dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,124
- 49,384
Wadau;
Hivi umewahi kujiuliza ni kwanini vyoo vya umma hutenganishwa vya wanaume na wanawake? Kwanini iwe hivyo? Mbona majumbani tuna-share toilets na hamna tatizo? Hii kitu ilikuwepo tangu mwanzo? Kama sio tangu mwanzo lilianza lini na wapi?
Kimsingi, sio zamani sana, hakukuwa na kutenganisha vyoo vya kike na kiume. Walikuwa wana-share. Desturi ya kutenganisha ilianza miaka ya 1700 huko Paris - Ufaransa ambapo baadaye ilienea katika mataifa mengine. Kwa mfano, Marekani kwenye miaka ya 1800 ndipo ilipopitisha utaratibu wa kutenganisha vyoo vya kike na kiume.
Baada ya mapinduzi ya viwanda, mfumo wa maisha ulibadilika ambapo uzalishaji ulibadilika kutoka wa majumbani na kwenda wa viwandani ambapo watu wengi walikusanyika kwa pamoja hivyo kupelekea hitaji la vyoo kwa jinsi tofauti.
Ila jamaa walikosea sana aiseeee! Maana hata dini hazijazungmzia kutenganisha vyoo badala yake ni mawazo tu ya kibinadamu.