Sababu za Marrian Girls ya Bagamoyo Kung'aa!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za Marrian Girls ya Bagamoyo Kung'aa!.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pascal Mayalla, Sep 24, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Leo ndio siku ya Interview ya kujiunga na Shule ya Sekondary ya St. Marrian Girls Sec. School iliyopo Bagamoyo.

  Interview hiyo inahusisha mtihani wa masomo matatu ya Hisabati, Kiingereza na Maarifa ambayo wataifanya kwa masaa 4 mfululizo. Imeelezwa mtihani huo ni mgumu mara 10 kumi zaidi ya mtihani wa taifa wa darasa la 7 uliofanyika wiki mbili zilizopita ili watakaofaulu ndio watakao chaguliwa kujiunga na shule hiyo.

  Jumla ya waombaji ni 3000 wakigombea nafasi 150 tuu!. Kila muombaji amelipia fomu ya kujiunga kwa Sh. 15,000/= hivyo kwa zoezi hilo la interview pekee, shule hiyo imeshajiingizia Shilingi Miilioni 45 ya chap chap!.

  Kufuatia interview hiyo, asubuhi ya leo imeanza kwa mashindano ya magari kuelekea Bagamoyo na mjini Bagamoyo penyewe ndio hapafai kabisa kwa makundi ya watu. Ziko familia zenye uwezo wamekuja na magari mawili kuanzia baba, mama, bibi, babu, mjomba, shangazi, na watoto wa familia wakimsindikiza mtoto kufanya interview as if wakiwa wengi basi mtoto wao ataongezewa maksi!.

  Magari zaidi ya 1000 kuizunguka Marrian Girls ni kizungumkuti, hivyo Traffic police wametanda kuyaongoza magari kwa kuyazuia kukaribia eneo la shule hivyo wanafunzi kulazimika kutembea nusu maili kuifikia shule. Hao traffic wakiona gari za kipesa pesa ziliruhusiwa kupita ndani kwa kihisiwa ni waheshimiwa!.

  Na tukirudi mitaani Bagamoyo leo, kila hoteli, kila mgahawa, kila kioski, kila chini ya mti kwenye kivuli ni parking za magari!. Waliokuja ki-pikiniki pikiniki, wamekuja,waliokuja ki beach beach wamekuja na mahotelini hakuna chochote watu wameshakomba kila kitu!.

  Kwa wale watoto wa familia za kula kuku sio mpaka siku ya sikukuu au soda sio mpaka wakija wageni au mayai mpaka wakiugua na matunda mpaka waambiwe na dakitari, ile kutembezwa tuu nusu maili kabla ya kuingia chumba cha mtihani ndio elimination test yao ya kwanza kwa wanafunzi wenye uwezo wa wastani kufanya mtihani wakiwa huku wakiwa wamechoka na kutembes hivyo kupata uwezekano wa kufanya vibaya!.

  Kwa idadi hiyo ya wanafunzi 3000 kugombea nafasi 150 inamaanisha watakaofaulu ndio top most cream hivyo wanakuwa ni wepesi kufundishika ukijumlisha na spoon feeding ya kutafuniwa kila kitu na wao kupewa kumeza tuu, then no wonder ni kwa nini St. Marrian Girls wanatoa Div 1 za darasa zima na kuongoza kwenye ufaulu kitaifa kipindi cha miaka kumi mfululizo!.

  Swali kwa nyie wanafunzi wa kisasa ambao mmekutana na hivi vichwa vya Marrian Girls huko mavyuoni, jee ni vichwa kiukweli mpaka huko mavyuoni?.

  Nakumbuka tukiwa UD shule zilizokuwa zikiongoza wakati huo zilileta nusu ya darasa kupiga Law. Tangu registration pale chini ya Mdigrii hadi faculty walikuwa wakipiga ung'eng'e tuu as if Kiswahili hawajui yaani hadi kucheka walikuwa wakicheka kizungu!. Hata ukimuuliza kitu kwa Kiswahili kwanza atakuuliza " what?" ili swali lako uliulize kwa Kiingereza na ukisisitiza kwa Kiswahili ndipo atajilazimisha kwa "you mean" nyingi na ma "what na what not" kibao ili mradi ni kiswanglish kwa kwenda mbele!. Sie wengine tukajisemea kimoyo moyo kumbe wenzetu wanaakili!. Kufika matokeo ya mwisho ya mwaka wa kwanza tuu, wanafunzi kumi naa wakapigwa Disco!, na wachache waliobakia nao wakalabwa disco mwaka wa pili, na sikumbuki hata ni wangapi walifanikiwa kumaliza ila tukikutana nao mitaani kwa sasa ni Kiswahili safi kwa kwenda mbele!.
  UPDATE
  Matokeo ya mtihani wa kujiunga Marrian Girls ya Bagamoyo yalitoka kesho yake Jumapili jioni kwa wazazi wa watoto wao walioshinda kujulishwa kwa simu na kesho yake Jumatatu asubuhi yalibandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa shule na kwenye ile ofisi yao iliyopo Msimbazi Center.

  Jumla ya wanafunzi 120 ndio waliochaguliwa cut off point ni wastani wa marks 35 chini ya 50.

  Nimeishuhudia marking scheme yao, mtihani wao sio tuu ulikuwa mgumu bali pia ulikuwa a bit tricky ili wanafunzi wale tuu wenye IQ above average ndio waliofaulu.

  Nimethibitisha beyond reasonable doubt kuwa mchakato wa kuipata Marrian Girls ya Bagamoyo ni mchakato wa haki wenye maximum transparency na waliochaguliwa wote walistahili, hakuna upendeleo wa aina yoyote na hakuna deals.

  Ila pia niliposoma majina ya ubini ya wengi walioshinda idadi kubwa ni majina ya watu kutoka makabila fulani fulani ambayo yanatambulika kirahisi. Lazima tukubali, tukatae, huu ni ukweli isiopingika kuwa japo Watanzania ni wamoja na hatuna ukabila, ila pia yapo makabila ambayo yamebarikiwa kwa wengi wao kuwa na akili kuliko makabila mengine.

  Pia mtihani wa kujiunga na shule hii haukubagua dini, yaani watu wa dini zote wamefanya interview ila kwenye matokeo very very unfortunately majina mengi ni ya dini fulani na sikubahatika kuyaona majina ya dini nyingine!.

  Mwalimu alipofanya affimative action ili watu wa makabila yote wapate fursa sawa za elimu, pia alitakiwa afanye vivyo hivyo kwa affimative actions ili watu wa dini wapate fursa sawa kupata elimu bora!

  Naomba Kuwakilisha.

  Pasco.
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Hzo mbwembwe 2 mkuu,mwaka huu nawajua 9 walioko vyuo mbalimbali hapa tz wamedisco.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Duhh kuna ile St. Francis ya Mbeya nayo ni balaa uzuri wa hapo hakuna rushwa wala kujuana
   
 4. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,928
  Trophy Points: 280
  hizo sio mbwembwe, hivyo ndivyo inavyotakiwa,....hata mimi shule yangu natarajia kufanya mchakato wa aina hiyohiyo....safi sana...
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ulimbukeni tu ndio unatusumbua!

  Ngoja nifanye mpango wa kuanzisha shule yangu!
   
 6. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu, enzi zetu, wanafunzi wa chuo kikuu walikuwa wanatokea shule za serikali na seminary, private walikuwa wachache sana..........nafikiri shule za private za A'level zilikuwa chache sana.

  Lakini kumbuka kwamba mazingira ya kusoma kutoka stage moja ya elimu kwenda nyingine huwa ina makeke yake. nakumbuka wapo vipanga waliokuwa wakali sana primary, lakini walipata IV na zero Form IV, wapo waliozungusha Form VI as well. na wapo waliokuwa avarage na wamepanda sana au kumentain hivyohivyo mpaka mwisho.

  Kwenye hili swala la private school kuchukua vichwa, nafikiri criteria za ufaulu ndio criteria peke zinazotumika duniani katika kuingia katika taasisi fulani ya elimu kwa maana ya kusoma. Nakubali kwamba pesa ni kigezo kingine, lakini kwa sehemu kama St. Marian na nyingine zinazofanana na hizo, issu ya kwanza ni ufaulu wa hali ya juu, then ili upate walimu wazuri, vitabu na vifaa vingine, chakula, mazingira mazuri, ni lazima kugharamikia. huwezi kukwepa hilo.

  All the best vijana.

  Mkuu, wewe umempeleka yule bint yako au ulikuwa unaenda shamba????
   
 7. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hebu dadavua DC...brigedia mstaafu!!

  wewe kwenye shule yako utafanyaje???
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hizi taarifa nimezisikia na kwa thread hii nimepata justification ... Kwamba ni kweli walikuja wakalala huko ili kuamkia interview hiyo. Kwa hilo natoa shukrani. HONESTLY kisichoingia akilini na ninaomba kusaidiwa ... What is the grand truth of the whole thing going on dwn there ... Hiyo SHOW ... Nini hasa msingi wake zaidi ya inavyoonekana ?
   
 9. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  mie nilisoma nao nairobi primary kufika secondary maisha yakaisha nkarud shule za uswahilin wenyewe wakienda hayo mashule mara fedha boys, marian na nyingine nimemaliza chuo kila niliesoma Nae primary akaenda hizo shule hajamaliza. Ni wachache sana waliomaliza. Mie nawashaur wazaz waskurupuke na hiz shule kule n luxury 2 na kuvuka form 6, lakin maisha hawawez unakuta et mtu kazaliwa dar mpaka anafika chuo hajawah fika hamjui hata jiran yake, ndo wakienda chuo wanachanyikiwa na maisha. Wanakutana na watu ambao wamesomea st. Kayumba kwao kutoroka n jad na kufaulu lazima, club ndo home, pombe ful mzuka, kenyewe unakuta hata kunywaa hakajawah Ila kwa sabab wanajifanyaga wenyewe wanajua wanaangukia pua, break ya kwanza apata boyfriend au girlfriend tapeli, Ile ndo yamekolea final hiyo, wanadharau kusoma SI wameingia chuo na 1. Wanajiona vichwa, na watoto wa uswaz kwa kupiga vibut wakat wa final ni balaa wataacha kudisco hapo.(kumbuka mtoto wa hizi shule mfano wa st. Francis hawajui kuweka mpenz wa ziada wakati wa maana)
   
 10. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  why do you guys call it a "SHOW"?
  kama wazazi wamewapeleka watoto wao kufanya interview, kwa nini inakuwa show?? kama wametokea iringa na wameona wapate wasaa wa kula maisha bagamoyo, after all wapo bagamoyo anyway, what the issue hapo??

  kna shule nyingi tu zinafanya mitihani sasa ya usaili..........mazinde juu, msolwa, n.k.
   
 11. P

  Peter lilayon Member

  #11
  Sep 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiz mbwembwe 2 final uzeeni
   
 12. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,064
  Likes Received: 3,247
  Trophy Points: 280
  Ivi inakuaje shule kama iyo inafanya mtihani swa na ule wa akina kayumba sec?
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  million 45 swaafi wakitoka hapo na mkewe ni Dubaiii hahahaha
   
 14. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #14
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kimsingi nakuunga mkono kuwa wazazi wasikurupuke.Zipo tetesi kuwa hawa watoto wanamezeshwa kila kitu na mbaya zaidi nilishawahi sikia kuwa huwa wamiliki wa hizi shule wanafanya jitihada binafsi za kuwaibia mitihani ya Taifa (NECTA).Hii ni kwa minajili ya kujenga jina la shule ili kuvutia wateja wengi kwani wao wapo kibiashara zaidi.
   
 15. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kwa hili la Mariann school Bagamoyo wanaoliwa ni wazazi kwani watoto wanaochaguliwa 150 pale tayari ni 100% cream kutoka kwa wazazi wanaojiweza tu, kumbuka kuwa pale hawaangalii kabisa kuwa huyu ni mtoto wa fisadi,CDM,CCM, Waziri au nani bali huangalia ufaulu wa mwanafunzi mhusika, hivyo mkuu bwana Pasco pale walimu hawapati mzigo mkubwa wa kufundisha kwani hata mwalimu kutoka shule za kata anaweza fundisha kidogo then wao wenyewe wakajirekebishia + tuition za wazazi wao wanapokuwa likizo mwisho wakati wa final..."A" darasa zima...Tafakari mkuu

  Ila na wewe Pasco uandishi huu umeanza lini?

  "Kwa wale watoto wa familia za kula kuku sio mpaka siku ya sikukuu au soda sio mpaka wakija wageni au mayai mpaka wakiogua na matunda mpaka waambiwe na dakitari, ile kutembezwa tuu nusu maili kabla ya kuingia chumba cha mtihani ndio elimination test ya kwanza kwa wabafunzi wenye uwezo wa wastan kufanya mtihani wakiwa tayari exhausted hivyo kufanya vibaya"

   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Huo ndiyo utamu wa shule za kikatoliki. Teacher ukibainka unapokea mlungula, unabwagwa kama ze comedy
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Jamani kiingerza kina umuhimu wake hasa kwenye baadhi ya profession, unatakiwa utoe longolongo kibaaaaaaaao na utaonekana wamo tu. Hili kenya wameligundua ndio maana wako fiti kwenye kazi za kuuza sura kama, hotel mngt, maafisa habari, walimu wa kozi za arts na religion. Hamuoni wengi wa waalimu waliopo tz toka kenya wanafanya kazi za aina hii? Tuwe makini, tutafakari na kuchukua hatua, lugha in nafasi yake.

  Teteteeeeeeeee, nimemkumbuka Msemaji wa Saddam Husein, Sghaf, cjui sakafu!!!!!!!!!
   
 18. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,064
  Likes Received: 3,247
  Trophy Points: 280
  Siku izi kuna St Islamic Seminari Sec School,, Kazi kweli kwel.
   
 19. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Hiz shule ni nzur lakin watoto wanalemaa hasa hiz za Bei kubwa kuna utofauti mkubwa na seminari za kikatorik kule mtoto anatoka yuko ful kwenye life cjui kwa sabab kuna kazi kama gerezan(hasa za mikoan) lakin huwa wakiingia chuo, wanakuwa na wknes kwa madem, seminiari zinafundisha maisha sana, nadhan kuliko shule zozote kwa Hapa tz. MI nadhan serikal inabid iige mfumo wa seminar(ukiondoa yale maswala ya kikatolik zaid) kama inataka iongeze idad ya ufaulu. Kumbuka hizi shule ni mara chache sana zinakuwa na walimu wenye hata hizo diploma, yaan wengi Wao tena hawana hata hizo pass za kuingia chuo. Je inakuwaje mtu aliye na four ya form 6, anakuwa anauwezo wa kumfundisha mtu na akapata 1? (karibia shule zote za serikali zina walimu wa ngaz ya diploma kwenda juu, lkn hazifaurish kama hiz seminar
   
 20. T

  The Priest JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sio wote kuna wengine ni vipanga kwelikweli hadi chuo...sitamsahau dada mmoja alisoma A-level Marian PCM alitukimbiza balaa hadi tunamaliza chuo..na ndie aliyeongoza mwaka huo kwa G.P.A kubwa pale udsm...my point is kuna wengine kweli ni dhaifu sana ila wengi wao wanajitahidi sana...sio wao tu mbona hata wale vipanga wa Mzumbe,Ilboru,Tabora boys n.k wakifika chuo wanapotea vibaya..ni akili ya mtu na juhudi binafsi..Chuo ni tifauti sana na secondary..
   
Loading...