Moderator! Kama unavyojua raisi wetu Jakaya Kikwete kila kukicha safari za kwenda nje ya nchi haziishi. In average anasafiri at least kwa wiki mara moja kwenda nje ya Tanzania. Cha ajabu kila taarifa ya safari ya huyu bwana mkubwa ikianikwa hapa jamvini immediately umekuwa unaitoa ama unai-combine na threads za safari zake za nyuma. Kwa nini usiache kila thread yenye safari yake ijitegemee?
Mfano: Jana hapa jamvini iliwekwa thread ya JK kuelekea Namibia next Monday, tayari umeshainyofoa jamvini na kui-combine na threads za nyuma. Kwa nini usiache kila safari iwe na thread yake hata kama hizo safari zitafika 1,000,000????
Ama hamtaki mkuu wa nchi kuambiwa ukweli kuhusu safari za nje ya nchi zisizoisha wala kuwa na tija?
Nawasilisha