiyo mkuu hata kama bashite angeua mtu na ikathibitika. na mitandao ikashinikiza bado mtukufu asingemtumbua?? yeye mtukufu hataki kushinikizwa mbona hakuna aliyemshinikiza hili ni swala lipo wazi kabisa
 
Wengi wanao pambana na Makonda walikosea target kabisa kabisa
Na tatizo kubwa la CHADEMA, Wanatumia nguvu na uwekezaji mkubwaaa kupambana na Makonda ambaye siyo mwanasiasa na wala hagombei 2020. SUBIRIA Watakavyopokea PIGO LA HAJA 2020 Ndo watakufa kabisa
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Mkuu ni rahisi kutukana kama ulivyofanya wewe..
Mimi nionavyo mpaka sasa upinzani wana goli tatu mkuu na timu yake wana ZERO. huhitaji kuwa mwanasiasa kuliona hili
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyonyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
Kutoka 10:1
. Bwana akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionyesha ishara zangu hizi kati yao;

Kutoka 10:2
. nawe upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana.

Kutoka 10:3
. Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
 
Bashite alipewa go ahead na mamlaka ya juu, Siyo kwamba alikurupuka tu.Ngosha hawezi kumtumbua ngosha mwenzie.
 
Back
Top Bottom