Safari ya kushtukiza kwa mpenzi

Safari ya kushtukiza kwa mpenzi

Surprise nzuri ni kama hizi: Weka mzigo wa kutosha kwenye simu kisha fanya muamala kwa mwenzio(mke, mpenzi, mchumba au rafiki) asilimia kubwa lazima watafurahi na kuchangamka hata kama walikua wameboreka watakaa sawa na hawatasahau hiyo kitu kwa muda mrefu sana

Pia waweza mpigia simu mwenzio umuite mahali umnunulie hata kizawadi cha handbag au basi hata kula ice cream pamoja, lakini surprise nyingine ni za kubomoa na sio kujenga

Kuna watu wengne wanakua na hasira tu na muda wote wanatafuta madhaifu ya wenzao ili wawachukulie hatua! Sasa ni mapenzi gani hayo ya kuviziana Shadeeya ?
Kama hujaoa mimi niko single mwaya
 
Suala la mapenzi haliitaji hofu,kama una mashaka au hofu na muhusika achana naye tu
Kabisa mkuu, mpe dharura mwenzio...yaani wakati wote jitahidi uwe na mawazo chanya juu yake

Akichelewa kurudi kazini usimdhanie tofauti, weka fikra zako kua alikua na kazi nyingi au foleni, kama hakupokea simu jiaminishe kwamba alikua mbali nayo, kaa mbali na simu yake na muonyeshe mapenzi wakati wote, juu ya yote na wewe mwenyewe uwe msafi wa matendo na nafsi
 
Mtu akija kwangu kwa surprise hata kama sina ishu nitasingizia nina safari natakiwa kuondoka. Na mimi pia hua siendi kwa mtu ghafla ghafla.
 
Nimesha fanya sana, tena usiku namkuta amelala
 
Nilikuhurumia tu kiubinadamu, lakini ungejuta kuzaliwa kutembea usiku kisa unataka ufumanie. Siku ukirudia utaisoma namba. (Anajijua)
 
Nilirudi safari bila taarifa. Nilipoingia ndani cha kwanza nilichofanya nikuchukua simu yake na kutoka nje nikamfungia ndani. Niliendeleza charting zake alipoishia na nikamwita aliekuwa anachart akaja tukaonana tukaelezana ukweli nikarudi ndani tukalala asubuh nikampeleka Ubungo nikamrudisha kijijini kwao. Nasikia karudi tena mjini ila sijawahi onana nae tena
Aisee ulikuwa jasirii khaaa...
 
Nilikuwa nafanya evening walk nikajikuta nimetokea kwa huyu manzi. Kwanza kufika nikapokelewa na viatu vya kiume mlangoni, kugonga akatoka akiwa na usingizi akaniambia kuwa, 'wamelala'. Sikuwahi tena kukanyaga kwenye ile nyumba.
Haa ha ha...noma
 
Back
Top Bottom