Kuhudhuria Rais mahali inategemea na ratiba zake, bahati nzuri kifo cha Kanumba kimetokea at a right time kwa yeye kuhudhuria. Hebu jamani niambieni, ndugu zako wote waliofariki ulihudhuria misiba yao? Inawezekana misiba mingine ilikuwa ni ya watu wa karibu zaidi ulishindwa kuhudhuria kwa sababu moja au nyingine lakini ile ambayo haikukugusa uliweza kuhudhuria. Kumbuka msiba huu umetokea wakati wa Pasaka ambao nina uhakika karibu dunia nzima walikuwa mapumzikoni (ukiacha sekta muhimu). Kila mtu ana kitu chake anachoona ni muhimu kwake (Priority) sio lazima kitu muhimu kwako kiwe muhimu kwa mwingine. Kwa kuamua kuacha kwenda mapumzikoni akaamua kwenda msibani, ilikuwa ni muda muafaka kwani hakuwa amepangiwa shughuli nyingine. Acheni wivu na madonge.