Safari ya Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukansola, Sep 27, 2011.

 1. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ninapoandika habari hii, nipo safarini nikitoke Igunga, hii ndio imekuwa mara yangu ya kwanza kutembelea wilaya hii.

  napenda ku-share nanyi ndugu zangu kuhusu machache niliyojifunza katika siku mbili nilizoishi hapo. Nikianzia na hali ya hewa kwa sasa Igunga kuna joto kiasi. Jambo ambalo nimeliona pia ni kwamba maisha ya wananchi wa Igunga hayana tofauti sana na maisha ya wakazi wa wilaya zingine za nchi hii. Umeme upo lakini mgao ni kama sehemu zingine. Maji ya Igunga ni ya visima na ni meusi kusema kweli.

  Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa RA amewapa Igunga maisha bora na hata Mkapa kwenye kampeni alisema Igunga iko juu katika mkoa wa Tabora. Mimi napinga kwa sababu wananchi wa Igunga wamechoka tu, mji umejaa vumbi jekundu. Stendi mpya ya mabasi ni mavumbi matupu.

  Jambo lililonishanga ni kusikia kuwa kumbe Rostam hana nyumba Igunga na kuna sehemu nyingi za vijijini ambazo hawamji wala hawakuwahi kumwona Rostam, mwenyeji mmoja aliniambia Rostam hajawahi kulala Igunga hata siku moja, huwa analala Mwanza.

  Nikiwa nasubiri basi, nimepata fursa ya kupiga story na vijana pale stendi, inaoneka safari hii ccm haikatishi maana kusema kweli watu wamebadilika, wanasema wamechoka kudanganywa na hawaitaki ccm. wanasema ccm imeleta watu ili kuwapeleleza na kuwashawishi vijana kuichagua ccm lakini wamekuwa wakiwaambia waziwazi kuwa wameshachoka na wasipotezewe muda wao.

  Kuhusu Dr. Kafumu ni kuwa amejenga nyumba chapchap wakati wa kura za maoni ili kujionesha ni mwenyeji wa huko.

  Pembeni yangu nilimsikia mzee mmoja wa kike akiwauliza wazee wenzie wa kiume wawili aliokuwa akizungumza nao kwamba wao ni vyama gani? Yeye aliwaambia ni chadema hata wale wazee walimjibu hivyohivyo.

  Kwa mtazamo wangu kutokana na experiance yangu ya muda mfupi ccm huenda wakalikosa jimbo hilo. I've got some pictures of Igunga but can't attach them cause am using a phone.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  ahsante mkuu lukansola kwa kutushirikisha uzoefu ulioupata igunga. mkuu ulijaribu kufanya ka utafiti kadogo juu ya hizi jezi za ccm, wananchi wa igunga wanaziheshimu, au wakimuona mtu kava sare hizo wanamuhusisha na rushwa, kama hakutaoa basi kapokea! ingawa hivyo tunakutakieni safari njema.
   
 3. M

  Mlabondo Senior Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 140
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lets hope chadema wins, for our own benefit we need More opposition MPs to make the government deliver
   
 4. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nilimtania kijana mmoja aliyekuwa amevaa T shirt ya kijani, akaniambia kaka hizi tuavaa tu, kwa kifupi watu wengi sana wanaonesha kuchoka na ccm. Pia nimekumbuka Igunga kuna ATM moja tu na haichukui Visa Card, mitandao ya mawasiliano kama simu na intenet pia ni dhaifu sana. Jogi kwa mtazamo wangu kama uchaguzi ukiwa huru na haki... Mmmmhhh.
   
 5. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye red, kujenga chap chap ni within how many days or weeks, tangu msingi hadi finishing? Ina maana Kafumu kama huko ni kwao hakuna nyumba ya wazazi wake hapo kijijini kwao hata ahitaji kujenga nyumba chap chap ili kujionesha ni mwenyeji wa huko?
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hukupata "bahati" ya kukutana na Malaria Sugu? Yupo huko tangu last week akigawa t-shirt na kofia za ccm. Nimeona na Ritz1 nae akiandika kuwa tar 3 atapitia Moro akitokea huko!
  Ulipata bahati ya kushuhudia mkutano wowote wa kampeni huko. Kama ndiyo, how was it!?
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Watawala dhalimu hawatadumu milele..
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu hao wajakazi wa nape wamekwenda igunga kwenye keyboards, kama bosi wao mwenyewe amepigwa marufuku kukanyaga igunga sasa wao watapataje nafasi ya kwenda huko?
   
 9. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Niliona uzi wake akisema yuko Igunga nikamwambia tukutane tupige story akaniambia anaogopa tindikali.
   
 10. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Honestly kwa hali niliyoiona huko ni kwamba ccm hawana chao, mpaka wazee wana support cdm kwa sasa.
   
 11. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mama Mdogo kwa taarifa yako hata RA hana nyumba Igunga, this means hakuna mtu anayejua kwa RA ni wapi igunga.
   
 12. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Katibu mwenezi amenyimwa fursa ya kueneza.
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160


  How!? Anaogopa tindikali wakati ameibeba! Alisema anakwenda kuimaliza kabisa cdm huko, nikajua yupo full equiped!
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ameogopa hata kurudi dar! Utamsikia mara yupo serengeti, mara yupo Mara, mara yupo Mwanza. Nadhani "anaeneza" moja kwa moja kutoka kanda ya ziwa!?
   
Loading...