Safari yangu ya dhahabu Botswana

Safari yangu ya dhahabu Botswana

Nimekaa mivinjeni kalibu na sehemu wanaita pound kama sikosei miaka 2005 asikwambie mtu yaani mabraza wao kalibia wote walizamia na wanawake wao walienda kwa ndege mitaa ya wanyakyusa
 
Keko machungwa miaka ya 90 kulikuwa na kijiwe kimoja kinaitwa "Saa ya kula" yaani watu walikuwa wanazamia sana, wengine wanarudi na magari yao yale Peugeot 504 na 404. Watoto wa kota za polisi na huku uraiani enzi hizo waliiuwepo akina marehemu Bosco a.k.a Cool Jay
 
Huu uzi ulipaswa kuisha kwa episode 2 au 3.
Isipokuwa anachofanya mwandishi ni kuingiza maelezo mengi ambayo siyo ya lazima sana.

Mfano angalia episode ya 1 na 2, akitaja eneo la hapa Bongo mfano mwenge mataa anataka elezee hapo mwenge mataa kuna nini, aelezee mpaka wauza magazeti hapo,,aelezee mama lishe, aelezee vibaka, haya yote ni kurefusha stori.


Issue ni safr anapaswa kunyoosha safr ilivyokuwa basi, lakini asilimia 95% ya maelezo yanazunguka hapa hapa bongo tu.

Endeleeni tu hizi tabia za kuanzisha uzi kupima upepo Mungu asaidie huu uishe salama.
 
Huu uzi ulipaswa kuisha kwa episode 2 au 3.
Isipokuwa anachofanya mwandishi ni kuingiza maelezo mengi ambayo siyo ya lazima sana.

Mfano angalia episode ya 1 na 2, akitaja eneo la hapa Bongo mfano mwenge mataa anataka elezee hapo mwenge mataa kuna nini, aelezee mpaka wauza magazeti hapo,,aelezee mama lishe, aelezee vibaka, haya yote ni kurefusha stori.


Issue ni safr anapaswa kunyoosha safr ilivyokuwa basi, lakini asilimia 95% ya maelezo yanazunguka hapa hapa bongo tu.

Endeleeni tu hizi tabia za kuanzisha uzi kupima upepo Mungu asaidie huu uishe salama.
Wazee wajuaji washaingia, kama unaona haukifai achana nao
 
Daah umenikumbusha huyu mwamba Jongo...alikua hatar sana yaani lile daraja la sava kuruka na madumu mkononi duhh...
Mwamba alipigwa kisu Cha tumbo akawa anakimbia utumbo kaushika mkononi...

Ugimbi siku hzi umejengwa na majukwaa unayo
Duh huyo mwamba alipona mkuu? 🤔🤔
 
Hiyo nafikiri ilikuwa staili yao ya nitoke vipi( kumbuka kasema hata stori za vijiwe zilikuwa na ushawishi katika maamuzi yao).

Mkuu kisa neno "jamaa" unataka kunipasua, sijamaanisha asee ulikuwa utani. Hope mzima first born.
Jamani firstborn siwezi kukupasua bana, ila nilikua nakutishia tu kidogo ujue uwepo wa firstborn 😀😀
Niko poa vipi wewe?
 
Kama ilivyo kwa wengine wapenda kusafiri kama mimi, daima tunapenda ku- share some stories na watu wengine ili nao angalau wapate kidogo mwanga wa maisha ya sehemu nyingine za mbali kidogo na nyumbani Tanzania.

Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na wimbi kubwa sana la vijana wa kitanzania kutamani kuondoka nchini na kukimbilia nchini Afrika ya kusini almaarufu bondeni kwa wakati huo. Nakumbuka sikuwa muhanga wa matamanio hayo yaliyokuwa sehemu kubwa ya vijana vijiweni kote huko, kuanzia temeke hadi kinondoni.

Nakumbuka rafiki zangu wengi tuliokuwa tukikaa pamoja pale maeneo ya Abbas club kama sikosei wakati huo miaka ya 2000 mwanzoni kabisa. Enzi za uwanja wa ugimbi na vita vya marefa na mashabiki...acha kabisa yaani, ukitoa matumizi ya bange kulikuwa na kubeli zilizotumiwa bila idadi maeneo hayo ya pembezoni mwa viwanja hivyo vyenye mchanga kibao. Kwa wakaazi wa kurasini, maeneo yote ya keko, zamkago kule na beach yetu pendwa ya Sava mtakuwa mnanipata vyema hapa.

Basi kipindi ndio safari za magendo zikiwa zimepamba moto huku waliokuwa washkaji kipindi hicho, maana kama kuna waliopo hai wakati huu wa sasa sio vijana tena. Mipango mingi ya kutafuta pesa za nauli za safari ilikuwa ikifanyikia nyuma ya kuta za bandari...aisee wizi wa mafuta ulipamba moto kweli kweli, kuna jamaa mmoja maarufu miaka hiyo aliita Jongo.

Kwa sasa ni marehemu kama walivyolala washkaji wengine wengi tu waliojihusisha na maswala ya wizi wa mafuta na vitu mbali mbali, kama unamfahamu Jongo na habari zake saluti kwako mkuu.

Huyu jamaa na genge lake walikuwa ni watu wakukaa nao mbali kabisa. Wakati mwingine unaweza kusema ni bora kushirikiana na wachuna ngozi wa mbeya huko kuliko hao jamaa.

Acha. Tusonge mbele sasa, baada ya vijana wengi kunogewa na habari za south na baadhi ya nchi nyingine za ulaya, ndipo safari za kuzamia meli zikaanza kwa Fuji sana na bila mpangilio na plan nzuri.
Nakumbuka kuna jamaa kadhaa waliobahatika kuzamia meli na hatukupata tena habari zao tena, hatujui kama walifanikiwa kufika walipo kusudia au la.

Kuna waliopitia njia za barabara kuelekea south Afrika ambapo ndio nchi pekee pendwa zaidi wakati ule.

Baadhi walizamia omani na kutokomea huko huko hadi hii leo tukiwa tunakisubili kwa hamu kimbunga chetu Jobo sijui nani.
Sasa wakati huo nchi kama Msumbiji, Kenya, sijui Uganda na huu upuuzi mwingine wote wa Afrika mashariki na kati sijui kama vijana walikuwa wanazifahamu kama zipo duniani hapa. Issue kubwa ilikuwa bondeni, Ulaya au angalau Arabuni kidogo kujipanga na kisha kuingia nchi za ulaya, na hata South Afrika ilikuwa ni kama njia tu au kituo cha kuelekea Italian, Finland, na kwingineko huko mbele kwa mbele.

Kwa upande wangu nilikuwa mwoga sana na ikizingatiwa makuzi na mazingira ya nyumbani yalivyokuwa. Maana kulikuwa na matabaka ya vijana kati ya watoto wa kota, watoto wa changanyikeni huko keko machungwa, keko mwanga, Tandika na viunga vyote vya wilaya ya Temeke (TMK) wilaya yetu ngumu na ya wagumu haswaaa.
Mwanzoni sikuwa na mawazo ya kusafiri nje kabisaaa, kwangu ilikuwa ngumu sana kushiriki katika mipango na plan za kutoroka nyumbani huku ukiwa umewaachia hasara kubwa ya wizi wa fedha, deki VHS kwa wale mnaozijua, TV Hitachi ya chogo, na vikorokolo kibao ilimradi tu upate kianzio cha safari.

Mwishoni mwa miaka ya 1999 kuelekea 2000 hivi kipindi kama sikosei ndio watu wengi wanaanza kumiliki simu za mkononi na zile vocha zetu pendwa zilizoitwa Dollar. Zilikuwa mtindo wa karatasi hivi, unalichana katikati na tarakimu unazikuta ndani kisha mkononi una Nokia yako kubwa 30410 jeneza full vibration, au Philips kidole juu.

Basi baada ya stori nyingi za marafiki waliofanikiwa kuescape manyumbani kwao kutufikia kuwa wanakula bata mbele huko, ndipo na mimi nilipo amua kujilipua na kuondoka na jamaa zangu wawili.


(Tukutane leo jioni hapa hapa)
Angalia virusi huko kwa akina Makirikiri ,totoz za huko hujiachie bure bila sababu.
 
Back
Top Bottom