GE2025 Sababu za wanaompinga Dkt. Samia

GE2025 Sababu za wanaompinga Dkt. Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
KWA NINI DKT SAMIA ANACHUKIWA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Hivi sasa, wakati mchakato wa uchaguzi unakaribia wamejitokeza baadhi ya Watanzania ambao ni WanaCCM na wengine Wanachama wa vyama vingine vya siasa kupeleka shutuma kadhaa kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Dkt Samia Suluhu Hassan. Shutuma zao hazina maana na msingi wa shutuma, lawama, hila na husda hizi zilianza kusukwa mwaka 2021 baada tu ya Dkt Magufuli kufariki. Kuna watu wachafu ambao hawastahili kuwa na legality wala legitimacy ya kukosoa utawala huu wamejitokeza front kukosoa. Yaani shetani kupata bahati ya kuwa kwenye kundi la Malaika anataka kujibatiza kuwa yeye pia ni malaika.

Leo nitakupitisha kidogo juu mkakati wa mwaka 2021ambao ndo vita hii ambayo leo watu wanahaha kujitakatisha kuwa wao ni wasafi na mwisho nitakueleza sababu ambazo zinasababisha hawa watu kumchukia Dkt Samia na wengine wakisema asingeweza hata kuchukua fomu ya kugombea. Kwa ufupi hii ni vita yetu sisi WanaCCM na hawa waliopata bahati ya kupitia CCM. Akiguswa Mwenyekiti wa CCM imeguswa ni CCM. Hakuna mtu mwema anayeweza kukusema mbele ya watu, ukiona mtu anakusema mbele ya watu huyo si rafiki yako ni adui Yako ambaye na wewe unataki ukabiliane naye kwa njia yoyote unayodhani ni sahihi kumkabili. Hawa waliotaka kuvunja katiba mwaka 2021 walikwama, hata leo tunatakiwa kuwaonyesha kuwa wamekwama kwa vitendo.

Baada ya Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli kufariki aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dkt Samia Suluhu Hassan aliapishwa tarehe 19/3/2021. Msingi wa uapisho huo unatokana na Ibara ya 36(5) ya Katibu ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ya mara kwa mara. Hivyo uwepo wake ni takwa la kisheria na siyo vinginevyo.

Ninaomba nikupitishe kidogo juu ya kelele unazozisikia leo kuhusu Dkt Samia. Nitarejea juu ya minong'ono ya mtaani na minong'ono iliyotawala pale uwanja wa Taifa wakati wa kuaga mwili wa hayati Dkt Magufuli. Mimi ni sehemu ya Watanzania wachache tuliohudhuria kuaga mwili wa hayati Dkt Magufuli Uwanja wa Uhuru Dar es salaam. Nimesema ni sehemu ya Watanzania wachache kwani Watanzania zidi ya milioni 60 hawakupata neema hii.

Wakati wa kuaga mwili kulikuwa na minong'ono mingi pale uwanjani hata nje ya uwanja kuwa kuna viongozi walikuwa hawataki Dkt Samia aapishwe kuwa Rais. Walitaka watumie mbinu bandia/ kinyume na katiba ili watafute Rais wanayemtaka wao. Tetesi zilisema hao watu walijipanga kugawana madaraka.Haya ni maneno yalikuwa yakisemwa. Mimi niliamini ni uzushi hasa ukizingatia kukiwa na msiba kwenye jamii zetu maneno hayakosekani. Hivyo nilihisi ni uvumi wa uongo. Nimeanza kuamini kuwa tetesi hizo zilikuwa na ukweli kwa kuwa wengine ambao tetesi hizo zilikuwa zinawahusu leo hii wameibuka kusema kuwa Dkt Samia hastahili kuchukua fomu ya kugombea Urais. Kwa mantiki hii hizi hazikuwa tetesi tena kuna nadharia ya ukweli. Ninadhani waliokuwa wakinong'onezana uwanjani walikuwa wameoteshwa ukweli huo.

Lakini baada ya Mhe Rais kuapishwa yalianza tena kuzagaa maneno mtaani kuwa eti Rais hafiki December, sikufahamu hafiki kwa mantiki ipi? Lakini alifika December na sasa tunazungumza miaka minne. Tafsiri yake ni kuwa hili kundi lilijipanga lakini hawakujua kuwa wao wanapanga na Mungu anaamua. Ninaamini Watanzania wengine waliosikia hii minong'ono walifunga na kuomba ndio maana Taifa limevuka na Mama amevuka salama mpaka leo. Kinachotokea saizi ingekuwa ni nyumbani Ileje tungesema Mungu anawaadhibu sasa waliyokuwa wanafanya gizani wanafanya hadharani. Mungu anawaumbua...

Kundi hili baada ya kukwama kukanyaga katiba na Rais akaapishwa pia baada ya kukwama mbinu zao zingine yakiwepo madarasa ya siasa leo wamekuja na mkakati mpya ikiwa ni azma yao ile ile ya awali ambayo Mungu alilivusha Taifa salama.

Mhe Rais pamoja na mawimbi makubwa, dhoruba, hila, husda na njama nyingi za kumkwamisha bado amelifanya Taifa kuwa imara, tulivu na kuweka rekodi ya miradi mikubwa kutekelezwa na maendeleo kuonekana kwa macho. Nani asiyefahamu kuwa sasa kiwango Cha furaha kimeongezeka nchini?

Walidhani atakwama, lakini ameweza. Sababu ambazo zinawafanya hawa watu washinde kwenye vyombo vya habari kumshambulia Mhe Rais na Serikali yake yaani kujaribu kuonesha wao ni wema ni sababu zifuatazo:-

1. Wanamchukia Rais Samia kwa kuwa baada ya kuapishwa aliondoa tozo 232 ambazo zilikuwa zinawakwaza Wafanyabiashara na wengine walikuwa wamehamishia biashara zao nje ya nchi. Serikali ya awamu ya sita imejenga mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara, mazingira ambayo yamechochea kuongezeka makusanyo ya kodi.

2. Wanamchukia Rais Samia kwa kuwa amefanikiwa kukuza Diplomasia na mataifa ya nje zikiwepo nchi za AFRIKA mashariki ambazo kuna wakati mahusiano yaliyumba. Rais Samia amefanikiwa kuifungua Tanzania katika Diplomasia ya kimataifa ambayo imechochea kuimalisha uchumi wa Taifa. Watalii wanakuja Tanzania sasa ni wengi sana ambao wanaongeza kuingiza fedha za kigeni.

3. Wanamchukia Rais Dkt Samia kwa kufanikiwa kumaliza ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere(JNHPP) ambalo wakati anaapishwa ujenzi wake ulikuwa umefikia 33%. Walidhani Mhe Rais ataachana na mradi huo mkubwa wa kimkakati. Kitendo cha Serikali ya awamu ya sita kumaliza ujenzi wa Bwawa hilo na kuanza kufanya kazi kimewachukiza sana hawa waliotaka nchi Iendelee kuwa gizani. Rais Samia akihutubia bunge kwa mara ya kwanza alisema atatekeleza miradi yote iliyoanzishwa na JPM. Watanzania aina hii hawakuelewa walisema hawezi, leo wanamchukia kwa kuwa ameweza.

4. Wamechukizwa sana Serikali ya awamu ya sita kukamilisha ujenzi wa Daraja la Magufuli (Kigogo-Busisi) ambalo mtangulizi wake aliliacha likiwa limefikia 16%. Leo Daraja limekwisha na kazi inaendelea. Hili jambo limewachukiza hawataki Dkt Samia achukue fomu wachukue wao ambao historia zao hazijulikani ndani ya Chama na Serikali. Walitaka lisijengwe ili wafurahie kuwa amekwama.

5. Wamechukizwa sana Rais Samia kuendelea kusimamia maono ya hayati JPM ya kufufua na kuimarisha shirika la ndege la ATCL kwa kununua ndege zingine tano ikiwepo ndege ya mizigo aina ya Boing 767-300F. Kuendelea kujenga na kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini. Hili ni kero kubwa kwao na kuongeza uhasama kwa Rais wa nchi. Rais Samia aliposema Mimi na JPM tulikuwa kitu kimoja hawakuelewa.

6. Wamechukizwa sana na Mhe Rais kufufua mradi wa NHC kote nchini kwa mfano ule wa Morocco Square ulioanzishwa na kukwama mwaka 2018 yeye ameufufua na kuumaliza. Mradi wa Kawe, Mradi wa Samia Housing wa nyumba 5000 katika maeneo mbalimbali nchini. NHC ilianzishwa mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge namba 45 kwa kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora. Mageuzi makubwa ya kihistoria yalifanyika mwaka 1990 na 2008, Mhe Rais Samia amekuja kulisimamia hili kwa vitendo. Hii imekuwa karaha kwa ndugu zetu hawa waliojipanga mwaka 2021.

7. Wanamchukia Rais Samia kwa kuendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara. Ukipita Wilaya zote Tanzania ardhi inaomboleza kwa namna Mitambo inavyoendelea kuitindua ardhi na kujenga barabara nzuri za rami na changarawe. Kwa mara ya kwanza Tangu Tanzania ipate Uhuru, Serikali ya awamu ya sita ilitoa milioni 500 katika kila halmashauri kwa ajili ya barabara za vijijini. Wamechukia kuona fedha hizi zinaenda kuwasaidia Wananchi wanyonge kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji.

8. Wamechukizwa na Mhe Rais kwa kuboresha miundombinu ya shule. Serikali ya awamu ya sita imekarabati shule za zamani, imejenga shule mpya, imeongeza nyumba za Walimu na imeweza kuajiri Walimu kwa mara ya kwanza mara baada ya ajira hizi kustishwa toka mwaka 2015. Shule nyingi zilikuwa zimechoka lakini awamu hii zimeboreshwa. Haitoshi zinajengwa shule shikizi ikiwa ni mkakati wa Serikali kuinua elimu nchini na kupunguza changamoto za watoto shuleni.

9. Wanachukizwa sana na uboreshaji wa Afya. Miaka michache iliyopita watu walikuwa wanapishana angani kwenda kutibiwa India. Serikali ya awamu ya sita si tu imeongeza ujenzi wa vituo vya huduma ya Afya kwa maana Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati kila mahali, rahasha! Rais Samia ameweza kununua pia vifaa vya hospitali. Tangu tupate Uhuru tulikuwa na MRI 7 TU, lakini Dkt Samia kwa miaka 4 amenunua MRI 6. Sijui unaelewa? Tangu tupate Uhuru tulikuwa na CT scan 13 lakini Dkt Samia kwa miaka minne amenunua CT scan 32. Tunaelewana? Unadhani kwa kasi hii wanakingine cha kusema zaidi ya ajenda ambazo hazina miguu wala vichwa. Hii ni mifano michache ambayo nimeona nikupe tu uelewa mdogo.

10. Wamechukizwa sana utawala bora. Kwa miaka minne tumeona nguzo zote za utawala bora zikifanya kazi. Watu wanafanya siasa, Waandishi wa habari wanafanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria za nchi, Watu makazini wanaadhibiwa kwa kufuata Sheria, Mahakama zinafanya majukumu yake n.k Mahali ambapo hakuna utawala bora basi hofu inakuwa ni maisha ya kawaida ya watu. Hawataki utawala bora wanataka monopoly
11. Wamechukizwa sana kushusha kwa riba ya mikopo ya Wanafunzi wa vyuo vikuu ambayo imeshuka kutoka 14% mpaka single digit (7%). Hii ilikuwa ni kero kwa wasomi ambao ni wanufaika wa bodi ya mikopo. Tukumbuke 100% ya wanufaika wa mikopo hii ni watu wanaotoka familia masikini na za kati. Unapomtoza 14% ni kumfanya aendelee kuwa masikini zaidi na kuona kukopa ni adhabu.

12. Wamechukizwa na kukerwa vibaya sana na elimu bure. Serikali ya awamu ya nne ilitangaza elimu bure kutoka chekechea hadi kidato cha sita. Lakini pia iliongeza fedha ya kujikimu kwa Wanafunzi wa vyuo. Hawa wanaona hii ni kete kwa Dkt Samia hivyo wanakwazika sana.

13. Wamechukizwa na Agribusiness, huko nyuma mtu kuitwa mkulima ilikuwa ni aibu. Lakini Serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa kwenye kilimo ambapo leo mtu kuitwa mkulima ni fahari. Mwaka 2021 bajeti ya kilimo ilikuwa billion 200± leo hii bajeti ya kilimo ni Trillion 1.2. Lengo la Serikali ni kuona sasa tunaacha kuagiza mafuta ya kula nje lakini pia sukari maeneo ambayo Serikali ilikuwa inatumia fedha nyingi. Wenzetu wanakerwa na mradi wa BBT uliojiri vijana wengi na tunaona matokeo ya kilimo wanachofanya Chinangali na maeneo mengine nchini. Mbolea ya ruzuku imechangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji mkubwa na wenye tija. Haya ndiyo yanawachukiza wenzetu.

14. Wanachukizwa na miradi ya kimkakati 901 yenye thamani ya Dola 127 ambapo mwaka 2021 tulikuwa na miradi ya kimkakati 93 TU yenye thamani ya Dola 1.6 bilioni TU. Hatuoni mapinduzi haya? Urasimu umepungua ndio maana watu wengi wanakimbilia TIC kutafuta fursa.

15. Wanachukizwa na ujenzi wa Daraja la TANZANITE walitaka lisijengwe.

16. Wanakwazika na makusanyo yaliyoongezeka pale bandarini fedha zinazosaidia kwenye miradi ya kimkakati na kuongeza mishahara kwa watumishi.

Pamoja na mengine mengi yanayowakera na kuwachukiza, haya ni machache kati ya mengi ambayo mahasimu wa Samia wanakwazika. Hakuna jambo jingine, wanateswa na mafanikio ya Dkt Samia. Walishajipanga kuwa atakwama. Walijaribu kumkwamisha lakini walishindwa. Kete iliyobaki ni hii wanayohangaika nayo ambayo nayo wamekwama.

October tunatiki.
HII YOTE UNATAFUTA UKUU WA MKOA ?
 
Huu udaktari kautoa wapi?

UNGESE TU na kujipendekeza. Kawaulize kule kijijini kwenu amewafanyia nn
 
Nimekaa hapa namsikiliza mwalimu aliesoma Ng’ong’ona.
 
Rubbish 😞!!. Aliyekufa alikuwa ni Rais wa tano kwenye ilani ya uchaguzi wa awamu ya tano. Aliyeapishwa baada ya kifo cha John Pombe Magufuli ni Makamu wake Samia Suluhu Hassan, ambaye anakuwa Rais wa sita wa JMT lakini akianza urais wake kwa kumalizia ngwe ya pili ya utawala wa awamu ya tano ambayo inakamilishwa na uchaguzi mkuu wa mwaka huu, October 2025.

Hiyo awamu ya sita 2025-2030/5 unayojaribu kuipamba kwa maua ya waridi ilianza vipi mwaka 2021, wakati ndio inatakiwa kuanza baada ya October mwaka huu?
 
Hii nchi yawezekana ina vichaa wengi kuliko tunaowaona mtaani
Ok nipe utofauti uliopo baada ya ujenzi wa bwawa kukamilika na kabla
Leo hii huku kwetu kila siku tupo gizan
Huko kwenu inatakiwa uhame na uhamie kwako.
 
Maelezo kibao uzuri wa mambo mema hayahitaji PR ukishaona inatumika nguvu nyingi kusifia nakueleza mema ya mtu basi ujue kuna shida hapo watu sio wajinga mjue TAL ana shine nakukubalika kwaajili ya Matendo yake,uadilifu wake,misimamo yake thabiti isiyoyumba na namna anavyoitetea nchi yake kwa dhati hadi mnamuona tishio ni kutokana na uungwaji wake mkono na makundi mbalimbali wahenga waliposema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza hawakua wajinga ujue wanajua ukweli utawaweka huru. Maelezo kibao ya miradi isiyoweza kuounguza gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida hakuna msaada leo hii mtu aliyeyepo Mangaka huko ukamueleze kuhusu SGR inamnufaisha vipi? Mtu alieko Ukara huko ukamuambie kuhusu bwawa la mwalimu Nyerere anakuelewa vipi? Mtu yuko zake Mchomolo huko ukamueleze kuhusu royal your anakuelewa vipi? Sasa mnaunganishaje haya mavitu na maisha ya mtu wa kawaida kabisa? Huo ndio uchumi unaopaswa kuleta multiplier effect na uwe jumuishi hizi rasilimali tulizonazo kila mmoja aonje matunda yake na wawe na maisha yenye staha na utu wao

No reform No Election
Kama mnatumia nguvu kuhalalisha uongo kwa nini isitumike nguvu hiyo hiyo kuujibu?
 
Twende na facts wananchi wanataka kuona maisha yao yanakua bora zaidi ya jana na si vinginevyo hakuna kiasi cha pesa kinachotosha kununua upendo nakukubalika, ndio mana mna media zote kubwa mna hela hazina nzima lakini mkitaka kuitisha mkutano tu lazima msombelee watu kwa malori hauoni hizo ni red flag zakutokukubalika halafu mshindani wako ambae unasema anasambaza uongo akiitisha mkutano watu wanajaa kumsikiliza despite yakuleta figisu nakutumia excessive power? Tuambie huo uongo kwa hoja haiwezekani wananchi majority wakawa wanakubali mtu muongo kweli?

TAL hahitaji huruma wala Hisani kutoka kwenu anahitaji Haki kwa Taifa ambayo uwepo wake hata masisiemu yatanufaika na vibaraka watanufaika pia mtu unakubalika lakini hautaki uchaguzi huru halafu unauaminisha umma kua unashinda kigalali sasa kwanini usiruhusu mabadiliko ili ukishinda mpinzani wako akose hoja? Woga unatoka wapi? Tunalinda nini? Maslahi ya nani?

No reform No Election
 
KWA NINI DKT SAMIA ANACHUKIWA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Hivi sasa, wakati mchakato wa uchaguzi unakaribia wamejitokeza baadhi ya Watanzania ambao ni WanaCCM na wengine Wanachama wa vyama vingine vya siasa kupeleka shutuma kadhaa kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Dkt Samia Suluhu Hassan. Shutuma zao hazina maana na msingi wa shutuma, lawama, hila na husda hizi zilianza kusukwa mwaka 2021 baada tu ya Dkt Magufuli kufariki. Kuna watu wachafu ambao hawastahili kuwa na legality wala legitimacy ya kukosoa utawala huu wamejitokeza front kukosoa. Yaani shetani kupata bahati ya kuwa kwenye kundi la Malaika anataka kujibatiza kuwa yeye pia ni malaika.

Leo nitakupitisha kidogo juu mkakati wa mwaka 2021ambao ndo vita hii ambayo leo watu wanahaha kujitakatisha kuwa wao ni wasafi na mwisho nitakueleza sababu ambazo zinasababisha hawa watu kumchukia Dkt Samia na wengine wakisema asingeweza hata kuchukua fomu ya kugombea. Kwa ufupi hii ni vita yetu sisi WanaCCM na hawa waliopata bahati ya kupitia CCM. Akiguswa Mwenyekiti wa CCM imeguswa ni CCM. Hakuna mtu mwema anayeweza kukusema mbele ya watu, ukiona mtu anakusema mbele ya watu huyo si rafiki yako ni adui Yako ambaye na wewe unataki ukabiliane naye kwa njia yoyote unayodhani ni sahihi kumkabili. Hawa waliotaka kuvunja katiba mwaka 2021 walikwama, hata leo tunatakiwa kuwaonyesha kuwa wamekwama kwa vitendo.

Baada ya Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli kufariki aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dkt Samia Suluhu Hassan aliapishwa tarehe 19/3/2021. Msingi wa uapisho huo unatokana na Ibara ya 36(5) ya Katibu ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ya mara kwa mara. Hivyo uwepo wake ni takwa la kisheria na siyo vinginevyo.

Ninaomba nikupitishe kidogo juu ya kelele unazozisikia leo kuhusu Dkt Samia. Nitarejea juu ya minong'ono ya mtaani na minong'ono iliyotawala pale uwanja wa Taifa wakati wa kuaga mwili wa hayati Dkt Magufuli. Mimi ni sehemu ya Watanzania wachache tuliohudhuria kuaga mwili wa hayati Dkt Magufuli Uwanja wa Uhuru Dar es salaam. Nimesema ni sehemu ya Watanzania wachache kwani Watanzania zidi ya milioni 60 hawakupata neema hii.

Wakati wa kuaga mwili kulikuwa na minong'ono mingi pale uwanjani hata nje ya uwanja kuwa kuna viongozi walikuwa hawataki Dkt Samia aapishwe kuwa Rais. Walitaka watumie mbinu bandia/ kinyume na katiba ili watafute Rais wanayemtaka wao. Tetesi zilisema hao watu walijipanga kugawana madaraka.Haya ni maneno yalikuwa yakisemwa. Mimi niliamini ni uzushi hasa ukizingatia kukiwa na msiba kwenye jamii zetu maneno hayakosekani. Hivyo nilihisi ni uvumi wa uongo. Nimeanza kuamini kuwa tetesi hizo zilikuwa na ukweli kwa kuwa wengine ambao tetesi hizo zilikuwa zinawahusu leo hii wameibuka kusema kuwa Dkt Samia hastahili kuchukua fomu ya kugombea Urais. Kwa mantiki hii hizi hazikuwa tetesi tena kuna nadharia ya ukweli. Ninadhani waliokuwa wakinong'onezana uwanjani walikuwa wameoteshwa ukweli huo.

Lakini baada ya Mhe Rais kuapishwa yalianza tena kuzagaa maneno mtaani kuwa eti Rais hafiki December, sikufahamu hafiki kwa mantiki ipi? Lakini alifika December na sasa tunazungumza miaka minne. Tafsiri yake ni kuwa hili kundi lilijipanga lakini hawakujua kuwa wao wanapanga na Mungu anaamua. Ninaamini Watanzania wengine waliosikia hii minong'ono walifunga na kuomba ndio maana Taifa limevuka na Mama amevuka salama mpaka leo. Kinachotokea saizi ingekuwa ni nyumbani Ileje tungesema Mungu anawaadhibu sasa waliyokuwa wanafanya gizani wanafanya hadharani. Mungu anawaumbua...

Kundi hili baada ya kukwama kukanyaga katiba na Rais akaapishwa pia baada ya kukwama mbinu zao zingine yakiwepo madarasa ya siasa leo wamekuja na mkakati mpya ikiwa ni azma yao ile ile ya awali ambayo Mungu alilivusha Taifa salama.

Mhe Rais pamoja na mawimbi makubwa, dhoruba, hila, husda na njama nyingi za kumkwamisha bado amelifanya Taifa kuwa imara, tulivu na kuweka rekodi ya miradi mikubwa kutekelezwa na maendeleo kuonekana kwa macho. Nani asiyefahamu kuwa sasa kiwango Cha furaha kimeongezeka nchini?

Walidhani atakwama, lakini ameweza. Sababu ambazo zinawafanya hawa watu washinde kwenye vyombo vya habari kumshambulia Mhe Rais na Serikali yake yaani kujaribu kuonesha wao ni wema ni sababu zifuatazo:-

1. Wanamchukia Rais Samia kwa kuwa baada ya kuapishwa aliondoa tozo 232 ambazo zilikuwa zinawakwaza Wafanyabiashara na wengine walikuwa wamehamishia biashara zao nje ya nchi. Serikali ya awamu ya sita imejenga mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara, mazingira ambayo yamechochea kuongezeka makusanyo ya kodi.

2. Wanamchukia Rais Samia kwa kuwa amefanikiwa kukuza Diplomasia na mataifa ya nje zikiwepo nchi za AFRIKA mashariki ambazo kuna wakati mahusiano yaliyumba. Rais Samia amefanikiwa kuifungua Tanzania katika Diplomasia ya kimataifa ambayo imechochea kuimalisha uchumi wa Taifa. Watalii wanakuja Tanzania sasa ni wengi sana ambao wanaongeza kuingiza fedha za kigeni.

3. Wanamchukia Rais Dkt Samia kwa kufanikiwa kumaliza ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere(JNHPP) ambalo wakati anaapishwa ujenzi wake ulikuwa umefikia 33%. Walidhani Mhe Rais ataachana na mradi huo mkubwa wa kimkakati. Kitendo cha Serikali ya awamu ya sita kumaliza ujenzi wa Bwawa hilo na kuanza kufanya kazi kimewachukiza sana hawa waliotaka nchi Iendelee kuwa gizani. Rais Samia akihutubia bunge kwa mara ya kwanza alisema atatekeleza miradi yote iliyoanzishwa na JPM. Watanzania aina hii hawakuelewa walisema hawezi, leo wanamchukia kwa kuwa ameweza.

4. Wamechukizwa sana Serikali ya awamu ya sita kukamilisha ujenzi wa Daraja la Magufuli (Kigogo-Busisi) ambalo mtangulizi wake aliliacha likiwa limefikia 16%. Leo Daraja limekwisha na kazi inaendelea. Hili jambo limewachukiza hawataki Dkt Samia achukue fomu wachukue wao ambao historia zao hazijulikani ndani ya Chama na Serikali. Walitaka lisijengwe ili wafurahie kuwa amekwama.

5. Wamechukizwa sana Rais Samia kuendelea kusimamia maono ya hayati JPM ya kufufua na kuimarisha shirika la ndege la ATCL kwa kununua ndege zingine tano ikiwepo ndege ya mizigo aina ya Boing 767-300F. Kuendelea kujenga na kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini. Hili ni kero kubwa kwao na kuongeza uhasama kwa Rais wa nchi. Rais Samia aliposema Mimi na JPM tulikuwa kitu kimoja hawakuelewa.

6. Wamechukizwa sana na Mhe Rais kufufua mradi wa NHC kote nchini kwa mfano ule wa Morocco Square ulioanzishwa na kukwama mwaka 2018 yeye ameufufua na kuumaliza. Mradi wa Kawe, Mradi wa Samia Housing wa nyumba 5000 katika maeneo mbalimbali nchini. NHC ilianzishwa mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge namba 45 kwa kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora. Mageuzi makubwa ya kihistoria yalifanyika mwaka 1990 na 2008, Mhe Rais Samia amekuja kulisimamia hili kwa vitendo. Hii imekuwa karaha kwa ndugu zetu hawa waliojipanga mwaka 2021.

7. Wanamchukia Rais Samia kwa kuendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara. Ukipita Wilaya zote Tanzania ardhi inaomboleza kwa namna Mitambo inavyoendelea kuitindua ardhi na kujenga barabara nzuri za rami na changarawe. Kwa mara ya kwanza Tangu Tanzania ipate Uhuru, Serikali ya awamu ya sita ilitoa milioni 500 katika kila halmashauri kwa ajili ya barabara za vijijini. Wamechukia kuona fedha hizi zinaenda kuwasaidia Wananchi wanyonge kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji.

8. Wamechukizwa na Mhe Rais kwa kuboresha miundombinu ya shule. Serikali ya awamu ya sita imekarabati shule za zamani, imejenga shule mpya, imeongeza nyumba za Walimu na imeweza kuajiri Walimu kwa mara ya kwanza mara baada ya ajira hizi kustishwa toka mwaka 2015. Shule nyingi zilikuwa zimechoka lakini awamu hii zimeboreshwa. Haitoshi zinajengwa shule shikizi ikiwa ni mkakati wa Serikali kuinua elimu nchini na kupunguza changamoto za watoto shuleni.

9. Wanachukizwa sana na uboreshaji wa Afya. Miaka michache iliyopita watu walikuwa wanapishana angani kwenda kutibiwa India. Serikali ya awamu ya sita si tu imeongeza ujenzi wa vituo vya huduma ya Afya kwa maana Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati kila mahali, rahasha! Rais Samia ameweza kununua pia vifaa vya hospitali. Tangu tupate Uhuru tulikuwa na MRI 7 TU, lakini Dkt Samia kwa miaka 4 amenunua MRI 6. Sijui unaelewa? Tangu tupate Uhuru tulikuwa na CT scan 13 lakini Dkt Samia kwa miaka minne amenunua CT scan 32. Tunaelewana? Unadhani kwa kasi hii wanakingine cha kusema zaidi ya ajenda ambazo hazina miguu wala vichwa. Hii ni mifano michache ambayo nimeona nikupe tu uelewa mdogo.

10. Wamechukizwa sana utawala bora. Kwa miaka minne tumeona nguzo zote za utawala bora zikifanya kazi. Watu wanafanya siasa, Waandishi wa habari wanafanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria za nchi, Watu makazini wanaadhibiwa kwa kufuata Sheria, Mahakama zinafanya majukumu yake n.k Mahali ambapo hakuna utawala bora basi hofu inakuwa ni maisha ya kawaida ya watu. Hawataki utawala bora wanataka monopoly
11. Wamechukizwa sana kushusha kwa riba ya mikopo ya Wanafunzi wa vyuo vikuu ambayo imeshuka kutoka 14% mpaka single digit (7%). Hii ilikuwa ni kero kwa wasomi ambao ni wanufaika wa bodi ya mikopo. Tukumbuke 100% ya wanufaika wa mikopo hii ni watu wanaotoka familia masikini na za kati. Unapomtoza 14% ni kumfanya aendelee kuwa masikini zaidi na kuona kukopa ni adhabu.

12. Wamechukizwa na kukerwa vibaya sana na elimu bure. Serikali ya awamu ya nne ilitangaza elimu bure kutoka chekechea hadi kidato cha sita. Lakini pia iliongeza fedha ya kujikimu kwa Wanafunzi wa vyuo. Hawa wanaona hii ni kete kwa Dkt Samia hivyo wanakwazika sana.

13. Wamechukizwa na Agribusiness, huko nyuma mtu kuitwa mkulima ilikuwa ni aibu. Lakini Serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa kwenye kilimo ambapo leo mtu kuitwa mkulima ni fahari. Mwaka 2021 bajeti ya kilimo ilikuwa billion 200± leo hii bajeti ya kilimo ni Trillion 1.2. Lengo la Serikali ni kuona sasa tunaacha kuagiza mafuta ya kula nje lakini pia sukari maeneo ambayo Serikali ilikuwa inatumia fedha nyingi. Wenzetu wanakerwa na mradi wa BBT uliojiri vijana wengi na tunaona matokeo ya kilimo wanachofanya Chinangali na maeneo mengine nchini. Mbolea ya ruzuku imechangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji mkubwa na wenye tija. Haya ndiyo yanawachukiza wenzetu.

14. Wanachukizwa na miradi ya kimkakati 901 yenye thamani ya Dola 127 ambapo mwaka 2021 tulikuwa na miradi ya kimkakati 93 TU yenye thamani ya Dola 1.6 bilioni TU. Hatuoni mapinduzi haya? Urasimu umepungua ndio maana watu wengi wanakimbilia TIC kutafuta fursa.

15. Wanachukizwa na ujenzi wa Daraja la TANZANITE walitaka lisijengwe.

16. Wanakwazika na makusanyo yaliyoongezeka pale bandarini fedha zinazosaidia kwenye miradi ya kimkakati na kuongeza mishahara kwa watumishi.

Pamoja na mengine mengi yanayowakera na kuwachukiza, haya ni machache kati ya mengi ambayo mahasimu wa Samia wanakwazika. Hakuna jambo jingine, wanateswa na mafanikio ya Dkt Samia. Walishajipanga kuwa atakwama. Walijaribu kumkwamisha lakini walishindwa. Kete iliyobaki ni hii wanayohangaika nayo ambayo nayo wamekwama.

October tunatiki.

..kilichomharibia Samia Suluhu ni kutokutekeleza 4R.

..
 
Tutakuwa hatuna akili kama wewe tukijifanganya kuamini upuuzi ulioandika hapa. Point moja tu, Nani aliweka tozo za simu na baadaye kuzipunguza?
 
Umeanza na namba ya simu, na majina kamili, unadhani serikali itakupa teuzi kwa njia hiyo, fanya kazi kijana, fungua hata biashara ndogo ndogo ili ulee familia, hauwezi Pata teuzi kwa mawazo finyu kama haya
 
Sgr iishe please, ifike Mwanza na kigoma na hiyo ndio legacy pekee ya Bimkubwa mengine yote ni taarabu tu.

Kuna video flani ya boss mjeda akieleza walichotaka kufanya baada ya kifo kile, ila sijui kwanini hakuwataja majina watz wawajue wahuni wa taifa! Aisee wahuni wapo wengi ndani ya suti! Mjeda anastahili nishani na heshma kubwa kuzuia wahuni kuvunja katiba na kuiweka nchi salama.

Wanamchukia Maza sababu ya jinsia, dini na alipotoka na ofcourse pia uwezo wake mkubwa wa kumaliza miradi na kuibua ya kwake kama the royal tour, the dream of nuclear power plant, scholarships etc

Mitano tena anastahili kabisa Bimkubwa. Mama ameweza!
Mbona nilisikia mluzi ukipuliza slowly pia alikuwemo
 
Maelezo mareeefu kumbe uharo mtupu, sa100 hana uwezo...short and clear!!!.
 
KWA NINI DKT SAMIA ANACHUKIWA?

Na Elius Ndabila
0768239284

Hivi sasa, wakati mchakato wa uchaguzi unakaribia wamejitokeza baadhi ya Watanzania ambao ni WanaCCM na wengine Wanachama wa vyama vingine vya siasa kupeleka shutuma kadhaa kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Dkt Samia Suluhu Hassan. Shutuma zao hazina maana na msingi wa shutuma, lawama, hila na husda hizi zilianza kusukwa mwaka 2021 baada tu ya Dkt Magufuli kufariki. Kuna watu wachafu ambao hawastahili kuwa na legality wala legitimacy ya kukosoa utawala huu wamejitokeza front kukosoa. Yaani shetani kupata bahati ya kuwa kwenye kundi la Malaika anataka kujibatiza kuwa yeye pia ni malaika.

Leo nitakupitisha kidogo juu mkakati wa mwaka 2021ambao ndo vita hii ambayo leo watu wanahaha kujitakatisha kuwa wao ni wasafi na mwisho nitakueleza sababu ambazo zinasababisha hawa watu kumchukia Dkt Samia na wengine wakisema asingeweza hata kuchukua fomu ya kugombea. Kwa ufupi hii ni vita yetu sisi WanaCCM na hawa waliopata bahati ya kupitia CCM. Akiguswa Mwenyekiti wa CCM imeguswa ni CCM. Hakuna mtu mwema anayeweza kukusema mbele ya watu, ukiona mtu anakusema mbele ya watu huyo si rafiki yako ni adui Yako ambaye na wewe unataki ukabiliane naye kwa njia yoyote unayodhani ni sahihi kumkabili. Hawa waliotaka kuvunja katiba mwaka 2021 walikwama, hata leo tunatakiwa kuwaonyesha kuwa wamekwama kwa vitendo.

Baada ya Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli kufariki aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo Dkt Samia Suluhu Hassan aliapishwa tarehe 19/3/2021. Msingi wa uapisho huo unatokana na Ibara ya 36(5) ya Katibu ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ya mara kwa mara. Hivyo uwepo wake ni takwa la kisheria na siyo vinginevyo.

Ninaomba nikupitishe kidogo juu ya kelele unazozisikia leo kuhusu Dkt Samia. Nitarejea juu ya minong'ono ya mtaani na minong'ono iliyotawala pale uwanja wa Taifa wakati wa kuaga mwili wa hayati Dkt Magufuli. Mimi ni sehemu ya Watanzania wachache tuliohudhuria kuaga mwili wa hayati Dkt Magufuli Uwanja wa Uhuru Dar es salaam. Nimesema ni sehemu ya Watanzania wachache kwani Watanzania zidi ya milioni 60 hawakupata neema hii.

Wakati wa kuaga mwili kulikuwa na minong'ono mingi pale uwanjani hata nje ya uwanja kuwa kuna viongozi walikuwa hawataki Dkt Samia aapishwe kuwa Rais. Walitaka watumie mbinu bandia/ kinyume na katiba ili watafute Rais wanayemtaka wao. Tetesi zilisema hao watu walijipanga kugawana madaraka.Haya ni maneno yalikuwa yakisemwa. Mimi niliamini ni uzushi hasa ukizingatia kukiwa na msiba kwenye jamii zetu maneno hayakosekani. Hivyo nilihisi ni uvumi wa uongo. Nimeanza kuamini kuwa tetesi hizo zilikuwa na ukweli kwa kuwa wengine ambao tetesi hizo zilikuwa zinawahusu leo hii wameibuka kusema kuwa Dkt Samia hastahili kuchukua fomu ya kugombea Urais. Kwa mantiki hii hizi hazikuwa tetesi tena kuna nadharia ya ukweli. Ninadhani waliokuwa wakinong'onezana uwanjani walikuwa wameoteshwa ukweli huo.

Lakini baada ya Mhe Rais kuapishwa yalianza tena kuzagaa maneno mtaani kuwa eti Rais hafiki December, sikufahamu hafiki kwa mantiki ipi? Lakini alifika December na sasa tunazungumza miaka minne. Tafsiri yake ni kuwa hili kundi lilijipanga lakini hawakujua kuwa wao wanapanga na Mungu anaamua. Ninaamini Watanzania wengine waliosikia hii minong'ono walifunga na kuomba ndio maana Taifa limevuka na Mama amevuka salama mpaka leo. Kinachotokea saizi ingekuwa ni nyumbani Ileje tungesema Mungu anawaadhibu sasa waliyokuwa wanafanya gizani wanafanya hadharani. Mungu anawaumbua...

Kundi hili baada ya kukwama kukanyaga katiba na Rais akaapishwa pia baada ya kukwama mbinu zao zingine yakiwepo madarasa ya siasa leo wamekuja na mkakati mpya ikiwa ni azma yao ile ile ya awali ambayo Mungu alilivusha Taifa salama.

Mhe Rais pamoja na mawimbi makubwa, dhoruba, hila, husda na njama nyingi za kumkwamisha bado amelifanya Taifa kuwa imara, tulivu na kuweka rekodi ya miradi mikubwa kutekelezwa na maendeleo kuonekana kwa macho. Nani asiyefahamu kuwa sasa kiwango Cha furaha kimeongezeka nchini?

Walidhani atakwama, lakini ameweza. Sababu ambazo zinawafanya hawa watu washinde kwenye vyombo vya habari kumshambulia Mhe Rais na Serikali yake yaani kujaribu kuonesha wao ni wema ni sababu zifuatazo:-

1. Wanamchukia Rais Samia kwa kuwa baada ya kuapishwa aliondoa tozo 232 ambazo zilikuwa zinawakwaza Wafanyabiashara na wengine walikuwa wamehamishia biashara zao nje ya nchi. Serikali ya awamu ya sita imejenga mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara, mazingira ambayo yamechochea kuongezeka makusanyo ya kodi.

2. Wanamchukia Rais Samia kwa kuwa amefanikiwa kukuza Diplomasia na mataifa ya nje zikiwepo nchi za AFRIKA mashariki ambazo kuna wakati mahusiano yaliyumba. Rais Samia amefanikiwa kuifungua Tanzania katika Diplomasia ya kimataifa ambayo imechochea kuimalisha uchumi wa Taifa. Watalii wanakuja Tanzania sasa ni wengi sana ambao wanaongeza kuingiza fedha za kigeni.

3. Wanamchukia Rais Dkt Samia kwa kufanikiwa kumaliza ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere(JNHPP) ambalo wakati anaapishwa ujenzi wake ulikuwa umefikia 33%. Walidhani Mhe Rais ataachana na mradi huo mkubwa wa kimkakati. Kitendo cha Serikali ya awamu ya sita kumaliza ujenzi wa Bwawa hilo na kuanza kufanya kazi kimewachukiza sana hawa waliotaka nchi Iendelee kuwa gizani. Rais Samia akihutubia bunge kwa mara ya kwanza alisema atatekeleza miradi yote iliyoanzishwa na JPM. Watanzania aina hii hawakuelewa walisema hawezi, leo wanamchukia kwa kuwa ameweza.

4. Wamechukizwa sana Serikali ya awamu ya sita kukamilisha ujenzi wa Daraja la Magufuli (Kigogo-Busisi) ambalo mtangulizi wake aliliacha likiwa limefikia 16%. Leo Daraja limekwisha na kazi inaendelea. Hili jambo limewachukiza hawataki Dkt Samia achukue fomu wachukue wao ambao historia zao hazijulikani ndani ya Chama na Serikali. Walitaka lisijengwe ili wafurahie kuwa amekwama.

5. Wamechukizwa sana Rais Samia kuendelea kusimamia maono ya hayati JPM ya kufufua na kuimarisha shirika la ndege la ATCL kwa kununua ndege zingine tano ikiwepo ndege ya mizigo aina ya Boing 767-300F. Kuendelea kujenga na kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini. Hili ni kero kubwa kwao na kuongeza uhasama kwa Rais wa nchi. Rais Samia aliposema Mimi na JPM tulikuwa kitu kimoja hawakuelewa.

6. Wamechukizwa sana na Mhe Rais kufufua mradi wa NHC kote nchini kwa mfano ule wa Morocco Square ulioanzishwa na kukwama mwaka 2018 yeye ameufufua na kuumaliza. Mradi wa Kawe, Mradi wa Samia Housing wa nyumba 5000 katika maeneo mbalimbali nchini. NHC ilianzishwa mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge namba 45 kwa kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora. Mageuzi makubwa ya kihistoria yalifanyika mwaka 1990 na 2008, Mhe Rais Samia amekuja kulisimamia hili kwa vitendo. Hii imekuwa karaha kwa ndugu zetu hawa waliojipanga mwaka 2021.

7. Wanamchukia Rais Samia kwa kuendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara. Ukipita Wilaya zote Tanzania ardhi inaomboleza kwa namna Mitambo inavyoendelea kuitindua ardhi na kujenga barabara nzuri za rami na changarawe. Kwa mara ya kwanza Tangu Tanzania ipate Uhuru, Serikali ya awamu ya sita ilitoa milioni 500 katika kila halmashauri kwa ajili ya barabara za vijijini. Wamechukia kuona fedha hizi zinaenda kuwasaidia Wananchi wanyonge kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji.

8. Wamechukizwa na Mhe Rais kwa kuboresha miundombinu ya shule. Serikali ya awamu ya sita imekarabati shule za zamani, imejenga shule mpya, imeongeza nyumba za Walimu na imeweza kuajiri Walimu kwa mara ya kwanza mara baada ya ajira hizi kustishwa toka mwaka 2015. Shule nyingi zilikuwa zimechoka lakini awamu hii zimeboreshwa. Haitoshi zinajengwa shule shikizi ikiwa ni mkakati wa Serikali kuinua elimu nchini na kupunguza changamoto za watoto shuleni.

9. Wanachukizwa sana na uboreshaji wa Afya. Miaka michache iliyopita watu walikuwa wanapishana angani kwenda kutibiwa India. Serikali ya awamu ya sita si tu imeongeza ujenzi wa vituo vya huduma ya Afya kwa maana Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati kila mahali, rahasha! Rais Samia ameweza kununua pia vifaa vya hospitali. Tangu tupate Uhuru tulikuwa na MRI 7 TU, lakini Dkt Samia kwa miaka 4 amenunua MRI 6. Sijui unaelewa? Tangu tupate Uhuru tulikuwa na CT scan 13 lakini Dkt Samia kwa miaka minne amenunua CT scan 32. Tunaelewana? Unadhani kwa kasi hii wanakingine cha kusema zaidi ya ajenda ambazo hazina miguu wala vichwa. Hii ni mifano michache ambayo nimeona nikupe tu uelewa mdogo.

10. Wamechukizwa sana utawala bora. Kwa miaka minne tumeona nguzo zote za utawala bora zikifanya kazi. Watu wanafanya siasa, Waandishi wa habari wanafanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria za nchi, Watu makazini wanaadhibiwa kwa kufuata Sheria, Mahakama zinafanya majukumu yake n.k Mahali ambapo hakuna utawala bora basi hofu inakuwa ni maisha ya kawaida ya watu. Hawataki utawala bora wanataka monopoly
11. Wamechukizwa sana kushusha kwa riba ya mikopo ya Wanafunzi wa vyuo vikuu ambayo imeshuka kutoka 14% mpaka single digit (7%). Hii ilikuwa ni kero kwa wasomi ambao ni wanufaika wa bodi ya mikopo. Tukumbuke 100% ya wanufaika wa mikopo hii ni watu wanaotoka familia masikini na za kati. Unapomtoza 14% ni kumfanya aendelee kuwa masikini zaidi na kuona kukopa ni adhabu.

12. Wamechukizwa na kukerwa vibaya sana na elimu bure. Serikali ya awamu ya nne ilitangaza elimu bure kutoka chekechea hadi kidato cha sita. Lakini pia iliongeza fedha ya kujikimu kwa Wanafunzi wa vyuo. Hawa wanaona hii ni kete kwa Dkt Samia hivyo wanakwazika sana.

13. Wamechukizwa na Agribusiness, huko nyuma mtu kuitwa mkulima ilikuwa ni aibu. Lakini Serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa kwenye kilimo ambapo leo mtu kuitwa mkulima ni fahari. Mwaka 2021 bajeti ya kilimo ilikuwa billion 200± leo hii bajeti ya kilimo ni Trillion 1.2. Lengo la Serikali ni kuona sasa tunaacha kuagiza mafuta ya kula nje lakini pia sukari maeneo ambayo Serikali ilikuwa inatumia fedha nyingi. Wenzetu wanakerwa na mradi wa BBT uliojiri vijana wengi na tunaona matokeo ya kilimo wanachofanya Chinangali na maeneo mengine nchini. Mbolea ya ruzuku imechangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji mkubwa na wenye tija. Haya ndiyo yanawachukiza wenzetu.

14. Wanachukizwa na miradi ya kimkakati 901 yenye thamani ya Dola 127 ambapo mwaka 2021 tulikuwa na miradi ya kimkakati 93 TU yenye thamani ya Dola 1.6 bilioni TU. Hatuoni mapinduzi haya? Urasimu umepungua ndio maana watu wengi wanakimbilia TIC kutafuta fursa.

15. Wanachukizwa na ujenzi wa Daraja la TANZANITE walitaka lisijengwe.

16. Wanakwazika na makusanyo yaliyoongezeka pale bandarini fedha zinazosaidia kwenye miradi ya kimkakati na kuongeza mishahara kwa watumishi.

Pamoja na mengine mengi yanayowakera na kuwachukiza, haya ni machache kati ya mengi ambayo mahasimu wa Samia wanakwazika. Hakuna jambo jingine, wanateswa na mafanikio ya Dkt Samia. Walishajipanga kuwa atakwama. Walijaribu kumkwamisha lakini walishindwa. Kete iliyobaki ni hii wanayohangaika nayo ambayo nayo wamekwama.

October tunatiki.
Isivyo bahati hakuna sheria inayozuia mtu kutumia utambulisho wa shahada ya udaktari kabla ya jina lake ka hiyo inatoa mwanya kwa baadhi ya watu kujikweza kielimu kwa digrii ya heshima pasipo uhalali wowote

Mfano ni maelezo haya hapa chini

Kuna shahada za udaktari wa aina nyingi. Kwa uchache kuna Shahada ya Udaktari wa Binadamu (MD), Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD), Shahada ya Udaktari wa Sheria (LLD), Shahada ya Udaktari wa Sheria za Kanisa (JCD), Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa).

Mifano ya shahada hizo inaweza kutofautishwa kwa kuwaangalia watu hawa na shahada walizonazo. Dk. Benson Bagonza (PhD), Dk. Chris Cyrilo (MD), Dk. Wilbroad Slaa (JCD), Dk. Seng’ondo Mvungi (LLD) na Dk. Jakaya Kikwete (Honoris causa).

Hakuna sheria, kanuni au mwongozo unaomzuia mtu mwenye Shahada ya Udaktari ya Heshima kuanza na utambulisho wa ‘Dk’ kabla ya jina lake, japo baadhi hawafanyi hivyo, na wale wanaopata udaktari kwa kusoma, baadhi hawapendi kuona wanaopewa kwa heshima wakitumia utambulisho huo.

Mifano ya waliotunukiwa lakini hawatumii ni pamoja na Bill Clinton ambaye ametunukiwa mara tatu, Mwl. Julius Nyerere alitunukiwa mara 8 na vyuo mbalimbali vyenye hadhi na hivi karibuni mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima na Manchester University, moja ya vyuo vikubwa sana duniani, lakini hajiiti Dk. Rashford.
 
Back
Top Bottom