Kwanza wana JF wenzangu poleni sana na msiba wa Kanumba
Pili poleni kwa hang over, na pilau la Pasaka
Tatizo langu ni kushindwa kumuelewa huyu baba riz (JK), nimeona katika moja ya magazeti ya leo, kupitia mtandao kuwa ameahirisha safari yake ya nje ili kuhani kifo cha Kanumba, hilo ni jambo jema lakini halina weledi wala maslahi kwa taifa isipokuwa tu kama safari yake ilikuwa ni binafsi, nayo pia iwe haikuwa na maslahi kwa taifa.
Kumbukumbu zangu zinanionesha kuwa ni huyuhuyu baba riz aliyeondoka nchini wakati akiacha mgomo wa madaktari unaanza na maelfu ya watz kupoteza maisha,
ni huyuhuyu baba riz aliyeondoka nchini akiacha maafa kule arusha ambapo polisi waliua watu kwa risasi Jan 5 2011
na mengine kama hayo
sasa kama huyu ndo hivyo tanzania inaenda wapi? maslahi ya taifa yako wapi? weledi na uwajibikaji viko wapi?
J3 ya pasaka njema
kama ni kweli imekuwa hivyo' ni mwendelezo mbaya wa stori za mheshimiwa raisi!