Sababu za Rais kuchelewa kuchukua Maamuzi

Sababu za Rais kuchelewa kuchukua Maamuzi

Vyovyote uitakavyouita ushauri ni ushauri tu na kumbuka kwa Rais wetu amekumbana na kadhia hii ya ushauri mwingi kutokuwa mzuri. Lakini hoja yangu ya msingi ni kwamba kwa kawaida Rais hufanyia kazi ushauri ule unapotoka kwa watu wake wa karibu sana.. Sasa hapo integemeana watu wake wa karibu wana nia gani na ushauri wanaotoa wakati huo.

hao washauri wake si kawachagua yeye mwenyewe wengi wa washauri wake alikuwa nao ktk kijiwe chake cha"saigon"
 
uwezo wa kufikiri kwa watanzania zaidi ya 85% ni mdogo sana. Sehemu kubwa ya fikra zao ni kula na starehe wengi hawana mda wa kujishughulisha kujua mengine zaidi ya kula kwao.....

Wenye akili kubwa ni wachache sana na ndio huibua mambo mazito but kwa kuzungukwa na kundi kubwa la wafu wanaotembea hujikuta wanaishiwa nguvu katikati baada ya maamuzi ya zimamoto....

Hii hali ya uduni wa akili umefika mpaka ngazi za juu ambapo hata watu duni sana kifikra wanakuwa mawaziri na wafanya maamuzi.....

Leo mtanzania anafurahia kujiuzulu kwa waziri lakini hajipi muda wa kutaka hatua zaidi na hii inagharimu nchi miaka nenda rudi....

Kundi kubwa la vijana wanaotegemewa kwa mageuzi ndio hawa ambao kabla hata ya 35 years wameridhika na maisha na 90% ya maisha yao ni starehe.....

hakuna ushahidi wa kisayansi kudhihirisha kuwa wewe una uwezo mkubwa wa kufikri kuliko wengine.kama unawaona wenzio wana uwezo mdogo wa kufikri kwa sababu tu wametofautiana na wewe,basi tuelewane kuwa uwezo wa kufikri is a relative.lazima tuipe nafasi sayansi iongoze maamuzi yetu.hatuwezi kumiukumu kuwa mtu flani ni mwizi kwa sababu tu wabunge wengi wamesema!
 
Kwahiyo shida yako nini? Nani kahukumu?? Vitu vingine Kama huelewi usikurupuke kuchangia ni vema ukaenda tu kujifurahisha kwenye mada za mapenzi pengine akili yako itafit....
 
Jamani mbona serikali haijaturipa pesa zetu imechukuwa mahindi yetu mpaka sasa sisi wakulima tutaishije mbona zuluma hata sisi wanyonge kuweni na huluma rais tusadie hali mbaya sana
 
Namshauri avunje bunge. Alisuke upya halafu hao mafisadi waachwe na kisha iwe rahisi kuqashughulikia. Vinginevyo uchaguzi uwahishwe ili kuondokana na hii kadhia.

Hakuna ufisadi ambao ikilu haihusiki kwa namna moja au nyingine. Usalama wa taifa uko chini ya ikulu na wanajua kila kitu. Kuvunja bunge kutasaidia nini?
 
Vyovyote uitakavyouita ushauri ni ushauri tu na kumbuka kwa Rais wetu amekumbana na kadhia hii ya ushauri mwingi kutokuwa mzuri. Lakini hoja yangu ya msingi ni kwamba kwa kawaida Rais hufanyia kazi ushauri ule unapotoka kwa watu wake wa karibu sana.. Sasa hapo integemeana watu wake wa karibu wana nia gani na ushauri wanaotoa wakati huo.

Yaani unamuongelea Rais kama universal recipient, hao washauri unaowazungumzia taarifa wanatoa wapi??!!
Huko wanakozitoa yeye hawezi kuzifikia??!!

Hebu chukulia urais kwa uzito wake!!
 
hakuna ushahidi wa kisayansi kudhihirisha kuwa wewe una uwezo mkubwa wa kufikri kuliko wengine.kama unawaona wenzio wana uwezo mdogo wa kufikri kwa sababu tu wametofautiana na wewe,basi tuelewane kuwa uwezo wa kufikri is a relative.lazima tuipe nafasi sayansi iongoze maamuzi yetu.hatuwezi kumiukumu kuwa mtu flani ni mwizi kwa sababu tu wabunge wengi wamesema!

Ndio ni relative ila unapokuwa below expected level in a given context wewe unakua jjuha tu no science needed for this task, be it realism nor positivism!!!
Hao wabunge wengi wameamua kutoka hewani??? hawana base ya hiyo convention??? PAC walibuni taarifa? ??na kama kweli spika aliruhusu taatifa isiyo na mashiko ijadiliwe???!!!

lusungo uko sawa sana tuna mizigo mingi sana kwenye jahazi!!!
 
Last edited by a moderator:
Raia anaweza kunyamaza tu bila kuifanyia kazi ripoti za PAC .
Hakuna sheria inayomlazimisha kukubali maamuzi ya kamati za bunge.
Na sasa kila mtu mwenye kufikiri anajua wazi hii ilikua moja ya propaganda chafu dhidi ya serikali
Tume ile ya zitto iliingiliwa na haikufanya maamuzi kwa matakwa ya uhalisia bali walifata matakwa ya watu wengine.
Rais sana sana ataunda tume huru kuchunguza tena na pia kuwachunguza wabunge kama walipewa pesa kuleta fitina
 
Ndugu wana JF
Naweza kusema kwa usahihi kabisa kuwa sasa nimemuelewa Rais Kikwete kwa nini anasita kufanya maamuzi ya kutengua uteuzi wa mawaziri na watumishi wa umma waliohusika katika ufisadi wa ESCROW Account. Sababu ya kusema hivyo ninayo tena ni ya msingi, nitaeleza kama ifuatavyo;

Baadhi ya watuhumiwa kutojumuishwa
Kuna kashfa nyingine zinakuja

Akiwemo yeye mwenyewe,
"Pesa zilipwe kama alivyoshauri mwanasheria mkuu" ilinukuu barua iliyosainiwa na Bwana Mbena kwa niaba ya Rais kwenda kwa gavana wa BOT, kwa kauli hii anakwepa wapi uhusiaka wake?

Pia kutakuwa na uhusika wake si ashatufanya watanzania wabwege kwamba hakuna lolote tunaweza kufanya, jeuri yao inaisha Oct 2015
 
Tangu mwanzo haikutarajiwa kuwa maazimio ya Bunge yatatekelezwa kwa urahisi. Ilikuwa wazi kuwa serikali kwa ujumla wake iliridhia fedha za escrow akaunti kulipwa PAP. Hivyo swali kubwa ni nani awajibishwe na nani aachwe?
 
Ushauri upi unazungumzia, pre emptive au remedial??!!!

Rais anapata ushauri kutoka kila pahala, lakini akifanya maamuzi, maamuzi ni yake.

Kinyamwezi rais anasema "the buck stops with me".

Kwa hiyo katika watu wanaojua habari za wajibu wa rais, hakuna utetezi wa kusema "alishauriwa vibaya".

Ni kazi yake kutoshaurika vibaya. Akishauriwa vibaya kashindwa jazi.
 
Jambazi kumwajibisha mwenzake kwa wizi ambao wameshirikiana ni vigumu labda tungewaomba CIA waweze kuwahoji watuhumiwa kwa kutumia mbinu walizotumia kuhoji watuhumiwa wa ugaidi
 
Binafsi nilishasahau ndo kwanza unanikumbusha... vijana wa Kitanzania tunaowatarajia eti wawe ndo wapiga kura wa kuiondoa CCM madarakani hivi sasa tupo bize na issue ya Zari na Diamond, Diamond na Davido, Idris Sultan na tuzo ya BBA na mara moja moja tunakumbushia bifu la Kiba na Diamond... hizo ndo habari za mjini kwa sasa manake hata kujiandikisha uchaguzi wa serikali za mitaa tulisahau!!

Hivi Eskroo inahusu nini vile? Hivi Naibu Waziri Aggrey Mwanri na yeye si yupo kwenye eskroo, au?

Watanzania mda mwingi huupotezea kwenye mabaa, story zikiisha huanza majungu, jaribu kuzichunguza story nyingi za kwenye ma-Bar utabaini hilo.
 
Tangu mwanzo haikutarajiwa kuwa maazimio ya Bunge yatatekelezwa kwa urahisi. Ilikuwa wazi kuwa serikali kwa ujumla wake iliridhia fedha za escrow akaunti kulipwa PAP. Hivyo swali kubwa ni nani awajibishwe na nani aachwe?

Mhongo aking'olewa lazima na Mwigulu,malima,na Kigoda nao watoswe, huku makatibu wakuu na naibu katibu wakuu pia Gavana na mkurugenzi wa fedha BOT nao watasombwa na mafuriko, Rais akifanya hivi itakuwa Mzuka ile mbayaa....
 
Anataka kuitangaza nchi kwa kuvunja rekodi za kitabu cha Guiness... kie kie kie!
 
Hilo la kushitakiwa kwa Tanzania bado sana.

Na jinsi tulivyo wepesi wa kuwasahau sitashangaa baada ya mwaka mpya tukawa tumesahau kabisa haya mambo ya escrow.

Nani atamshitaki nani?

*Sitti Mtemvu licha ya kuwa busted, kalivua taji na sasa watu tushasahau na uwezekano wa yeye kutofikishwa mbele ya vyombo vya sheria ni mkubwa sana*

Kuna Mabomu makali yanakuja ambayo yataifunika Escrow na kuonekana ni cha mtoto
 
Nchi hii mda wa kufanya Kazi huwa ni Mdogo sana,watu hupoteza masaa mengi kwenye Ulabu sanjari na story za KU-copy, huko maofisini mda wa kunywa chai ni mkubwa mno hata runch nayo huchukua masaa changanya na kuugua, kwenda kwenye misiba na visingizio kibao.Nchi hii hakuna mwenye Uwezo wa kukemea hata wale wavaa Suruali chini ya Makalio ( mlegezo) sembuse haya ya michongo! Hapo wa kwanza kufukuzwa alipaswa awe Waziri wa Fedha na Gavana kwani ndiyo waliidhinisha malipo.
 
Tangu mwanzo haikutarajiwa kuwa maazimio ya Bunge yatatekelezwa kwa urahisi. Ilikuwa wazi kuwa serikali kwa ujumla wake iliridhia fedha za escrow akaunti kulipwa PAP. Hivyo swali kubwa ni nani awajibishwe na nani aachwe?

Mhongo aking'olewa lazima na Mwigulu,malima,na Kigoda nao watoswe, huku makatibu wakuu na naibu katibu wakuu pia Gavana na mkurugenzi wa fedha BOT nao watasombwa na mafuriko, Rais akifanya hivi itakuwa Mzuka ile mbayaa....
 
Mhongo aking'olewa lazima na Mwigulu,malima,na Kigoda nao watoswe, huku makatibu wakuu na naibu katibu wakuu pia Gavana na mkurugenzi wa fedha BOT nao watasombwa na mafuriko, Rais akifanya hivi itakuwa Mzuka ile mbayaa....

Duuh! hayo kweli mafuriko!
 
Yaani unamuongelea Rais kama universal recipient, hao washauri unaowazungumzia taarifa wanatoa wapi??!!
Huko wanakozitoa yeye hawezi kuzifikia??!!

Hebu chukulia urais kwa uzito wake!!

Ndio uko sahihi kabisa. Rais ni Universal receipient kwa maana hupokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ukiwemo hata "udaku" wa mtaani. Kuna jamaa yangu mmoja alinitonya kuwa magazeti ya udaku yanasomwa hadi ikulu. Kwa hiyo usishangae Rais akiwa universal receipient.
 
Back
Top Bottom