Sababu za Marrian Girls ya Bagamoyo Kung'aa!.

jibu swali,acha kuzunguka mbuyu haujaulizwa huko shule za govt huwa mnafanya nini??kakuuliza miaka yote hiyo zaidi ya kumi ambayo marian inaongoza walikuwa wanaiba mitihani??

jibu ni ndiyo.
 
Hiz shule ni nzur lakin watoto wanalemaa hasa hiz za Bei kubwa kuna utofauti mkubwa na seminari za kikatorik kule mtoto anatoka yuko ful kwenye life cjui kwa sabab kuna kazi kama gerezan(hasa za mikoan) lakin huwa wakiingia chuo, wanakuwa na wknes kwa madem, seminiari zinafundisha maisha sana, nadhan kuliko shule zozote kwa Hapa tz. MI nadhan serikal inabid iige mfumo wa seminar(ukiondoa yale maswala ya kikatolik zaid) kama inataka iongeze idad ya ufaulu. Kumbuka hizi shule ni mara chache sana zinakuwa na walimu wenye hata hizo diploma, yaan wengi Wao tena hawana hata hizo pass za kuingia chuo. Je inakuwaje mtu aliye na four ya form 6, anakuwa anauwezo wa kumfundisha mtu na akapata 1? (karibia shule zote za serikali zina walimu wa ngaz ya diploma kwenda juu, lkn hazifaurish kama hiz seminar
hAPO KWENYE UBLUU UMENENA.MIMI MWENYEWE NIMEFUNDISHWA NA WALIMU AMBAO HAWAKUPATA HATA ELIMU YA DIPLOMA WALA DEGREE LAKINI NILIELEWA SANA HADI LEO HII.NILIPOENDA A LEVEL NIKAANZA KUONANA NA HAO WANAITWA WANADEGREE. KWA HAKIKA NILIFELI NA SIKUWAELEWA NA NILIWADHARAU SANA.MIMI HUWA NAISHANGAA SERIKALI INAPONG'ANG'ANIA KUWA WALIMU WAWE NA DIP AU DEG.MBONA SEMINARI ZINAONGOZA NA WALIMU WAKE WENGI NI FORM 6 LEAVER.?ELIMU SIO CHETI NI UWEZO.
 
Sio wote kuna wengine ni vipanga kwelikweli hadi chuo...sitamsahau dada mmoja alisoma A-level Marian PCM alitukimbiza balaa hadi tunamaliza chuo..na ndie aliyeongoza mwaka huo kwa G.P.A kubwa pale udsm...my point is kuna wengine kweli ni dhaifu sana ila wengi wao wanajitahidi sana...sio wao tu mbona hata wale vipanga wa Mzumbe,Ilboru,Tabora boys n.k wakifika chuo wanapotea vibaya..ni akili ya mtu na juhudi binafsi..Chuo ni tifauti sana na secondary..

Nimependa reasoning yako.
 
kaka wewe mwalimu nini wa marian???........umeshawai kusikia ilboru,mzumbe,makongo,azania na st antony zikijitangaza??.......hapa point ni ileile kama kweli wanatoa elimu bora wachukue vilaza wawafundushe wakiwatoa ndo tutasema kweli ile shule kama kufahuru wanafahuru ilboru,aza,benja na mishule mingi tu msilete thread za kuadvertise shule.

Hii sio thread ya kuadvertise shule, wala Marian haihitaji kujitangaza...

Vilevile angalia unavyoandika 'kufahuru'

Kwanini wawe na low standards kuchukua vilaza, na ukilaza unatokana na shule au akili ya mwanafunzi mwenyewe ? Wao ni wafanyabiashara na wana target zao na wanamalengo yao kila mwaka wajiboreshe vipi, kwanini wakatafute vilaza kuprove kuwa wao ni best?

Hizo reasoning za kusema UDSM wanakuja kufeli etc etc, inategemea na juhudi binafsi ya mwanafunzi, pale masister wakiona umeshuka kiwango u either repeat a class or u r returned muda uliopo shule ni wa kusoma na si mambo mengine

Unapoingia chuo huna kengele ya kukuhimiza kuwahi, huna roll call, huna fimbo, huna adhabu,huna sister wa kusimamia umeenda prep usiku, usipokuwa makini na kilichokuleta utafeli tu!
 
Wadau acheni chuki za kishamba, Kama wewe hukupata nafasi ya kusoma shule nzuri usiponde wenzako vilaza, HAKUNA MTU ANAYEPENDA SHIDA NA NAJUA HATA WEWE MTOA MADA UNATAMANI UNGESOMA SHULE NZURI AS HAKUNA ASIYEPENDA MAISHA MAZURI YALIYOZUNGUKWA NA VITU VIZURI KWENYE MAZINGIRA MAZURI,,

Marian galz are good, my sister goes there na alikuwa Kipanga mpaka chuo tellecom na alibakizwa tutorial udsm, na si yeye tu hata mashoga zake aliosoma nao wote waligraduate vizuri na wana kazi nzuri, sasa unaesema wanadisco kwa research ipi?

nimesoma chuo Mzumbe na hata hao wa shule za serikali mzumbe, kibaha, ilboru na nyinginezo walikuwa kibao BAF graduates of 2010 but tuliongozwa na demu kutoka hizo shule mnaoziita za kutafuniwa jina lake linaaza na P. na hata group lake wote aliotoka nao hizo shule za mnazoponda walipiga gpa nzuri na kuajiriwa Big four auditing firms soon baada ya kumaliza chuo bila kuzunguka na vibahasha na CV mtaani

So acheni majungu kama hamkupata nafasi ya kusoma mazingira mazuri, work hard ili mwanao akasome shule nzuri,
 
jibu ni ndiyo.

Uwe serious na mawazo yako. Kweli miaka 10 wanaiba wasikamatwe, Sasa hata Epiphany primary school (hii ni shule ambaye mmiliki wake ni huyo wa marian) nayo anaiba mitihani maana watoto wake wa pale hakuna anayekwenda shule za kata, wote wanakwenda shule za vipaji/ govt school. tafakari semi zako
 
Kubali kataa io ni mazingira ya rushwa imetengenzwa, 150 > 3000 wapi na wapi..! hadi rushwa ngono lazma ipo. Watu watapigwa njenje apo hawatakaa waamini

Mkuu nadhani hukufanya utafiti kabla ya kuandika. Kwa kweli ondoa kabisa hilo wazo la Rushwa. Uliza wazazi na watoto wenyewe haki tupu inatendeka pale Marian. Hata wanaokosa wanaridhika kabisa.

Huenda una ushahidi, but Marian wana Integrity ya hali ya juu. Manager wa shule Rev. Fr. Bayo ni mtu wa haki kabisa.

By the way sababu moja ya mafanikio ya shule hiyo ni Discipline, kuanzia kwenye management hadi wanafunzi. Na wazazi hukimbilia hilo hasa kwa watoto wao wa kike.
 
Mkuu ondoa kabisa hilo la Rushwa. Uliza wazazi na watoto wenyewe haki tupu pale Marian. Hata wanaokosa wanaridhika kabisa.

Huenda una ushahidi, but Marian wana Integrity ya hali ya juu. Manager wa shule Rev. Fr. Bayo ni mtu wa haki kabisa.

Asante kwa kuwaelimisha watu. Nimekuja ona kuwa watu hawaamini kuwa Marian wana integrity ya hali ya juu. That excellent performance wanadhani wanaiba mitihani. jamani huwezi kuba mitihani miaka 10 mfululizo bila kukamatwa. Sasa na marian boys kuwa wa kwanza form 2 kanda ya pwani wameiba mitihani. Lo huyu father Bayo hafanyi kazi ingine ila kuiba mitihani ya darasa la saba (maana ana epiphany primary school ambayo nayo inafanya vizuri), mitihani ya form 4, mitihani ya form 6!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hAPO KWENYE UBLUU UMENENA.MIMI MWENYEWE NIMEFUNDISHWA NA WALIMU AMBAO HAWAKUPATA HATA ELIMU YA DIPLOMA WALA DEGREE LAKINI NILIELEWA SANA HADI LEO HII.NILIPOENDA A LEVEL NIKAANZA KUONANA NA HAO WANAITWA WANADEGREE. KWA HAKIKA NILIFELI NA SIKUWAELEWA NA NILIWADHARAU SANA.MIMI HUWA NAISHANGAA SERIKALI INAPONG'ANG'ANIA KUWA WALIMU WAWE NA DIP AU DEG.MBONA SEMINARI ZINAONGOZA NA WALIMU WAKE WENGI NI FORM 6 LEAVER.?ELIMU SIO CHETI NI UWEZO.

Kwa hiyo wewe ungependa mambo yawe holela?

Kumbuka mwalimu hawi mzuri kwa kuwa ni Form VI wala mbaya kwa kuwa ni wa Dip au Degree. Kuna walimu wengi wazuri sana wenye diploma au Degree pia. Na kuna Form VI ambao ni mabomu. General statements are very dangerous and, in most cases, fallacious.

We must have policies and standards anyway.
 
ni sawa tu na shule za enzi zile za serikali "special schools"
inachukuliwa cream tu,hayo mengine ya ulegelege chuo ni tabia/life style ya mhusika
 
hivi Udsm ni chuo basi? Nakumbuka long time kitambo wkt niko VET SUA, watu waliokuwa wakidisco pale walikuwa wanakimbilia Udsm. Mfano halisi ni classmate aliedisco mwaka wa 3. (NB Veterinary medicine ni miaka5) alipokuja udsm alikimbiza mbaya huko huko engineering.
So ukitaka kuonyesha ugumu wa shule either refer SUA or Muhimbili. Not udsm generally

One thing i dont understand is hapa naona most people mnashindana kuonesha kwamba wenye akili ni wale wanaofaulu sana kwenye elimu ngumu sio elimu bora. wat is there to brag abt kwamba umefaulu sana kwenye chuo kama UD cha miaka hii. We all know most students wanafail kutokana na matatizo mengiiiiiii ambayo hata kuyalist nackia uvivu(eg mkopo matatizo, migomo,siasa,vitendea kazi,maprofesa kuwabania wanafunzi,rushwa, rushwa ya ngono,nk). hata hao wanaofanikiwa kufaulu sana most of them are incompetent hata wakienda kwenye soko la east africa tu hawauziki cjui la dunia. Mfano mzuri ni kila siku hapa tunavyogopa upinzani na kenya kwenye soko la afrika mashariki. wakenya watachukua kazi zetu.
 
Hakuna cha ajabu kuhusu hao watoto. tatizo kama taifa tumepoteza muelekeo katika elimu. Inatia aibu na kusikitisha sana katika hili. Suala la ubora katika elimu inaonekana ni msamiati mgumu sana kwa serikali yetu. Ni muhimu kama taifa tukatambua kuwa njia iliyobora zaidi katika kugawana keki ya taifa ni kupitia elimu bora. Nje ya hapo ni usanii.
 
hizo sio mbwembwe, hivyo ndivyo inavyotakiwa,....hata mimi shule yangu natarajia kufanya mchakato wa aina hiyohiyo....safi sana...

Wewe hujaelewa mantiki, asiyejuaa maana .................................
 
UPDATE
Matokeo ya mtihani wa kujiunga Marrian Girls ya Bagamoyo yalitoka kesho yake Jumapili jioni kwa wazazi wa watoto wao walioshinda kujulishwa kwa simu na kesho yake Jumatatu asubuhi yalibandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa shule na kwenye ile ofisi yao iliyopo Msimbazi Center.

Jumla ya wanafunzi 120 ndio waliochaguliwa cut off point ni wastani wa marks 35 chini ya 50.

Nimeishuhudia marking scheme yao, mtihani wao sio tuu ulikuwa mgumu bali pia ulikuwa a bit tricky ili wanafunzi wale tuu wenye IQ above average ndio waliofaulu.

Nimethibitisha beyond reasonable doubt kuwa mchakato wa kuipata Marrian Girls ya Bagamoyo ni mchakato wa haki wenye maximum transparency na waliochaguliwa wote walistahili, hakuna upendeleo wa aina yoyote na hakuna deals.

Ila pia niliposoma majina ya ubini ya wengi walioshinda idadi kubwa ni majina ya watu kutoka makabila fulani fulani ambayo yanatambulika kirahisi. Lazima tukubali, tukatae, huu ni ukweli isiopingika kuwa japo Watanzania ni wamoja na hatuna ukabila, ila pia yapo makabila ambayo yamebarikiwa kwa wengi wao kuwa na akili kuliko makabila mengine.

Pia mtihani wa kujiunga na shule hii haukubagua dini, yaani watu wa dini zote wamefanya interview ila kwenye matokeo very very unfortunately majina mengi ni ya dini fulani na sikubahatika kuyaona majina ya dini nyingine!.

Mwalimu alipofanya affimative action ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za elimu, pia alitakiwa afanye vivyo hivyo kwa affimative actions ili watu wa dini wapate fursa sawa kupata elimu bora!

Naomba Kuwakilisha.

Pasco.
 
Kaka em taja basi ilo kabila mbona uwasilishaji umetuacha na maswali mengi sisi wasomaji.
 
Mkuu nadhani hukufanya utafiti kabla ya kuandika. Kwa kweli ondoa kabisa hilo wazo la Rushwa. Uliza wazazi na watoto wenyewe haki tupu inatendeka pale Marian. Hata wanaokosa wanaridhika kabisa.

Huenda una ushahidi, but Marian wana Integrity ya hali ya juu. Manager wa shule Rev. Fr. Bayo ni mtu wa haki kabisa.

By the way sababu moja ya mafanikio ya shule hiyo ni Discipline, kuanzia kwenye management hadi wanafunzi. Na wazazi hukimbilia hilo hasa kwa watoto wao wa kike.


Nidhamu ndio msingi wa mafanikio ya shule hiyo. Hata walimu kama hufikii standard ya nidhamu yao unatimuliwa. Na wanafunzi hivyo hivyo.
 
wakuu hizo spoon feeding zinawamaliza hao watoto maana nakumbuka miaka kadhaa nilikuwa UDSM campus ya UCLAS wengi wa wale watokao hizo ST fulalni fulani ni hoi balaa.
 
Nilibahatika mwaka jana kwenda kumpeleka mtoto kwenye interview ya kidato cha tano. Nilipokuwa pale tulikuta wazazi fulani ambao watoto wao wamemeliza kidato cha nne mwaka juzi wakiomba uongozi wa shule watoto wao wafanye usaili ili wapata kusoma kidato cha tano hapo Mirian. Nilipofuatilia sababu ya wazazi kuomba, niliambiwa kuwa watoto wao walitaka kuanzisha mgomo walipokuwa kidato cha tatu, pamoja na adhabu nyingine, uongozi uliamua kuwa hawataruhusiwa kuendelea kidato cha tano katika shule hiyo. Hii ni dalili moja ya kuwa shule hii ina taratibu wanazozifuata, na hili ni jambo la msingi sana kwenye maendeleo ya mtoto shule. Na sijui hii dhana ya kuwa waalimu wa shule hizo hawana sifa inatoka wapi, tukumbuke kuwa sifa ni jambo moja lakini hata kama una sifa za mwalimu wa kemia, unawezaje kufundisha wakati huna maabara , vitabu vya kiada wala ziada.

Kumekuwa na matatizo mengi sana kwenye mfumo wetu wa elimu, wanasiasa wameanza kutuaminisha kuwa shule ni majengo na si taasisi. Matokeo yake, tunaendelea kuwa na majengo na wanafunzi bila kuwa na uwiano wa wanafunzi wa mwalimu. Wakati darasa la Mirian lina wanafunzi 35 maximum, kuna shule (Kawe ukwamani) mkondo mmoja una wanafunzi 150 na darasa wanafunzi 600 wakisoma kwa session ya asubuhi na mchana, Kuna mwalimu hata mwenye bidii kiasi gani anaweza kufuatilia maendeleo ya mtoto mmoja mmoja? Lakini lazima uwepo mfumo wa kuwaangalia walimu ( wakaguzi wa elimu), siku hizi sijui hata kama wakaguzi wapo, na kama wapo wanafanya kazi yao sawasawa. Sasa haya ni matatizo yanayozipata sehemu kubwa ya shule zetu za serikali, kinyume chake shule kama Marian, ina waalimu ( ambao uongozi unahakikisha wanafanya kazi yao sawasawa), kuna vitabu, maabara na wanafunzi wana shughuli moja tu, kusoma. Wana test za mara kwa mara kupima wanafunzi, kwanini wasifaulu vizuri wakipewa mitihani.

Mimi siamini kuwa Marian ina magenius, bali mazingira mazuri ya kusoma kitaasisi (walimu, vitabu, maabara, uongozi, chakula na malazi) unachangia sana wao kufanya vizuri katika masomo yao.

Kuhusu suala la makabila na dini za wanafunzi wanaochanguliwa kuingia shule hiyo, naona inachangiwa zaidi na background za hao watoto. Kuna ukweli kuwa makabila fulani wao elimu ilianza kutiliwa maanani zamani kidogo, na kwa mtazamo wangu ilikuwa kosa kuwapa upendeleo wanafunzi kutoka mikoa iliyokuwa nyumba kieimul kuingia sekondari hata kwa maksi za chini, kama uamuzi ule ulikuwa urudiwe ingekuwa kutengenza shule nzuri huko huko na kuwaandaa wanafunzi wataopata viwango vya ufaulu vinayvotakiwa kuliko kuwabeba.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom