SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

Uchambuzi mzuri unaoonyesha dalili zote za mtu aliyesoma halafu akaelimika. Nakuombea Mama akukumbuke siku moja hata kwenye post ya ubalozi mdogo ili ukasaidiane na Balozi wetu huko New York City

Nashukuru kwa sifa ulizonilundikia lakini mimi sasa nacheza na wajukuu tu na ndio maana nakumbuka historia ya nchini yetu!!! Huko unakosema niliishi miaka mingi iliyopita!!!
 
Muongo huyo anasema kipindi Cha mkapa Tony Blair katusaidia kupunguza madeni wakati ndio alituuzia rada kwa Bei kubwa hadi waingereza wenzake wakaingilia Kati.
Kwani yeye Mh. Tony Blair alitulazimisha kununua hiyo rada?
cc: Bulesi
 
Nashukuru kwa sifa ulizonilundikia lakini mimi sasa nacheza na wajukuu tu na ndio maana nakumbuka historia ya nchini yetu!!!
Ubarikiwe sana. Wasalimie wajukuu zangu waambie babu mdogo anawasalimia sana
 
Eti kwny Pandora yumo kaficha pesa zake za kula rushwa?Mlipoambiwa elimu elimu elimu mlibisha.Jifunze tofauti Kwanza Kati ya Tax Avoidance vs Tax Evasion.
Mkuu Tony Blair ndio alihusika na kuiuzia Tanzania radar kwa ufisadi, Hadi ikapelekea wabunge wa uingereza kuingilia Kati.
Blair alikuja kujiuzulu nafasi zake zote kutokana na madudu aliyofanya akiwa waziri mkuu.
 
SA chama kipya kinaandaa Xenophobia ya kuaa na kupokonya mali za wageni weusi mwezi ujao Nov njaa ikiwabana wanaamini katika kupora hiyo SABC hutawaona wakiwata watu kuhoji huo ujinga ndio watufundishe sisi..
 
Kwani yeye Mh. Tony Blair alitulazimisha kununua hiyo rada?
cc: Bulesi
Hujui alichofanya behind the scene, ndio maana wabunge wa uingereza wakaingilia Kati hili suala na kumshutumu Blair
Unahisi kwa nini bunge la uingereza liliingilia Kati ikiwa hatukulazimishwa kununua?
 
Tumefeli kwa kiwango cha juu kuwasikiliza wale wahuni...
Blair ana majanga mengi miaka na miaka na hapo ndio concern yao ilipo
Blair alihusika na kutuuzia radar kwa Bei kubwa, hali iliyopelekea bunge la uingereza kuingilia Kati.
 
Ingekuwa hivyo humu kusingekuwa na watu kabisa. Jf imebaki salama siku zote, ndio maana hata wakati wa Jiwe tulimtukana vizuri tu humu.
Mama hajamfungulia yoyote, ukitaka kujua hilo tumia jina halisi Facebook au Instagram uone Kama atakuacha.
Juzijuzi tu katoka kukamatwa mchora katuni, yule daktari n.k

Nakubaliana na wewe kwa hili, KONGOLE kwa Maxence kwa kuwa professional, tumesalimika toka enzi za JIWE!!!
 
Shirika la habari la South Africa walikuwa na mjadala kuhusu Mama Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake.

Hoja ya wachambuzi haikuwa kwa nini Tony Blair Bali ilikuwa credibility ya Tony Blair.

Wanasema Tony Blair hana credibility, hivyo kumteua kuwa mshauri ni kosa na wanashangaa imekuwaje Tanzania nchi iliyopigania ukombozi kufanya kitu kama hicho.

Mimi binafsi kwenye hili sijui hata nisimamie wapi maana sijui pa kuanzia, ngoja tuendelee kusubiri wajuvi wakilichambua kwa hoja.

View attachment 1987100
Anachokijua mama ni kurembua macho tu kama kala kungu.
Huyu Tony brair atakuwa anatumika au ana maslahi na makampuni ya hizi dawa za covid,
Hii kitu ina implications kubwa kwa keai ya mbowe,maana Kuna "mabeberu"wanataka Mbowe aachiwe,wakati huo huo na ccm imewakumbatia baadhi ya "mabeberu"sasa Hawa mabeberu wataangalia wapi Kuna maslahi yao makubwa?!!kwenye kesi au ccm??
Hapo ndio tunasema mbwa kala mbwa
 
Kuna tatizo kubwa kama Mkuu wa nchi atakuwa na washauri peke yao walioelimishwa kwa fedha za multilateral institutions au taasisi za magharibi!!! Mlengo wao mara nyingi sio kuwa independent thinkers bali to always lean towards western interests na sio interests za nchi zao!!! Ni vema kama kiongozi akiwa na jopo [ diversity] la washauri hasa kwenye mambo ya uchumi kuliko kumtegemea kiumbe mmoja!!

Kuhusu uteuzi wa Tony Blair, mimi binafsi sina tatizo kutegemeana na nchi inataka nini kutokana na uteuzi huo. Katika miaka hii ya utawala wa Magufuli nchi yetu haikuwa na uhusiano mzuri na mataifa mengi hasa ya Ulaya na Marekani; hivyo ikaonekana kutokana na historia ya huko nyuma enzi za Mkapa, mtu pekee ambae anaifahamu vizuri nchi yetu na angeweza kutusaidia kurudisha uhusianao mzuri na nchi za nje ili kupata misaada hasa wa kupambana na covid 19 ni taasisi ya Tony Blair.
Tukumbuke kuwa huko nyuma akiwa Waziri Mkuu enzi ya Mkapa nchi yetu ilikuwa na ludo la madeni ya nje na ni huyu huyu Tony Blair aliyetusaidia kuwashawishi wadeni wetu kupunguza na hata kuyafuta madeni na nchi ikapata afueni. Ni kufuatana na historia hiyo na matatizo tuliyonayo na covid 19 ndio maana ikaonekana kuwaomba taasisi ya Tony Blair kutusaidia ni jambo la busara. Tukumbuke pia kuwa hizi chanjo za covid19 zinapatikana hasa kwenye nchi zilizoendelea na hasa marekani hivyo tunahitaji mtu anayekubalika na BIDEN iili kupata hizo chanjo!!!!

Tanzania sio nchi pekee ya Africa inayomtumia Tony Blair kwa ushauri. Majirani zenu wa Rwanda wamekuwa wanamtumia kwa muda mrefu sasa na wana matokeo mazuri
Unaongea vitu ambavyo huvijui
Blair ni mhuni, alihusika na kutuingiza mkenge kwenye ununuzi wa radar Hali iliyopelekea bunge la uingereza kuingilia Kati hilo suala.
Najua huwezi kukumbuka maana pengine ulikuwa upo nursery
 
Shirika la habari la South Africa walikuwa na mjadala kuhusu Mama Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake.

Hoja ya wachambuzi haikuwa kwa nini Tony Blair Bali ilikuwa credibility ya Tony Blair.

Wanasema Tony Blair hana credibility, hivyo kumteua kuwa mshauri ni kosa na wanashangaa imekuwaje Tanzania nchi iliyopigania ukombozi kufanya kitu kama hicho.

Mimi binafsi kwenye hili sijui hata nisimamie wapi maana sijui pa kuanzia, ngoja tuendelee kusubiri wajuvi wakilichambua kwa hoja.

View attachment 1987100
Kosa wanalolifanya ni kumrithisha rafiki au adui rais wetu. Kama wao walikosana na Blair kipindi hicho Mama Samia halazimiki kufuata nyayo zao.
 
Hujui alichofanya behind the scene, ndio maana wabunge wa uingereza wakaingilia Kati hili suala na kumshutumu Blair
Unahisi kwa nini bunge la uingereza liliingilia Kati ikiwa hatukulazimishwa kununua?

Unamkumbuka mama Claire Short mbunge wa Chama Cha Tony Blair aliyelivalia njuka suala la ununuzu wa Radar kule kwenye Bunge lao?
 
Unaongea vitu ambavyo huvijui
Blair ni mhuni, alihusika na kutuingiza mkenge kwenye ununuzi wa radar Hali iliyopelekea bunge la uingereza kuingilia Kati hilo suala.
Najua huwezi kukumbuka maana pengine ulikuwa upo nursery
Alikuwa mhuni miaka ya nyuma. Usikariri tukio moja la zamani ukalihusisha na jingine la miaka ya sasa. Kila mtu anao ujanja wa kuongea na mtu mwingine, anao ushawishi wake usiofanana na wa mwingine.
 
Ngoja wale wanaomuunba mkono waje! Yaani nchi hii haijawahi kuwa kwenye kipindi cha hovyo kama hiki! Tony Blair anawexaje kuwa mshauri wakati si mtu msafi huko kwao?
Kwa mtanzania hajawahi kutokea rais msafi mpaka awe ameshaondoka ikulu. Anachojua ni malalamiko na kilio kisichokuwa na msingi.

Najua kuwa Mama alipokuwa anaongea na Blair mimi na wewe hatukuwa karibu na tukio tumeliona tu kwenye picha. Tupunguze kuhukumu.
 
Shirika la habari la South Africa walikuwa na mjadala kuhusu Mama Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake.

Hoja ya wachambuzi haikuwa kwa nini Tony Blair Bali ilikuwa credibility ya Tony Blair.

Wanasema Tony Blair hana credibility, hivyo kumteua kuwa mshauri ni kosa na wanashangaa imekuwaje Tanzania nchi iliyopigania ukombozi kufanya kitu kama hicho.

Mimi binafsi kwenye hili sijui hata nisimamie wapi maana sijui pa kuanzia, ngoja tuendelee kusubiri wajuvi wakilichambua kwa hoja.

View attachment 1987100
Covid-19. and trades adviser,whats wrong with that?....!,zama za mismamo ya kina MUGABE zimeshapita,Tuko kwenye Dunia ingine kabisa,yenye kuitaji akili kubwa zaidi,shutup to SABC.
Binafsi namsifu sana sana,anafikra za juu zaidi.
 
Unaongea vitu ambavyo huvijui
Blair ni mhuni, alihusika na kutuingiza mkenge kwenye ununuzi wa radar Hali iliyopelekea bunge la uingereza kuingilia Kati hilo suala.
Najua huwezi kukumbuka maana pengine ulikuwa upo nursery

Usiniambie nilikuwa nursery, wewe unamkumbuka Claire Short mbunge wa labour aliyelivalia njuga hili suala la RADAR akaja mpaka Dar? Tony Blair has intergrity sio muhuni ila pengine kulikuwa na wahuni ndani ya serikali yake;na ndio maana hata aliweza kukili makosa ya IRAQ invasion. WHO ELSE WOULD YOU RECOMMEND TO GET US VACCINATIONS FROM BIDEN IF NOT TONY BLAIR?
 
Back
Top Bottom