Nilibahatika mwaka jana kwenda kumpeleka mtoto kwenye interview ya kidato cha tano. Nilipokuwa pale tulikuta wazazi fulani ambao watoto wao wamemeliza kidato cha nne mwaka juzi wakiomba uongozi wa shule watoto wao wafanye usaili ili wapata kusoma kidato cha tano hapo Mirian. Nilipofuatilia sababu ya wazazi kuomba, niliambiwa kuwa watoto wao walitaka kuanzisha mgomo walipokuwa kidato cha tatu, pamoja na adhabu nyingine, uongozi uliamua kuwa hawataruhusiwa kuendelea kidato cha tano katika shule hiyo. Hii ni dalili moja ya kuwa shule hii ina taratibu wanazozifuata, na hili ni jambo la msingi sana kwenye maendeleo ya mtoto shule. Na sijui hii dhana ya kuwa waalimu wa shule hizo hawana sifa inatoka wapi, tukumbuke kuwa sifa ni jambo moja lakini hata kama una sifa za mwalimu wa kemia, unawezaje kufundisha wakati huna maabara , vitabu vya kiada wala ziada.
Kumekuwa na matatizo mengi sana kwenye mfumo wetu wa elimu, wanasiasa wameanza kutuaminisha kuwa shule ni majengo na si taasisi. Matokeo yake, tunaendelea kuwa na majengo na wanafunzi bila kuwa na uwiano wa wanafunzi wa mwalimu. Wakati darasa la Mirian lina wanafunzi 35 maximum, kuna shule (Kawe ukwamani) mkondo mmoja una wanafunzi 150 na darasa wanafunzi 600 wakisoma kwa session ya asubuhi na mchana, Kuna mwalimu hata mwenye bidii kiasi gani anaweza kufuatilia maendeleo ya mtoto mmoja mmoja? Lakini lazima uwepo mfumo wa kuwaangalia walimu ( wakaguzi wa elimu), siku hizi sijui hata kama wakaguzi wapo, na kama wapo wanafanya kazi yao sawasawa. Sasa haya ni matatizo yanayozipata sehemu kubwa ya shule zetu za serikali, kinyume chake shule kama Marian, ina waalimu ( ambao uongozi unahakikisha wanafanya kazi yao sawasawa), kuna vitabu, maabara na wanafunzi wana shughuli moja tu, kusoma. Wana test za mara kwa mara kupima wanafunzi, kwanini wasifaulu vizuri wakipewa mitihani.
Mimi siamini kuwa Marian ina magenius, bali mazingira mazuri ya kusoma kitaasisi (walimu, vitabu, maabara, uongozi, chakula na malazi) unachangia sana wao kufanya vizuri katika masomo yao.
Kuhusu suala la makabila na dini za wanafunzi wanaochanguliwa kuingia shule hiyo, naona inachangiwa zaidi na background za hao watoto. Kuna ukweli kuwa makabila fulani wao elimu ilianza kutiliwa maanani zamani kidogo, na kwa mtazamo wangu ilikuwa kosa kuwapa upendeleo wanafunzi kutoka mikoa iliyokuwa nyumba kieimul kuingia sekondari hata kwa maksi za chini, kama uamuzi ule ulikuwa urudiwe ingekuwa kutengenza shule nzuri huko huko na kuwaandaa wanafunzi wataopata viwango vya ufaulu vinayvotakiwa kuliko kuwabeba.