Safari yangu ya dhahabu Botswana

Safari yangu ya dhahabu Botswana

Habari za jioni wakuu, na samahani sana kwa kuchelewa sana kurudi hapa jukwaani. Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam watakuwa wananielewa ninaposema foleni zinazosababishwa na maboresho ya barabara zetu ndizo zilizochangia sana kuchelewa kwangu hapa.

Pia napenda kuwatia moyo ya kuwa tutakuwa hapa pamoja hadi mwisho wa habari hii, ijapokuwa wakati mwingine mnapaswa kumvumilia mleta habari yeyote kwa kuchelewa kwake kwa sababu nature ya maisha yetu hapa nyumbani Tanzania mnaijua. Mara nyingi muda unakuwa kikwazo zaidi kuwasilisha habari kwa wakati.

Tunaendelea..... Tulipanga safari tukiwa watu watatu pekee, na safari yetu tuliazimia kwenda mjini Gaborone.
Chaguo letu lilikuwa moja tu, yaani kufika Gaborone tu. Katika safari yetu tulikuwa vijana wenye makamo sawa na hata elimu na shule tulio soma ilikuwa moja.
Sitaweka majina wazi hapa lakini mmoja alikuwa anatokea sehemu moja inaitwa Mivinjeni, pale karibu kabisa na kilipokuwa kituo cha mafuta cha BP, nadhani wanao ifahamu vyema barabara ya kilwa road kupitia ufundi wananipata vyema.
Jamaa wa pili huyu alikuwa anakaa sehemu moja inaitwa shimo la udongo huko, karibu na msikiti hivi kama upo siku hizi, maana nasikia bomoa bomoa ilipita maeneo hayo. Kwa miaka ya nyuma kidogo maeneo hayo yalikuwa yamechangamka sana, na pia wote kwa pamoja enzi za makuzi ya utoto wakati huo tukiwa tunatumikia kanisani katika kanisa la Mt Maurus hivi kama sikosei, hili ni kanisa katoliki lililopo maeneo hayo karibu kabisa na polisi ballacks. ( Kwakweli nakumbuka mambo yanayo nifanya nihisi zaidi taabu na huzuni wakati huu, Nakushukuru Mungu kwa uzima na afya hadi wakati huu.)
Mtu wa tatu ni mimi mwenyewe, mtoto wa kota, mtoto wa mama wakati huo, kiukweli maeneo hayo kulikuwa na kota nyingi za mashirika mbali mbali. Kwa wenyeji ebu twende pamoja na kama nitakosea mtasaidia kuweka mambo sawa. Kuna kota za polisi, bandari, lililokuwa shirika la reli wakati huo TRC, na nyinginezo.
Sasa nilikuwa mmoja wa watoto wa maeneo hayo, nikizaliwa hapo, kukua na kusoma hapo kati ya shure muhimu na zenye mafungamano na jeshi.

Kila mmoja alifanya maandalizi yake binafsi na tulipojilizisha ya kuwa sasa tunaweza kumudu safari ndipo tukakaa chini na kuwaza ni wapi tutaanzia na kumalizia. Wakati huo ndipo tulipo amua kuzamia Botswana.
Lengo la kwanini ilikuwa Botswana na sio Afrika ya kusini ilikuwa ni kwa sababu yule mwenzetu mmoja ana mjomba kule, na mama yake huyo angeweza kutushika mkono hadi pale tutakapojiweza na kuendelea na safari kama ilivyokuwa kwa vijana wengine wengi walivyotamani.
Kwa kweli tulihofia sana maisha ya south na ndio maana tulitazamia kuwa Kule Gaborone tungeweza kujipanga vizuri na ikiwezekana tuunganishe safari huko huko kuelekea nchi za ulaya tusizozijua abadani.
Kitu muhimu tulichozingatia ni jina la mwenyeji wetu asiekuwa na taarifa za ujio wetu, pia jina la mji wa Gaborone, njia tutakayopita na ujanja ujanja mwingi kweli kweli wa kukwepa vizingiti tutakavyokutana navyo mbele ya safari huko. Hayo yote tuliyapata vijiweni wakati tukishauriana namna bora ya kuweza kuvuka mipaka kienyeji, niseme ukweli kulikuwa na vijana wenye uwezo mkubwa wa kushauri wenzao upumbavu na wakaufuata bila kufikilia.

SIKU YA KWANZA YA SAFARI.

Kama unge bahati kukutana nasi usingehisi chochote kabisa. Tuliamu kutoweka manyumbani kwetu kipekee sana. Kwanza tulipanga kuwepo mjini kwa siku tatu mbele bila kuondoka, yaani tuangalie upepo wa waliobaki kututafuta huku nyuma.
Binafsi sikubeba kitu chochote zaidi ya pesa na ilikuwa t-shirts ya fubu kitu kama hicho, yenye mikono mirefu na chini nilivaa suruali flani hivi siku hizi sizioni sana, zile ambazo ilikuwa ukiamua unafungua zipo zilizowekwa magotini kisha inakuwa pensi, au unaunganisha zipu kisha inakuwa suruali kamili. Pia ilikuwa na mifuko mingi hivi. Hivyo ndivyo nilivyotoka nyumbani siku ya mwisho.
Wenzangu pia walikuwa kama mimi, japo nguo hazikufanana lakini wote hatukuwa na mzigo wowote zaidi ya vijisenti tu vya safari tuliyoipanga kuianza kesho kutwa yake.
Wote kwa pamoja tulikutana malindi chini kabisa kule kwenye njia ya treni na safari ya kuelekea kariakoo kidongo chekundu ikaanza. Njiani tunapisha na ndugu jamaa na majirani kana kwamba tunaenda posta kushangaa maji kumbe ndio safari hiyo.
Tulifika kidongo chekundu, maeneo ya gerezani pale, kisha tukaangalia utaratibu wa kupata usafiri wa magari ya mizigo kama upo. Tunashukuru kwa msaada mkubwa wa jamaa yetu mnunua mali za magendo na vyuma chakavu pamoja na siso, shaba, copper na dalali mkubwa wa enzi hizo wa Mali za wizi alituunganisha kwa jamaa fulani hivi watu wa nyanda za juu kusini huko waliokuwa wanasubili kupakia mzigo na kusafilisha kwenda Iringa mjini. Wale jamaa ilikuwa hawana siku maalumu ya kuondoka pale na sisi tuliitaji kutokomea mjini baada ya siku tatu kupita. Maana tulikuwa bado tunapima upepo kwanza.

Baada ya kupeana miadi ya lini lile gari litaondoka pale na tuliwakabidhi kiasi kidogo kama kishika uchumba wa safari ndipo tukaingia mjini sasa. Aisee pale mnapopandia mabasi yenu ya mwendokasi hapo gerezani terminal enzi hizo mtu aliweza kula bata la kati hapo vibaya mno, kariakoo ya zamani haikuwa ya kitoto kabisa, maana kuuziwa pea tofauti tofauti za viatu ilikuwa kawaida sana, michezo ya kitapeli kila kona na mengine mengi sana. Wakati huo maeneo ya buguruni tulikuwa hatuyafahamu kabisa yaaani.. Nakumbuka tulikuwa tukikaa juu gholofani usiku tunaona kwa mbaali sana lile bango lililopo pale tazara juu kwenye majengo ya baharesa lililoandikwa Azam.
Miaka hiyo ilikuwa unaweza kuliona jengo la Azam tazara pale kutokea kota za kurasini kule.
Majengo marefu yalikuwa machache mno ukanda huo.
Basi katika siku hizo nne tulizo zamia town ilibidi tufike maeneo ya buguruni kushangaa shangaa, maana mimi nilizani kule kulikuwa ndio mwisho wa mji kutokana na sisi kuzoea kila siku kusikia honi za meli na milio ya bunduki bandalini huko wakati wakina jongo wanapambania mafuta ya wizi na vitu mbalimbali.

( Subili mwendelezo)
 
Tupia kengine ka mwisho kwa siku hii ya leo brother
 
Mwendelezo leo au kesho??
 
Back
Top Bottom