Mtu anayetetea Saddam hakujua wala kusikia uovu wake. Saddam alikuwa mwuaji nambari moja. Wakati wake ukishukiwa tu kuwa mpinzani unakufa, tena unakufa kifo kibaya. Kuna mama mmoja, Binti al-Huda, Shia, aliandika tu kwamba Iraq inafaa iongozwe Kiislamu. huyu mama aliuawa kifo kibaya sana. Alilazimishwa kukalia chupa ilivunjwa kwenye shingo yake. Hebu fikia mauaji kama hayo. Na mengine mengi ya kutisha ikiwemo watu kuyeyushwa kwenye mapipa ya acid. Saddam aliamuru kuuawa kwa maelfu ya Wakurdi kwa silaha za kemikali wakiwamu mamia ya watoto wasio hatia yeyote.
Alianzisha vita dhidi ya Iran kwa kuona angeweza kushinda Kirahisi na kuigawa Iran. Wakati wa vita hiyo nilikuwa Iran, mabomu ya masafa ya mbali yalikuwa yanalengwa makusudi kwenye nyumba za raia usiku wa manane. zaidi ya raia 70,000 wa Iran waliuawa kwa njia hii. Hii ni vita aliyoianzisha bila sababu za msingi, kiasi kwamba siku chache kabla hajaivamia Iran Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran alikwenda kumwomba kama kuna matatizo yeyote wayasuluhishe kwa amani. Muda alipoondoka tu akaanza vita. Mtu wa namna hiyo anafaa hata kuombewa? Kama kungekuwa na adhabu kubwa zaidi ya kifo angestahili mbwa yule mkatili na mwovu- pure evil.