Sababu Za Mwanaume Kuwa Na Wanawake Wengi

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kila mtu na mapenzi yake apendayo.
Kila mtu na malengo yake kwenye mahusiano. Mwanaume kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja ni jambo la kawaida, pia ni vyema afanye hivyo. Lakini inategemea maamuzi ya mtu binafsi. Hivyo, wakati unaamua angalia sababu hizi. Twende nyuma kwanza, zamani utajiri ulitegemea nguvu ya familia.

Kwahiyo kadri mnavyokua wengi thamani yenu na nguvu yenu inaongezeka na mnaweza kujilinda, kuzalisha mazao mengi vilevile mnaweza kuvamia wanyonge na mkashinda kirahisi. Kibaiolojia tunafahamu kuwa mwanamke ana ukomo wa uzao na mwanaume ana nafasi kubwa ya kuendelea kuzaa hata kama mke wake mmoja akiwa amefikia ukomo, hivyo basi ili kulinda nguvu na utajiri wa familia ilibidi mwanaume aongeze mwanamke amzalie watoto wengine.

Turudi sasa, kilichobadilika sasa ni kwamba hakuna haja ya kuwa na familia kubwa ili uweze kuilinda familia, polisi wapo. Lakini kibaiolojia hakuna kilichobadilika. Bado kama wanaume tunataka kuwa na urithi mkubwa, bado tunataka majina yetu yawe makubwa, bado tuna ile hamu ya kuwa na wanawake wengi. Haijafuka kwenye damu.

Mwanamke mmoja ana mudi tofauti kwenye mwezi.

Wengine husema ‘wanawake hawaeleweki’.

Wanaume wengi hawawezi kuyahimili mabadiliko hayo. Suluhisho ni kwenda kwa mwanamke mwingine hadi mwanamke wa kwanza awe mtulivu amrudie. Wapili nae akiwa na mudi tofauti, atarudi kwa wa kwanza, na mzunguko utaendelea hivyo.

Mwanamke ndiye anayechagua kuwa na mwanaume au la.
Wanawake wenyewe ndio wapo tayari kuwa na mwanaume mwenye wanawake wengi. Japo anaweza asilikubali hili wazi. Sababu, kwake huyo mwanaume ndo mshindi na jasiri kuliko wanaume wengine.
Wanawake wanapenda kuwa na wanaume jasiri na washindi.

Wanawake wana sehemu kubwa ya kuchagua kuliko wanaume.
Mwanamke mmoja wa kawaida tu anaweza kuwa anafukuziwa na wanaume hata watano.
Lakini mwanaume mmoja anaweza asifukuziwe na mwanamke hata mmoja.

Inapelekea hata ukiachana na mwanamke tayari ana mbadala wako, wakati we unabaki kuhangaika kurudiana naye. Ili kuweka mchezo sawa nawe ni muhimu uwe na mbadala pia. Usibaki ukaumia.

Mara nyingi mwanamke ana mtu wa kuchukua nafasi yako. Hata kama asipokuambia. Wewe pia kama mwanaume uwe na mtu wa kuchukua nafasi yake. Unakuta mwanamke wako anachombezana na wenzake sehemu anayoshughulika.

Ujue mbadala wako unaandaliwa.
Sababu kubwa kwamba mwanamke anamheshimu zaidi mwanaume ambaye anajua ana mwanamke zaidi ya mmoja. Anajua akizingua tu ameachika. Mwanamke anapenda kuacha kuliko kuachika, anaogopa kuumia. Hivyo, atajitahidi yeye awe namba moja. Katika kupambania huko, ni vigumu wewe kama mwanaume kuachwa. We kazi yako inakua kumridhisha kulingana na anavyojitolea kwenye mahusiano.
 
Kila mtu na mapenzi yake apendayo.
Kila mtu na malengo yake kwenye mahusiano. Mwanaume kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja ni jambo la kawaida, pia ni vyema afanye hivyo. Lakini inategemea maamuzi ya mtu binafsi. Hivyo, wakati unaamua angalia sababu hizi.
Mbona hapo sijaona sabb za msingi.......yote hata ukiwa na michepuko ya kutosha yanafanyika sio lazima uoe.
 
Sababu za mwanaume kuwa na wanawake wengi ni UMALAYA Tu.
Sijui hata kama umesoma ukaelewa,naweka nukuu kutoka main post!

"Inapelekea hata ukiachana na mwanamke tayari ana mbadala wako, wakati we unabaki kuhangaika kurudiana naye. Ili kuweka mchezo sawa nawe ni muhimu uwe na mbadala pia. Usibaki ukaumia"

Ukisoma hapa unaelewa nini,mimi naona amekumbusha wanaume kuiga utaratibu wa wanawake,tunaweza kusema kuuiga umalaya wao kwa kujiandaa mapema ili ngoma iwe droo.
 
Sijui kama umesoma ukaelewa,naweka nukuu kutoka main post!

"Inapelekea hata ukiachana na mwanamke tayari ana mbadala wako, wakati we unabaki kuhangaika kurudiana naye. Ili kuweka mchezo sawa nawe ni muhimu uwe na mbadala pia. Usibaki ukaumia"

Ukisoma hapa unaelewa nini,mimi naona amekumbusha wanaume kuiga utaratibu wa wanawake,tunaweza kusema kuuiga umalaya wao kwa kujiandaa mapema ili ngoma iwe droo.
Okay twende tuishi kwenye maneno ya mtoa mada.

Ameandika "Wanawake wana sehemu kubwa ya kuchagua kuliko wanaume.
Mwanamke mmoja wa kawaida tu anaweza kuwa anafukuziwa na wanaume hata watano.".

Sasa mimi kufukuziwa na wanaume watano au zaidi ndio pakufanye na wewe utafute wanawake wa mbadala?
 
Mimi ni mwanaume ninaependa kuwa na wanawake wengi ,kiufupi hakuna sababu nyingne inayonipelekea kuwa hivyo zaid ya tamaa tu kama za fisi, nasioni ninachopata zaid ya mtu mwenye mwanamke mmoja , chakushangaza sitaki ushauri wakubadilika kwa sababu ninajua ninacho kifanya.
Hahaha ushauri siku hizi ni lazima.

Acha zinaa.
 
Kila mwanamke ana taste yake ya pekee ndio maana mtu anakuwa na wanawake tofauti tofauti
Na taste ya pekee sio s3x tu ni kuanzia namna ya kuongea mawazo muonekano etc
Tatizo hyo raha utakayopata ata ukiwa na 1000 haina ukomo wake utazdi kuitafuta tu kumbe raha ipo kichwani mwako , pale unaenda saka utelezi tu mkuu , utamu upo kichwani tu na sio jambo halisi ni illusion tu.
 
Tatizo hyo raha utakayopata ata ukiwa na 1000 haina ukomo wake utazdi kuitafuta tu kumbe raha ipo kichwani mwako , pale unaenda saka utelezi tu mkuu , utamu upo kichwani tu na sio jambo halisi ni illusion tu.
Nimekwambia sio suala la s3x tu
Unaweza kuwa na mtu tofauti sabb ya mawazo yake muonekano lafudhi etc
 
Back
Top Bottom