Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
Ndugu wana JF
Naweza kusema kwa usahihi kabisa kuwa sasa nimemuelewa Rais Kikwete kwa nini anasita kufanya maamuzi ya kutengua uteuzi wa mawaziri na watumishi wa umma waliohusika katika ufisadi wa ESCROW Account. Sababu ya kusema hivyo ninayo tena ni ya msingi, nitaeleza kama ifuatavyo;
Baadhi ya watuhumiwa kutojumuishwa
Ukifuatilia vizuri ripoti ya PAC ailiyojikita katika uchunguzi wa CAG, PCCB na TRA kuna ushahidi wa bila shaka kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda hawezi kukwepa kitanzi, Waziri wa fedha na katibu wake mkuu pamoja na Gavana wa Benki Kuu pia hawawezi kukwepa kitanzi cha kuwajibishwa. Hali kadhalika Waziri wa Viwanda na biashara pamoja na BRELA yake hawaponi kwani walikuwa na uwezo wote kubaini uhalalali wa kampuni feki ya PAP. Lakini cha kusikitisha ni kwamba bunge limeridhia kukwepesha kitanzi kwa wote hao. Jambo hili linampa ugumu Rais kutekeleza mapendekezo ya bunge kwani itaonekana naye anapendelea kwa kuwajibisha baadhi ya watuhumiwa huku wengine wakiachwa.
Kuruhusu uchunguzi zaidi
Sababu ya pili ni kwamba; Kutokana na kosa la bunge la kukwepesha kitanzi kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa umma, ama kwa makusudi ama kwa kuzidiwa nguvu na baadhi ya mafisadi na wapambe wao, Rais anaogopa kuingia katika mtego huo hivyo kuruhusu uchunguzi zaidi ili itafutwe namna ama ya kuwaingiza wahusika wote bila kusaza ama kuwasafisha baadhi yao kwa kigezo kuwa walilazimika kutenda hayo waliyotenda kwa nia njema wakitekeleza ushauri wa wataalamu hasa mwanasheria mkuu. Katika hili pia inawezekana watuhumiwa wakatenda makosa mengine yanayowahusisha moja kwa moja na sakata hilo (kama inavyosemekana kuwa muhongo anagawa rushwa ili asafishwe humu na katika mitandao mbalimbali )hivyo kuepuka lawama kuwa wanaonewa.
Kuna kashfa nyingine zinakuja
Kama "tulivyoumwa sikio" na mwenyekiti PAC Bwana Zitto Kabwe, kuna kashfa nyingine nyingi zinakuja ambazo huenda zikawakumba mawaziri hawa hawa hivyo itakuwa rahisi kushindilia maamuzi ya bunge. Kwa mfano sulala la uagizaji wa sukari kiholela bila kujali athari za viwanda vya ndani, hapo waziri mkuu na mawaziri wa fedha na yule wa viwanda na biashara hawawezi kukwepa lawama. Huenda safari hii ukapatikana ushahidi wa kuwaingiza mojakwa moja katika tuhuma, hivyo kazi ya Rais kuwatimua itakuwa imerahishishwa mno. Pia kuna kashfa katika mradi wa bomba la gesi, tuhuma hizi hazitamwacha salama waziri muhongo na katibu wake mkuu bwana Maswi. Hapa tena kazi ya Rais itakuwa rahisi tu kama kumsukuma mlevi.
Kutokana na sababu nilizoeleza hapo juu, Rais anachelea kuchukua maamuzi sasa kwani akimwacha Waziri mkuu na mawaziri wa fedha na waziri wa viwanda na bishara, atakakuwa hajafanya kitu kwani huenda Januari mwakani wakati wa Bunge lijalo akalazimika kuvunja baraza zima kwa kutimuliwa waziri mkuu kutoka na vuguvugu la kashfa zinazomwandama katika ESCROW, sukari, gezi n.k. Rais hataki kupoteza muda kuwatimua baadhi ya mawaziri sasa kisha kuteua wengine ambao mwezi januari mwakani watalazimika kuondolewa kutoka na kutimuliwa waziri mkuu. Hivyo ngoma ya ESCROW itahitimishwa mwakani, japo inauma lakini huo ndo ukweli.