Ahmed Abdel hadi Chalabi

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
Kuna kisa kimoja cha Ahmed Chalabi, nadhani mnamkumbuka sana huyu bwana, alikuwa mpinzani mkubwa sana wa Saddam Hussein

Kwanza tumfahamu huyu mtu hatari kuwahi kutokea kwenye siasa na ujasusi huko mashariki ya kati.

Jina lake kamili aliitwa Ahmed Abdel Hadi Chalabi, alizaliwa tarehe 30 October 1945 huko Kadhimiya Iraq na kufariki tarehe 3 November 2015, alifariki siku tatu mbele alipo timiza miaka 70, alikuwa ni mwanasiaasa maarufu na mashuhuru huko Iraqi, alibatizwa jina la Gorge Washington wa Iraq, ndie mwasisi wa chama cha Iraqi National Congress (INC), aliwahi kuhudumu kama raisi wa balaza la utawala la Iraq (President of the Governing Council of Iraq) pia akawa waziri mkuu wa 37th Iraq, pia amewahi kuwa naibu waziri mkuu chini ya uongozi wa Ibrahim al-Jaafari.

Alipo kuwa rais wa balaza la utawala Iraq (President of the Governing Council of Iraq) nafasi aliyoanza kuitumikia tarehe1 September 2003 mpaka tarehe 30 September 2003 akiwa chini ya kiongozi Mmarekani Paul Bremer, huyu Bremer alikuwa ni Mmarekani aliyekabidhiwa nchi baada ya kumfurusha Saddam Hussein.

Sasa turudi kwenye Kisa chenyewe...

Kama nilivyosema huko nyuma, Ahmed Abdel Hadi Chalabi alikuwa ni mpinzani mkubwa sana wa Saddam Hussein, kumbe pia alikuwa ni jasusi wa Iran.

Iran ilitaka kuuangusha utawala wa Saddam Hussein, lakini kila walipojaribu kumuangusha Saddam Hussein ilikuwa ngumu, Yani walishindwa, ndipo wakaona Sasa wamtumie Ahmed Abdel Hadi Chalabi katika ujasusi pacha, kwa kuwa alikuwa mtu wao kitambo, Iran ikamuandaa Chalabi, ikumbukwe Chalabi ni muumini wa Shia, mfuasi wa siasa za Ayatollah na muhafidhina wa siasa za kiuajemi.

Kisa chenyewe sasa

Iran wakasuka ushahidi fake kuwa Saddam Hussein ana silaha za maangamizi, wakidai kuwa Saddam Hussein kanunua uranium toka Niger na ana mobile labaratory za kutengeza chemical weapons, wakampa huo ushahidi wote Ahmed Abdel Hadi Chalabi.

Kwakuwa Ahmed Abdel Hadi Chalabi alikuwa mpinzani wa Saddam Hussein kwa mda mrefu, pia alikuwa Muiraq aliye mpinga Saddam kwa muda mrefu hivyo Iran waliamini Marekani wangemuamini haraka, ikizingatia pia Marekani huungana na yoyote hata kama ni adui pale tu wanapo tetea masrahi Yao.

Hivyo Ahmed Abdel Hadi Chalabi akawafuata wamarekani na kuwaonyesha huo ushahidi, Mmarekani akaingia mkenge, akaamini ule ushahidi wakamvamia Saddam Hussein na kumtoa madarakani na kumsimika Ahmed Chalabi kuwa rais wa muda na kisha Waziri mkuu.

Kilichofuata Sasa ni Chalabi kufungulia Wairan kuingia Iraq, Yani washia wakamwagika Iraq, ambao tena hao washia-Wairan wakaanza kuwaua Wamarekani, mrejee Moqtada Al Sadr, kiongozi wa kishia aliyepata nguvu kupitia Ahmed Abdel Hadi Chalabi na kuongeza ushawishi wa Iran na ushia Iraq, Marekani kuja kushituka tayari Iraq imekuwa under Iran influence mpaka kesho.

Wamarekani waliudhika sana walipogundua kumbe Chalabi ni agent wa Iran, yaani Iran wamewatumia Wamarekani kumtoa Saddam Hussein na hatimae kumuua Saddam Hussein ambae alikuwa adui yao mkubwa, Saddam Hussein aliwachukia sana Iran na ushia, rejea vita ya Gulf War.

Kiufupi ni kuwa Marekani iliingizwa chaka na Iran, kupitia Ahmed Abdel Hadi Chalabi.

Hilo suala la Chalabi halikuwapendeza Wamarekani, ikaandaliwa Operation maalum iliyoitwa "Operation Petra", Marekani ikatuma kikosi kazi cha CIA , kitengo cha SAD (Special Activities Deparment) kwenda Iraq kummaliza Chalabi.

Basi siku moja Chalabi akiwa zake Aljazeera anahojiwa jinsi ushahidi wa kumtoa Saddam Hussein ulivyokua fake, Chalabi akawaponda Marekani kuwa haiwezekani taifa kubwa kama Marekani Tena super power kama Marekani itegemee ushahidi wao akina Chalabi kuanzisha vita wakati wao Wamarekani wana asset za kutosha kupata information zote na kuact accodingly.

Mtakumbuka kuwa ule ushahidi wa kina Chalabi ulipofika Marekani Gorge W. Bush mwenyewe alipotoshwa na makamu wake Dick Cheney, someni Ile makala yangu ya "Dick Cheney; Chuma cha White House na Mwamba wa Washington" nimeonesha namna ushahidi ule ulivyo pikwa pale pentagon kwa baraka za Cheney na Donald Rumsfeld.

Kwenye yale mahojiano ya Chalabi kule Aljazeera kumalizika kama masaa kumi hivi ya mahojiano kuisha Ahmed Chalabi akapatikana amekufa chumbani kwake, maelezo ya kitabibu yakaonesha sababu ya kifo ni heart attack.

Bado aijawekwa wazi sababu hasa ya kifo cheke, japo duru kadhaa za kijasusi hudai kuwa wale majasusi wa SAD walipaka sumu kwenye koti lake la suti, wengine hueleza kuwa kitasa cha chumba chake kilipakwa sumu ya polonium, huku wengine wakieleza kuwa waliitumia Aljazeera kupaka sumu microphone bila yeye kujua.

Wengine utamatisha kwa kusema kuwa walimpulizia sumu-hewa chumbani kwake akiwa kalala, hizi sumu za kafie mbele ni noma, huwezi kujua nini hasa na wapi ilikunyakua.

Leo nimewaletea huku Uzi ... Kutokea Maktaba Kuu...

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526/0765026057 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu-CMCA
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057(Whatsapp).
Email-mbwanaallyamtu990@gmail.com

The CMCA, Copyright 2023, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.

FB_IMG_1673794945779.jpg
 
Back
Top Bottom