Safari ya kushtukiza kwa mpenzi

Safari ya kushtukiza kwa mpenzi

Ushawahi kufanya/ kufanyiwa safari ya ghafla na mpenzi wako bila kukitarifu juu ya ujio wake.
Je ilikuwaje na ulikuta nini?
Mi nilifanya siku moja nikakuta anacheza rede na wanaume wa dar wala sikumfiria au kuwawazia vibaya wale jamaa juu yake maana nilijua kabisa hawana madhara kwake
 
Siendagi kwa watu bila taarifa. Labda anipe funguo yangu. Nilimshtukiza ex bf tu. Nilienda mkoa aliokuwepo kwa issues zangu nikaenda sehemu yake ya biashara kumsalimia na sikumkuta alienda kwenye msiba kijijini. Nikafanya kilichonipeleka nikasepa.
Zaidi ya hapo bado sijaingia na huba la kumsurprise kiumbe mwingine
Geita uko
 
Hazifai hizi kitu.Kuna mmoja alimuaga mke wake anasafiri kikazi kumbe uongo lengo aje asuprise akasubiri usiku mnene ndio akarudi kufika anagonga geti kaja kufungua mdada wa kazi anauliza mama yuko wapi anaambiwa katoka toka saa kumi Alasir. Hebu wazia hapo kilitokea nini. Safari za kushtukiza ni hatari sana kwa Afya.
[emoji1] [emoji1] kama una presha, unadondoka unakufa
 
Nilirudi safari bila taarifa. Nilipoingia ndani cha kwanza nilichofanya nikuchukua simu yake na kutoka nje nikamfungia ndani. Niliendeleza charting zake alipoishia na nikamwita aliekuwa anachart akaja tukaonana tukaelezana ukweli nikarudi ndani tukalala asubuh nikampeleka Ubungo nikamrudisha kijijini kwao. Nasikia karudi tena mjini ila sijawahi onana nae tena
Safi,tunafanana misimamo. Hamna kuremba ni kumsafirisha tu ulipomtoa. Habari inaishia hapo
 
Jamaa alimtembelea mpenzi wake we chuo bila taarifa akamfumnia na mwanaume mwingine Demu akamgeukà jamaa kamwitia mwizi wananchi wakapiga wakaua sasa nyie Endeleeni Kusaprise ipo siku mtakiona Pia kwa mwanaume aliyekomaa kifikira huwezi kumshtukiza mpenzi wako unataka nini? Kama si Ushamba wewe unafanya vingapi?
 
[emoji1] [emoji1] kama una presha, unadondoka unakufa
Umeonaeee. Unaweza kuta alikuwa na hisia mbaya kwa mke wake ila si kwa kiasi alichokutana nacho sababu kamkosa na kumkosa.
 
Jamaa alimtembelea mpenzi wake we chuo bila taarifa akamfumnia na mwanaume mwingine Demu akamgeukà jamaa kamwitia mwizi wananchi wakapiga wakaua sasa nyie Endeleeni Kusaprise ipo siku mtakiona Pia kwa mwanaume aliyekomaa kifikira huwezi kumshtukiza mpenzi wako unataka nini? Kama si Ushamba wewe unafanya vingapi?
Aiseee. Hiyo mbaya sana.

Tatizo watu wanapenda kulazimishia makosa na ndio sababu yanatokea yote hayo. Na hapo kwenye red unakuta yeye ana mabaya mengi tu.
 
Aisee ni kama kamari ukidhamiria kufanya hivyo lazima uwe tayari kwa matokeo utayoyakuta

Binafsi siwezi na pia sitaweza kujaribu
 
Haya mambo haya, shida tupu tulio nje tunatamani tuingie na walio ndani wanatamani watoke[emoji4] [emoji4]
Nyie wa nje muingie tu hao wandani wanatishia nyau sababu kuiacha ndoa si jambo jepesi Mkuu. Labda mtu yamfike hasa.
 
Back
Top Bottom