Kwa wale wajuzi wa mambo ningependa kufahamu kati ya shirikisho hizi mbili za kikanda, Southern African Development Community (SADC) na East African Community (EAC), ni ipi yenye manufaa zaidi kwa Tanzania?
SADC
1. ingeweza kuwa na manufaa zaidi ya kiuchumi iwapo uchumi wetu ungekuwa competitive. May be baadaye, kama Tanzania itatumia vizuri geographic advantage( bandari zake, miundo mbinu mf. Tazara) na utajiri wa maliasili kuvutia uwekezaji unaolihakikishia Taifa maslahi mazuri. Sina uhakika na maslahi ya Taifa katika uwekezaji wa wenzetu wa SADC katika sekta ya madini, mahoteli nk. Ningetarajia TZ pia kuimarisha uwekezaji wake katika nchi zingine za SADC.
2.Kisiasa SADC ni more stable na inashabihiana na TZ katika tunu hiyo. SADC inaweza kuwa na uhakika zaidi kisiasa. Isipokuwa Congo DRC kwa sasa na nchi za kusini wakati wa vita vya ukombozi, hatutarajii nchi za SADC kuibebesha TZ mzigo wa wakimbizi au uzagaaji wa silaha haramu kutokana na vita vya ndani. Lakini bado kuna mtihani Zimbabwe,na hata Angola.
3. SADC ina defence pact , maana yake ina meno. Pact hii ndiyo iliyomnusuru Joseph Kabila. Huwezi kujua TZ nayo inaweza kuitumia siku moja au nyingine. Kabla hujafa hujaumbika-msemo wa wahenga.
EAC
1.EAC kwa sehemu kubwa ni politically volatile. Kuna viashiria vingi vya vurugu za kisiasa kutokea kwa sababu ya kupigania madaraka. Demokrasia bado sana karibia katika nchi zote ikiwemo Rwanda, Uganda, Burundi au hata Zanzibar na Southern Sudan. Katika hali kama hiyo one has to be very careful. Hakuna uhakika, kwa mfano, iwapo wababe wa kivita wanaweza kuachia madaraka kwa kura au ni kusubiri mapenzi ya Mungu tu!
2. Kijiografia TZ ndiyo daraja kati ya EAC na SADC. Naamini disorietation iliyopo hivi sasa ni zao la wababe wa kivita ambao waliibuka miaka ya hivi karibuni. Kwa TZ huu ni wakati wa kujifunza na kujipanga upya lakini siyo kukatishwa tamaa. Ukiangalia ndani ya nchi za EAC, kuna vyama vya upinzani ambavyo vina mawazo tofauti kabisa na msimamo wa wababe hao. Hivyo ni upungufu mkubwa kuuchukulia msimamo wa wababe hao kuwa ndiyo msimamo wa nchi hizo. Fikiria baadhi wanatarajiwa kwenda ICC, je ni wao watakaohukumiwa au ni nchi zao ? Kwa hivyo huenda upepo huu utapita na wababe hao.
3. Ni muhimu TZ kubuni mkakati wa kimahusiano ambao unalenga nchi moja moja na siyo EAC kwa pamoja ili kulinda maslahi yake. Kwa mfano misingi ya maslahi ya Tanzania katika kila nchi ya EAC huenda ni tofauti. Hakuna sheria ya kimataifa ambayo inazuia nchi mbili kuhusiana. Nitoe mfano Sudan Kusini kila mwaka wanahitaji mahindi, nadhani waliwahi kupiga hodi hapa Dar kuulizia mahindi. Burundi wana mahitaji mengi Tanzania. Waganda wengi wanaiheshimu TZ, na wengi sana wamemchoka M7. Jamaani Wanyarwanda -majority ni anti PK.
4. Naamini kwamba SADC na EA ni muhimu kwa TZ kiuchumi, kisiasa, kiusalama, na kijamii. Ukitaka kujadili umuhimu wa moja wapo katika msingi mmoja tu, huenda ukafikia tamati isiyo pana, ambayo haitalisaidia Taifa vya kutosha kuibua mkakati mpya kulingana na hali iliyopo.