SoC03 Sababu zinazoweza kukuza uchumi

Stories of Change - 2023 Competition
May 24, 2016
15
10
Wachumi na watalaamu wa mambo ya uchumi wamekuna vichwa na sasa wanakubali kuwa sababu hizi zinaweza kukuza uchumi wa nchi kama zitafanywa kwa kuzingatia kanuni zake, na kwa msisitizo.

Na suala la uchumi mbovu katika nchi zinazoendelea ni jambo la kawaida, kiasi kwamba viwanda vingi vimekufa na ajira ni tatizo kubwa tu kabisa.

Nazo ni hizi:

Nguvu kazi ya watu, Mitaji halisia, Maliasili, Ukuaji wa teknolojia, Ujasiriamali,Ongezeko la watu na Mambo ya kijamii.

Katika makala hii tutajadili kwa pamoja kwa undani kuhusu sababu mbalimbali za kiuchumi na jinsi ya kuangalia njia za kuchukua kuhakikisha uchumi wa nchi unakua kwa kiwango kinachotakiwa.

Chanzo cha habari hii ni tafiti katika mtandao wa www.google.com


Utangulizi

Mambo ya kujadili ni haya,

1. Sababu zinazoathiri ukuaji wa uchumi

2. Vipimo vya kuchukua kuhakikisha ukuaji wa uchumi

3. Hitimisho

Kwa kuanza mjadala kwa mujibu wa Wanauchumi, kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha uchumi wa nchi ukakua vizuri na kufanya ustawi wa watu wa nchi husika ukawa mazuri pia, ila kuna baadhi ya sababu ambazo kwa msaada wa mtandao wataalamu wa uchumi wamezitaja ambazo ni:

Uwepo wa maliasili
- Wanasema maliasili ni sababu ya muhimu kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla.

- Maliasili zenyewe ni pamoja na ardhi yenye rutuba, uoto wa misitu ya asili,mtiririko wa mito ya asili,madini, mafuta, na hali nzuri ya hali ya hewa.

- Kuwepo na uwingi wa maliasili ni kichocheo cha uchumi na wanasema nchi isiyokuwa nazo inaweza kuwa na ukuaji wa kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi.

-Wanasema kuwepo kwa maliasili za kutosha siyo hali muhimu sana ya kusababisha ukuaji wa uchumi kama hakutakuwa na kuzingatia.

- Wanatolea mfano nchi kama Japan, Singapore hazina maliasili za kutosha lakini ni miongoni mwa nchi tajiri duniani. Kwanini unaweza ukauliza? Kuna jibu huko chini lakini hapa nitasema ni kwa maliasili ndogo walizonazo walizingatia wakazitumia vizuri.

- Wanaendelea kusema nchi hizo zimezingatia kulinda hiyo maliasili ndogo walionayo katika kuitumia vizuri na kupunguza upoteaji usiosababu wa rasilimali za taifa.

2. Ukuzaji wa mitaji
Wanasema ukuzaji wa mitaji ni njia ya kuchukua akiba za wananchi na kuziingiza katika kuanzisha viwanda na kujipatia zana pamoja na mashine za kuongeza uzalishaji, katika kiwango cha uzalishaji katika taifa na kuboresha utendaji kazi na kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa bidhaa na utoshelevu wa huduma katika nchi.

- Wanasema ukuzaji wa mitaji ni pale ambapo jamii haitumii mapato yao yote kununua bidhaa za kutumia kwa wakati wa sasa lakini wanashauriwa kuweka akiba kiasi na kitumike katika uzalishaji au kuwa mtaji wa uzalishaji wa bidhaa kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uzalishaji wa taifa.

3. Mwendelezo wa teknolojia ya kisasa
- Wnaongeza kwa kusema teknolojia ni pale mnapoitumia kwa kufanya tafiti mbalimbali zinazochangia kuboresha mbinu za uzalishaji sehemu za kazi.

- Maliasili ipo kwa ajili ya matokeo ya mwendelezo wa teknolojia. Hata hivyo teknolojia ipo kuongoza na kukuza uzalishaji.

- Kwa maneno mengine kuwa na teknolojia bora kunaongeza uwezo wa kuzalisha zaidi na kuwa na matumizi mazuri ya maliasili.

- Mwendelezo wa teknolojia unaboresha uwezo wa kufanya matumizi bora ya maliasili zilizopo hata kama ni chache.

4. Ujasiriamali
- Wanasema ujasiliamali ni njia ya uwezo wa kutambua fursa mpya za uwekezaji na hatua madhubuti za kujitoa muhanga kuchukua hatua hizo na kuwekeza katika biashara mpya na kukuza zilizopo.

- Wanasema watu wengi katika nchi zinazoendelea ni masikini siyo kwasababu ya ukosefu wa mitaji, miundombinu ya barabara, hawana taalumu sahihi, bali ni kwa ukosefu wa kuwa na mbinu za kiujasiriamali.

- Hivyo inatakiwa katika nchi zinazoendelea kuwekeza katika ujasiriamali kwa kusisitiza elimu ya ujasiriamali, tafiti mpya, na sayansi katika ukuzaji wa teknolojia.

5. Ukuzaji wa nguvu kazi kwa watu
- Wnasema ubora wa uwingi wa watu ni njia ya uwezo wake wa kupima kiwango cha ukuzaji wa uchumi.

- Na matokeo yake kuwekeza katika nguvu kazi ya watu hao katika njia ya elimu, kupewa madawa na njia nyingine katika mifuko ya kijamii ni ya kutamanika sana kuifanya.

- Ukuzaji wa nguvu kazi inasaidia kukuza uelewa wa watu katika mbinu na uwezo ambao utaongeza uzalishaji katika kazi azifanyazo.

6. Ukuaji wa ongezeko la watu
- Wnasema kukua katika sekta ya ajira kunategemea sana ukuaji wa ongezeko la watu katika nchi na kusababisha ukuaji wa masoko ya bidhaa na huduma. Na matokeo yake ajira zaidi zinatoa matokeo makubwa na soko kubwa linameza uzalishaji wote.

- Hivyo ukuaji wa ongezeko la watu linatakiwa liwe la kiasi. Likiwa kubwa kupita kiasi litasababisha matatizo katika ukuaji wa uchumi.

- Linatakiwa ongezeko la watu liwe la kiasi kuleta ubora wa ukuaji wa uchumi.

7. Mambo ya kijamii
- Wanasema upatikanaji wa huduma za kijamii kama shule, vyuo vya kiufundi, vyuo vya kitabibu, hospitali, na huduma za afya za umma ni njia nyingine ya kubainisha ukuaji wa uchumi.

- Huduma hizi husaidia ongezeko la watenda kazi katika soko la ajira kuwa wenye afya bora,kuongeza nguvu ya utendaji kazi na wanakuwa wawajibikaji.

- Hawa watu wanakuwa na uwezo wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi wa nchi yao kwenda mbele.

Sasa hebu tuangalie hatua za kuchukua ili kufanya ukuaji wa uchumi unaotakiwa;

Hatua za kuchukua kuhakikisha uchumi unakua:
- Ukuaji wa uchumi unaweza kufanikiwa pale kiwango cha pato la uzalishaji linapokuwa kubwa Zaidi ya kiwango cha uwingi wa ongezeko la watu.

- Nguvu kazi ya nchi iwe ya kutosha iliyowezeshwa kwa mbinu muhimu na uwezo wa kukabiliana na teknolojia inayotumika kufanyia kazi na uwepo upatikanaji wa fedha.

- Nchi ya watu walioelimishwa katika soko la ajira wenye uwezo wa kutumia teknolojia vizuri na kutimiza malengo yao husaidia kukuza uchumi wa nchi zao.

- Uboreshwaji wa teknolojia husaidia kuongeza uzalishaji hata kama hakuna maliasili za kutosha. Nchi zilizofanyia kazi suala hili la kiteknolojia walikuza uchumi haraka Zaidi kuliko nchi ambazo hawakuweka mkazo katika suala hili.

Hitimisho
Hayo ni baadhi ya mambo niliyokwambia tuyajadili kwa pamoja yanaweza kusaidia kubadili kwa kiasi uchumi wa nchi yetu. Tukichukulia mifano na ushauri uliotolewa na watalaamu hawa wa mambo ya kiuchumi duniani.

Je wewe unasema ni sawa serikali yetu iyachukue na kuyafanyia kazi kupitia kwa watunga sera? au una mawazo gani? Karibu tujadili pamoja.
 
Back
Top Bottom