Hivi ndivyo Marekani alivyoiharibu Iraq

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Ni miaka 20 imepita sasa tangu marekani aivamie Iraq kwa kile kinachosemekana Saddam Hussein alikuwa anamiliki silaha hatari za maangamizi ,anafadhili magaidi pia alikuwa anatesa raia wake, hivyo marekani kwa kibali Cha UN ikafanya kitu alichokuwa anakitamani kwa muda mrefu.

Mambo yalianzaje
Mwaka 2001 September,11 marekani ilipata pigo kubwa sana kwa kumshambuliwa kwa world trade center na pentagon ,shambulio lililopelekea maelfu ya roho za wamarekani kufariki ni siku ambayo itakumbukwa kwa miaka yote na wamarekani
Screenshot_20230328-144051.png

Taarifa za kintelejesia zilionyesha waliohusika na shambulio hilo ni kikundi Cha wanamgambo wa al-kaida ambacho kilikuwa ya chini Osama bin laden.

Deputy secretary of state ikatuma memo kwenye kitengo Cha kupambana na ugaidi ,memo hio ilikuwa inasema wasiangalie tu Al Qaeda kwenye huu mkasa pia waiangalie na Iraq kwasababu iraq ni miongoni mwa inchi zilizokuwa uhasama mkubwa na marekani ,
Screenshot_20230327-142319.png
pia Secretary of defense alikuwa anaomba taarifa za kiintelejesia kuhusu matukio ya ugaidi inchini iraq , Na mtu aliyetuma hio memo si mwingine Paul worfowitz.
440px-Paul_Wolfowitz.jpg

Raisi George bush alikuwa ameketi na washauri wake wakijadili ni kwa namna gani watajibu shambulio hilo ,kikako kikiwa kinaendelea Paul worfowitz akanyoosha mkono aksema.

"Unajua Mheshimiwa raisi shambulio la 9/11 lilikuwa ni shambulio la hali ya juu sana (sophisticate attack), haiwezekani kundi la kigaidi kama al-Qaeda lingeweza kulifanya peke yao, bila shaka walipata msaada kutoka kwa Saddam huko Iraq."

Pia akaongezea kwa kusema linapokuja suala la ugaidi middle east Saddam ni kama kichwa cha nyoka yeye ndio mfadhili mkuu hivyo Kuna Kila Sababu Saddam yupo nyuma ya 9/11 .

Kila mtu mule ndani hakukubaliana na maneno ya bwana Paul akiwemo Joseph cofer black afisa wa CIA ambaye alikuwa The head of the counterterrorism center, akanyoosha mkono na kusema

"Tumeshambuliwa 9/11 na Osama bin laden na kundi lake la Al-qaeda , Saddam hausiki kwenye hili"

Black_jcofer_sct.jpg

Kikao kikaisha bila kukubaliana na taarifa alizotoa bwana wolfowitz .

Paul hakukata tamaa na report yake akaendelea kumshawishi George bush kuwa Saddam Hussein anamiliki siraha za maangamizi zikiwemo za nuclear na za kibiologia na anatoa ufadhiri kwa magaidi ambao wanamuunganiko na kikundi Cha al-Qaeda waliotushmbulia 9/11 hivyo Saddam anahusika kwa namna Moja au nyingine, Tumeshapata Sababu muhimu tuliyokuwa tunaitafuta kuangusha utawala wa saddam, safari hii George bush akakubaliana na report ya bwana Paul.

Mbegu ilyopandwa ikaota
George bush na serikali yake kwa muda mrefu ilikuwa inapingana na utawala Saddam kwasababu ni mtu ambaye aliyekuwa anatishia maslahi ya marekani kwa muda mrefu kwa kinachosemekana alikuwa na mpango wa kuacha kutumia dollar kwenye kuuza mafuta ,hivyo kwa muda mrefu marekani ilikuwa inatafuta Njia ya kuuangusha utawala wa Saddam ili kulinda maslahi yake.Na sasa amefanikiwa kupata Sababu ya kuingia Iraq.

Bunge la marekani likapiga kura juu ya uamuzi wa Bush kupeleka majeshi yake Iraq ,Karibia wabunge wote wa Republican walipiga kula ya ndio na kwa upande wa Democrats Nusu na zaidi ya wabunge walipiga kula ya ndio ,hivyo marekani akapata baraka kwa wabunge wake kuingia Iraq.

Report za kwamba Saddam anamiliki siraha hatari za maangamizi zinazotishia usalama wa middle east na Dunia kwa ujumla na kwamba anatoa ufadhili wa siraha kwa vikundi vya kigaidi ambavyo vikundi hivyo vinakuja kufanya mashambulizi kwa marekani ikwe lile la 9/11 na duniani kote zikawasilishwa UN.Ruhusa ikatolewa majeshi yaingie Iraq Kumng'oa saddam na yakatafute siraha za maangamizi bila kusahau kupeleka democracy.

Hapa marekani akafanikiwa kupiga ndege wawili kwa jiwe Moja kwanza 9/11 ikampa Sababu marekani kuingia Afghanistan pia report ya umiliki ya Saddam kumiliki siraha na kufadhili magaidi ikampa tiketi ya kuingia Iraq tena na backup ya kutosha.

Mwaka 2003 Marekani na uingereza na inchi zingine za NATO kwa kibari Cha UN wakaingia Iraq kusaka siraha hatari za maangamizi kama report zilivyokuwa zinasema ,majeshi ya Saddam yalishindwa kufua dafu mbele ya majeshi ya marekani hivyo utawala wa Saddam ukaangushwa na yeye akanyongwa.

Chuki na visasi

Kuundwa Islamic state.
Kuna baadhi ya watu wanailaumu marekani kwamba imehusika katika kuunda Islamic state kwamba marekani kwa namna Moja au nyingine anahisika katika uwepo wa Islamic state Iraq .Hivi ndivo inavyoelezwa kwa namna gani anahusika.

Baada kuangusha serikali ya saddam marekani akafanikiwa kuliweka jeshi la Iraq chini yake kwakua lile lilikuwa jeshi la Saddam marekani akaamua kulivunja na akaliunda upya jeshi, kitu kilichopelekea wanajeshi wa wengi kukosa kazi (waliachishwa kazi kwasababu walikuwa wanamuunga mkono Saddam) hivyo askari wengi walikuwa hawana ajira mtaani hivyo ikapelekea kutengenezwa vikundi vya kupambana na US kwasababu kwanza walikuwa na uzoefu na vita pili walikuwa na hasira na marekani kwa alicho kifanya kwenye inchi yao.

Huo naweza kusema ulikuwa ndio mwanzo wa IS ,mwanzoni walifahamika kama Al-Qaeda in Iraq wakaja baadae wakaitwa Islamic state in Iraq kule Syria hali ikawa hivyo hivyo kikaundwa kikundi kingine klijulikana kama Islamic state in Syria baadae kukawa na muunganiko wa vikundi hivi viwili vya Iraq na Syria ndio kinachofahamika hadi sasa kama Islamic State of Iraq and Syria (ISIS).

Inchini Iraq baada ya miaka kadhaa marekani akazidi kuikalia Iraq na kunufaika na mabilion ya Hela za mafuta ,vita vya wenyewe kwa wenyewe vikaiubuka ,umasikini ukashika kasi ,raia wakajigawa wapo walikuwa upande wa marekani na serikali iliyopo madarakani pia wapo walikuwa na hasira na marekani ikapelekea raia wengi kuendelea kujiunga na IS ili kupambana na marekani na serikali yao na wale waliokuwa wanyonge kipindi Cha saddam (Kurdish) baada ya saddam kuanguka wakawa imara ,Hali ya Iraq sasa haitamaniki wakurd wanapigana na Islamic state serikali huku nayo serikali inapigana na vikundi hivyo .

Bila uwepo wa marekani Hali isingekuwa mbaya namna hii, ni kweli hatukatai Iraq ilikuwa na machafuko kipindi Cha saddam lakini Tangu aingie marekani Hali imekuwa mbaya mara 50 ilivyokuwa kipindi Cha saddam .

Uongo na majuto.
Screenshot_20230328-203420.png

Gordon Brown aliyekuwa waziri mkuu wa uingereza wakati wa uvamizi wa Iraq akiwa kwenye mahojiano na kipindi Cha Good morning Britain amekiri na kusema pentagon iliudanganya ulimwengu kuhusu uwepo wa siraha Iraq na ilikuwa unajua kwamba sadam Hana siraha za maangamizi lakini haikutoa information zozote kwa washirika wake.

Pia Donald Trump anamlaumu mrepublican mwenzie Goerge Bush kwa kusema kwamba yalikuwa makosa makubwa kuingiza marekani Iraq , aliipeleka US Iraq kwa Njia ya uongo hakukuwa na siraha zozote hatari Iraq na alikuwa anajua hilo ,akasema pia binadamu tunakosea hivyo George Bush akubali alifanya kosa kupoteze Ma billions ya Kodi za wamarekani na kuangamiza maelfu ya roho.

Marekani aliingia Iraq kwa masrahi yake binafsi taarifa aliyotoa kwa UN ilikuwa ni ya uongo lengo lake hasa lilikuwa kumuangusha Saddam ili kulinda maslahi yake. Hakuna ushahidi wowote wa uwepo wa siraha za mangamizi Iraq uliopatikana, aliingia Iraq kufuata mafuta like always US does.

Takribani wairaq 300,000 wamepoteza maisha bila hatia yeyote na wamarekani zaidi ya 4000 wamekufa kwenye vita wasivyovielewa vinahusu nini ,Waliobahatika kurudi vitani wengi wao wameokana kujutia uamuzi wa wa kujihusisha na vita Iraq na wanailahumu serikali yao kuwadanganya pia wameomba radhi kwa familia zilizodhurika na vitendo vyoa.

Huyu ni Moja wa mwanajeshi aliyeshiriki vita vya Iraq ameonekana akimshambulia kwa maneno George bush kwa kusema amewadanya kuhusu Iraq na rafiki zake wamekufa hivyo aombe msamaha.

Marekani ilitakiwa iwajibishwe kwa hili.
 
Ukisoma maandiko hasa Biblia. Hawa waarabu kuteseka na kuwa na machafuko sio jambo la kushtushwa.

US atalaumiwa bure tu ila kuna spiritual issues behind.
So waarabu Mungu kawaandikia wawe watu kuteseka ,na Mungu gani huyo anafanya hivyo .

Marekani hawezi kutolewa kwenye lawama alichokifanya ni non-spiritual hakiwezi kuunganishwa na vitabu vya dini ,

Mafuta ndio yaliyompeleka Iraq like always US does
 
Mungu mvuta bangi anayebagua mataifa na raia aliyewaumba mwenyewe.
 
Ukisoma maandiko hasa Biblia. Hawa waarabu kuteseka na kuwa na machafuko sio jambo la kushtushwa.

US atalaumiwa bure tu ila kuna spiritual issues behind.
Islamophobia inakutesa,,, acha roho mbaya,, yani hata hili unawatetea wamarekani?
Kama usemavyo ndivyo mambo ya spiritual issues ni wayahudi kwa mujibu wa vitabu vya dini ndo wanaotakiwa kutaabika na kuhangaika mpaka pale watakapofika kwenye nchi yao ya ahadi,, lkn mbona kina Netanyahu ambao tunaambiwa ndo wayahudi wenyewe wanakula bata,, kilichofanya waarabu wauwae pale Iraq ni mambo tu ya kisiasa za kidunia mwenye nguvu ndo mwenye haki,, usituongopee sijui habari za spiritual..
 
Marekani hawawezi kujutia ata siku moja swala la kuivamia Iraq kwa ulikuwa ni mpango sahihi ndani ya muda sahihi.

Hebu fikiri Sadamu angeachwa hadi leo Dunia ingetuwa kwenye tension gani?

Sasa hivi ni muda muafaka tena kwa Amerika kutafuta sababu ya kumkabili Irani as they did to Sadam sababu wakimuacha kwa baadae ni tatizo kubwa sana.
 
Fafanua Kwani Iran anashida gani?
 
Ukisoma maandiko hasa Biblia. Hawa waarabu kuteseka na kuwa na machafuko sio jambo la kushtushwa.

US atalaumiwa bure tu ila kuna spiritual issues behind.
Mmmh!Ebu tuwekee mistari kadhaa ya Biblia tupitie.
 
Marekani hawawezi kujutia ata siku moja swala la kuivamia Iraq kwa ulikuwa ni mpango sahihi ndani ya muda sahihi.

Hebu fikiri Sadamu angeachwa hadi leo Dunia ingetuwa kwenye tension gani?

Sasa hivi ni muda muafaka tena kwa Amerika kutafuta sababu ya kumkabili Irani as they did to Sadam sababu wakimuacha kwa baadae ni tatizo kubwa sana.
Iran siyo taifa dogo kama unavyodhani.Wale ni Waajemi.
 
Marekani hawawezi kujutia ata siku moja swala la kuivamia Iraq kwa ulikuwa ni mpango sahihi ndani ya muda sahihi.

Hebu fikiri Sadamu angeachwa hadi leo Dunia ingetuwa kwenye tension gani?

Sasa hivi ni muda muafaka tena kwa Amerika kutafuta sababu ya kumkabili Irani as they did to Sadam sababu wakimuacha kwa baadae ni tatizo kubwa sana.
Hivi uko timamu kweli? Dunia ingekuwaje Sadam angekuwepo?
 
Marekani hawawezi kujutia ata siku moja swala la kuivamia Iraq kwa ulikuwa ni mpango sahihi ndani ya muda sahihi.

Hebu fikiri Sadamu angeachwa hadi leo Dunia ingetuwa kwenye tension gani?

Sasa hivi ni muda muafaka tena kwa Amerika kutafuta sababu ya kumkabili Irani as they did to Sadam sababu wakimuacha kwa baadae ni tatizo kubwa sana.
Saddam hajawahi kuwa tishio la usalama wa middle east na Dunia na marekani hakuwa na Sababu sahihi ya kuivamia Iraq alidangsnya ulimwengu Saddam anamiliki siraha za hatari,anafadhiri Al Qaeda je hizi ndio unaziita sababu sahii.

Lengo la uvamizi ni kuunda serikali itakayo Linda maslahi yake , miaka 20 sasa imepita labda Dunia ipo kwenye tension gani?

Back
Top Bottom