Sababu za kutokuendelea kwa Jiji la Mwanza

Sababu za kutokuendelea kwa Jiji la Mwanza

Msibishane sana!Jumla ya nyumba Dar ni laki 9 huku Mwanza laki 8! Zinazoendelea kujengwa Mwanza 64,000 na Dar 53,000! Kwa hiyo Mwanza sio ya kuchukulia poa hata kidogo!
Sasa nyumba za mwanza hzo za chumba kimoja kimoja ..? Na zile za tope..?
 
Habarini wote Wana JF,

Leo nimemaliza utafiti wangu kwa nini mwanza kushindwa kuendelea na Moja ya Jiji kwenye majiji Tanzania.

Jiji la mwanza Lina idadi kubwa ya mchanganyiko wa makabila mbalimbali waliopo hapo kutoka mikoa mbalimbali.

Sababu zinazofanya kutokuendelea hizi hapa:

1. Ndoto ya wakazi mwanza Kila mtu anawaza dar es salaam. Asilimia kubwa ya wakazi wamwanza kuanzia mwenyeji, mgeni Toka mikoa inayozunguka, wafanyabiashara, wanafunzi, watumishi na n.k wote Wanawaza kutimiza ndoto zao dar.

Ni kwa nini ?
Ufinyu wa fursa na mzunguko kufanikiwa jijini mwanza unataka moyo ukilinganisha na dar es salaam ndio maana mwanza Ina walionacho na wasio nacho ukilinganisha na dar unaweza kuja unakitu na ukatoboa.

Wafanyabiashara wengi waliopo mwanza wanapofanikiwa kimaendeleo asilimia kubwa nguvu zao uzipeleka jijini dar es salaam sababu ya mzunguko wa biashara.

2. Vyuo Bora kukosena mwanza.
Ili nalo ni tatizo katika Jiji la mwanza kukosa vyuo vyenye ushawishi. Wahitimu wengi wa vyuo vilivyopo mwanza wakimaliza mazingira Yana washawishi kurudi dar wakiona Kuna kupata zaidi.

3. Jeographia ya mwanza
Katika sehemu ambazo mwanza inapata shida ni changamoto miundo mbinu kimaeneo Yani roli linakatiza mjini sababu mjini ndio njia ya kuelekea sehemu nyengine.

Maeneo ya biashara ni mafinyu ukilinganisha na dar na Ili uwafanya watu kuhisi dar ni rahisi kupata nafasi ya biashara mfano kariakoo.

4. Ushamba
Japo ni Jiji ila limejaa ushamba ndio maana ni ngumu kubuni au kuanzishwa biashara mpya mfano KFC wakati msukuma anataka samaki chukuchuku.

Pili upande wa ufugaji wa kisasa kama samaki,kuku na n.k umetengenezwa zana mbaya kwa wakazi wenyeji kuona sio chakula.

5. Uelewa
Japo ni Jiji ila Lina uelewa mdogo sana ukilinganisha na dar Ili upelekea mtu au watu uelewa wao ukiwa mkubwa anaona Bora kwenda dar.

Mwisho:
Mwanza ni sehemu nzuri kimaisha kama unapata pesa.
Ongeza na unyoko wako pia. Hiyo siyo tafiti ni fikira zako wewe za kizwazwa zimekutuma kuandika huu upuuzi. Wasukuma wangapi wanaishi dar es salaam vs makabila mengine?.
 
Kwenye ushamba hapo umezingua ila chakula wanapenda cha asili hata kwenye sherehe wanakula kuku wa kienyeji,ukifuga broilers kanda ya ziwa utakula wewe na familia yako. [emoji28]
Mi hadi leo broiler naila kwa machale hadi kuwe labda kwenye Sherehe au event isiyo na alternative food
 
Kula samaki chukuchuku ni ushamba

Kula hayo mavyakula ya kisasa na ma broilers ndo ujanja
Yaya ghete
[emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Angalizo tu hilo vyakula viwe na diversity na variations sio kila mtu anakula chukuchuku mkuu
 
Sio mwanza tu wabongo kwa ujumla ni closed minds hawapendi vitu vipya.yaani hawapendi vitu mbali na vile waliovizoea

Ndyo maana hata ukienda kwenye migahawa sehemu mbali mbali hapa Tanzania menu huwa ni zile zile karibia migahwa yote.
 
Hakuna Jiji linaloendelea kwa haraka Afrika Mashariki kama Mwanza. Utafiti wako una kasoro kubwa.
Kuna maeneo amesema ukweli. Watu wa mwanza walio wengi ndoto zao huwa ni dar yaani kila mtu stori huwa ni dar tu hawauamini mkoa wao.
 
kwa ufahamu wangu katika mikoa yote niliyopita kwa majukumu yangu mwanza pekee ndiyo mkoa sikuona ugeni na utofauti mkubwa kiuchumi na dar,
Na ukarimu wa watu wa mwanza nawaza kabisa kwenda kuishi hapo.
Mi nimeishi mwanza miaka 5 na niseme ukweli ni sehemu yangu pendwa kuliko sehemu yoyote Tanzania na nina mipango ya kurudi ingawa nilikula za uso kwenye biashara.
 
Kweli Mwanza miundbinu ni shida, hasa barabara. Ila Dar shida kubwa uchafu - nenda soko la Buguruni huone. Mafuriko na usafiri. Bora kuishi Mwanza
 
Listen up yoh, listen up yoh !
Sijajua ni Mwanza ipi inayozungumziwa hapa ila kama ndio ile ya kanda ya nyonyo shida ni miundombinu tu, kwenye miundombinu hata kwa Dodoma haingii

Ila vingne vyotee tumepgwa, pigwaa kbsaa, I have been in Mwanza twice within this year, the city is a little bit beautiful jus headed by Dar es Salaam nationally!!

Kuhusu ushamba mm huwa sjui ndio uko vp huwa naona watu wa huko ni kama waliopo tu hapa Dom, Dar etc
 
Listen up yoh, listen up yoh !
Sijajua ni Mwanza ipi inayozungumziwa hapa ila kama ndio ile ya kanda ya nyonyo shida ni miundombinu tu, kwenye miundombinu hata kwa Dodoma haingii

Ila vingne vyotee tumepgwa, pigwaa kbsaa, I have been in Mwanza twice within this year, the city is a little bit beautiful jus headed by Dar es Salaam nationally!!

Kuhusu ushamba mm huwa sjui ndio uko vp huwa naona watu wa huko ni kama waliopo tu hapa Dom, Dar etc
Wenzako huwajui mtu akiwa Msukuma tu au eneo lolote wakiwa majority ni Wasukuma wanasema washamba!
Ndo silaha yao ya kuwapigia hata ukitaja Katoro au Kahama kuwa ina biashara watakwambia pa kishamba!
Watu wengi hawapendi maendeleo ya Mwanza na kanda ya ziwa wao huwa wanaamini jamii za huko hasa wasukuma wanaishi maisha duni sana ila wakifika wanaona tofauti!
 
Back
Top Bottom