Saddam Hussein Alikuwa Akitetemeka Siku Aliyonyongwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Mtandao wa WikiLeaks umeendelea kutoboa siri za Marekani kwa kuelezea jinsi Saddam Hussein alivyokuwa akitetemeka kabla ya kunyongwa na jinsi maafisa wa Iraq walivyokuwa wakimtukana Saddam na kuchukua picha na video za kunyongwa kwake.
Kwa mujibu wa nyaraka mpya za siri za Marekani zilizowekwa hadharani na mtandao wa Wikileaks, Aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein alikuwa akitetemeka kabla ya kupandishwa kwenye kitanzi disemba 30, mwaka 2006.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotumwa Marekani na aliyekuwa na balozi wa Marekani nchini Iraq, Zalmay Khalilzad kuhusiana na kunyongwa kwa Saddam Hussein, Saddam alionekana mwenye hasira na alikuwa akitetemeka kabla ya kunyongwa.

Taarifa hizo zilisema kuwa Saddam alipelekwa kwenye gereza alilonyongwa na helikopta ya jeshi la Marekani, jukwaa alilonyongewa lilijengwa na Marekani lakini utekekelezaji na usimamiaji wa kunyongwa kwake ulifanywa na serikali ya Iraq.

Saddam aliingizwa gereza hilo huku sura yake ikiwa imefunikwa kwa kitambaa huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma.

Mikono yake ilifunguliwa na Saddam alisomewa mashtaka yake mbele ya watu 13 walioteuliwa na serikali ya Iraq.

Alipoulizwa kama anahofia kufariki, Saddam alijibu "Sihofii kufariki, tangu nilipochaguliwa kuwa Rais nilijua kuwa marais huwa wana maadui wengi".

Baada ya kusomewa mashtaka yake, Saddam alimkabidhi msahafu aliokuwa akiusoma naibu Mwanasheria mkuu wa Iraq, Monqith al-Faroun na kumwomba aukabidhi kwa faimilia yake, al-Faroun aliahidi kuukabidhi kwa familia yake.

Saddam alifungwa tena mikono yake kwa nyuma huku miguu yake ikifungwa minyororo. Saddam alipandishwa kwenye jukwaa tayari kwa kunyongwa, alipokuwa akipanda kwenye jukwaa mmoja wa walinzi alisikika akisema "Nenda Motoni" na kumfanya al-Faroun awaonye watu kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kusema chochote.

Saddam alisali sala yake ya mwisho huku baadhi ya maafisa wa Iraq wakipiga kelele za "Moqtada, Moqtada, Moqtada" wakiashiria jina la kiongozi wa Shia, Moqtada al-Sadr aliyepata umaarufu baada ya kuanguka kwa Saddam.

Saddam alikataa kuvalishwa kitambaa cheusi kwenye sura yake na alifariki ndani ya muda mfupi baada ya shimo chini ya kitanzi kufunguka na kuufanya mwili wa Saddam uning'inie.

Mwili wa Saddam ulihifadhiwa na baadae ulioshwa na kuzikwa kwa misngi ya kiislamu.

Al-Faroun alielezea jinsi alivyoshuhudia maafisa wa Iraq wakipiga picha na kuchukua video za tukio hilo kwa kutumia simu zao ingawa ilikuwa ni marufuku kuingia na simu kwenye eneo hilo.

Picha na Video za kunyongwa kwa Saddam ziliingizwa kwenye internet na kusababisha mjadala mkubwa kuhusiana na jinsi Saddam alivyonyongwa.

Mtandao wa WikiLeaks ulimalizia kwa kusema kuwa serikali ya Iraq ililaumiwa kwa kuruhusu kuvuja kwa picha na video za tukio hilo.
 
Oh!maskini hakutendewa haki!alinyanyaswa !mungu amweke mahali pema peponi!!
 
Mbona tunaambiwa hiyo mashine ilifyeka kichwa mbali kiwili wili kikaanguka badala ya kuningi'nia?? au wazushi walitunga? it was a sad death i've ever heard. Bora wangemchoma sindano ya sumu.
 
Hata hao wasimamizi wa kimarekani walitaka haswaa picha za kunyongwa kwa Sadam Hussein ziwepo online, kwani waishindwa nini kuzuiya watu wasiingie na simu au camera!?
 
Sadam was the MAN Iraq will remember him for a long long time to come. Some of these Arab countries you need to be strong to lead them. Whats happening in Iraq now. Im telling you Sadam showed he was a man, wasnt afraid of being hanged, and mind you he said he dont want his face covered when heading to the gallows. Just imagine Bush receive the same verdict what will happen.
 
Hii inadhihirisha uharamia wa Merekani, hususan kwa waIslam.
 
Mtu anayetetea Saddam hakujua wala kusikia uovu wake. Saddam alikuwa mwuaji nambari moja. Wakati wake ukishukiwa tu kuwa mpinzani unakufa, tena unakufa kifo kibaya. Kuna mama mmoja, Binti al-Huda, Shia, aliandika tu kwamba Iraq inafaa iongozwe Kiislamu. huyu mama aliuawa kifo kibaya sana. Alilazimishwa kukalia chupa ilivunjwa kwenye shingo yake. Hebu fikia mauaji kama hayo. Na mengine mengi ya kutisha ikiwemo watu kuyeyushwa kwenye mapipa ya acid. Saddam aliamuru kuuawa kwa maelfu ya Wakurdi kwa silaha za kemikali wakiwamu mamia ya watoto wasio hatia yeyote.
Alianzisha vita dhidi ya Iran kwa kuona angeweza kushinda Kirahisi na kuigawa Iran. Wakati wa vita hiyo nilikuwa Iran, mabomu ya masafa ya mbali yalikuwa yanalengwa makusudi kwenye nyumba za raia usiku wa manane. zaidi ya raia 70,000 wa Iran waliuawa kwa njia hii. Hii ni vita aliyoianzisha bila sababu za msingi, kiasi kwamba siku chache kabla hajaivamia Iran Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran alikwenda kumwomba kama kuna matatizo yeyote wayasuluhishe kwa amani. Muda alipoondoka tu akaanza vita. Mtu wa namna hiyo anafaa hata kuombewa? Kama kungekuwa na adhabu kubwa zaidi ya kifo angestahili mbwa yule mkatili na mwovu- pure evil.
 
duh kumbe alikuwa mbaya hivi....naomba unipe habari zake zaidi huyu mtu......niko interested sana kumfahamu
 
Pamoja na kwamba Saddam lifanya ubaya, haitakiwa kabisa kulipa kwa ubaya, mweye kuhukumu ni mmoja tu,
 
Jamani tuacheni mambo ya ushabiki tuwe wakweli kama binadamu.

Hebu tujiulize Maswali yafuatayo.

Tangu Sadam amekufa Je Iraq imekuwa na amani ambayo marekani iliahidi?

Na je kati ya Sadam na George Bush ni nani aliyeuwa watu wangi na anayestahili kunyongwa.

Kwa wapenda haki na amani sidhani kama watashabikia namna walivyomfanya Sadam.
 
Saddam killed hundreds
Bush killed thousands

They are all killers regardless of numbers!!!!!

Mkileta ushabiki wenu wa magharibi na mashariki hapatatosha hapa, wote wauaji, ukisoma uuaji wa saddam utatetemeka na wananchi wake ndio walioshangalia!! wa Bush ndio huu wa sasa!! Bush may say have defence on those deaths, but he dont have enough reasons and evidence to fight with Iraq, he cooked story which is not there!!
 
mi binafsi niliridhika kabisa kuuawawa kwa yule mdudu.very gud bush!
 
Hii inadhihirisha uharamia wa Merekani, hususan kwa waIslam.

hii inadhihirisha uharamia na unyama wa uislam dhidi ya ubinadamu. Kumbuka ni watu wangapi waliouawa na sadamu kwa sumu, kukatwa kichwa ama kunyongwa wakati wa uhai wake. Wangine (kurdi) aliwaua kwa kisingizio kuwa hawatii uislam- muosha huoshwa.
 
Ninakuunga mkono hoja yako Mkuu. Saadam alikuwa mtu wa ajabu sana yaani kwake kila kitu anataka kiwe anavyotaka. Kama sijakosea yeye na watoto wake aliamuru timu ya taifa wote wauawe pindi walipofungwa na ujerumani mabao zaidi ya tisa bila shaka. Any way ni kwa jinsi gani hata kwenye michezo alipowatibua wapenda michezo kwani huwa siasa huwekwa kando kwani hata watoto wasiojua siasa basi tuwape nafasi na wao washangile maishe kupitia michezo yeye Saadam hata watoto kawachukia.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom