Uchaguzi 2020 Sababu ya Vyama vya Upinzani kutomuunga mkono Lissu, CHADEMA walivunja makubaliano ya kugawana Ruzuku kuvipa Vyama vyote vya UKAWA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,906
2015 kuliundwa UKAWA na vyama vilivyounda UKAWA vikakubali kutoweka mgombea Uraisi vimuunge mkono mgombea mmoja tu wa CHADEMA, Lowasa na CUF ilimtoa Duni Haji ajiunge CHADEMA kama mgombea mwenza kumpa nguvu zaidi ya kura Lowassa za Zanzibar na za waislamu.

Vyote vikakubaliana kuwa kwa kuwa kupata ruzuku inategemea kura nyingi za Uraisi wote wakubaliana wapambane kuhakikisha Lowassa anapata kura nyingi zitazofanya CHADEMA ipate ruzuku kubwa Sana Kisha baada ya ushindi CHADEMA kikipata Ruzuku kiwagiwie vyama vingine vilivyo sacrifice kutoweka wagombea Uraisi

Matokeo baada ya Chadema kuanza kupata ruzuku wakagoma kugawia wenzao ikiwemo hata CUF iliyowapa Duni Haji ndio.maana Duni Haji Aliondoka Chadema kwa hasira baada ya kuona Makubaliono yamevunjwa na CHADEMA

Sasa mwaka huu Chadema walipoanza kuviomba vyama vingine vimuunge mkono Lissu vikagoma kuwa mnataka tuwasaidie mpate kura nyingi za kuwawezesha kupata ruzuku hakafu mle peke yenu Kama mlivyotutapeli 2015 hatutaki Kila mtu apambane kivyake na mgombea Uraisi wake.

Ndio sababu kuu ya vyama kugoma. CHADEMA imekuwa ikipita kupiga magoti kuomba isamehewe vyama vingine vimegoma kuwa sio kosa kufanya kosa Mara moja Sio kurudia kosa. Vimegoma.

Utapeli wa CHADEMA safari hii umekwaa kisiki.
 
Lissu anawalaza macho kuanzia mwenyekiti wenu.
Mwambieni kuungwa mkono Safari hii kumegoma kura za kufikia ruzuku hazifikiki Safari hii

Anatafuta asikimie 20 ya kura chama kipate ruzuku lakini Ni ndoto 2015 iliwezekana sababu ya UKAWA Chadema waliowatapeli pesa zao
 
Mmelitumia Bunge vibaya kwa kupitisha Sheria kandamizi zinazotumiwa na Tume ili kuvibana Vyama vitakavyo taka kuungana ,ni kama mliamua kumuua Mende kwa kutumia Nyundo.Janja yenu imejulikana mmebaki na kusema Uongo tu humu kinyume na Hali halisi.
 
Lissu anawalaza macho kuanzia mwenyekiti wenu.
Bado kidogo wavae boxer kichwani😁😁!
Yaani moja haikai wala mbili haikai!Wamebaki kama kuku aliyekatwa kichwa!Sasa hivi kila wanalookota basi wanakimbia nalo JF kuanzisha uzi,Lissu akiendelea kubana spana mpaka kampeni ziishe kuna watu watakuwa ICU kama sio milembe!
 
Bado kidogo wavae boxer kichwani😁😁!
Yaani moja haikai wala mbili haikai!Wamebaki kama kuku aliyekatwa kichwa!Sasa hivi kila wanalookota basi wanakimbia nalo JF kuanzisha uzi,Lissu akiendelea kubana spana mpaka kampeni ziishe kuna watu watakuwa ICU kama sio milembe!
Lissu ndiyo habari ya mjini, kwenye daladala, maofisini, sokoni, bar, hospitali, majumbani kila mtu anasikiliza hotuba za Lissu you tube.
 
Kila uzi utaandika lakini bado ngoma ngumu.
Kwenye hili ngoma ni ngumu kwa Lisu na chadema sio Mimi Lisu sasa hivi hapiganii hasa uraisi anajua hatashinda anapigana zipatikane kura asilimia 20 za kura zote ili chama ki qualify kupata ruzuku

Chadema pesa za ruzuku walikuwa hawapeleki mikoani na wilayani baada ya kuwa wamezisotea zote wakawa wanazila makao mkuu

Malalamiko yako kibao niwashauri Chadema mikoani ukimpa kura Lisu unaipa ruzuku Chadema ambayo ikipatikana wanaila wenyewe makao mkuu

Kuwaadhibu wasipate ruzuku msimpe kura mgombea uraisi Lisu wapeni kura wabunge na madiwani huyo msaka ruzuku ya Chadema msimpe kura sababu ruzuku ikipatikana haiendi chini mikoani na wilayani n.a. nyie mumetapeliwa kama UKAWA mkataeni Lisu walimu kura wabunge wenu na madiwani
 
Hivi Rungwa, Shibuda, Muta nk, ushiriki wao wa kuwania Urais, una athari yoyote kwa Lissu?
Au Lipumba ana athari gani?
Wapiga kura wao wana athari kwa mgombea uraisi wa Chadema kupunguza kura za kuwawezesha Chadema ku qualify kupata ruzuku
 
Lissu peke yake anawatesa hivi mpaka mwenyekiti wenu anapatwa na vipandauso.
 
Uzushi tuu kwann hoja ije wakati huu, wewe ni nani katika ukawa? ok tusrme ni kweli ni chama gani cha kuungana cdm ? ACT, CUF au CHAUMA ? wana nin cha kuunganisha? kwa ufupi wote hao wanaitaka cdm iwabebe na baada ya hapo wanaunga juhudi.
 
Huu uchaguzi uko pande mbili kwa Chadema

Chadema makao makuu wanatafuta ruzuku mgombea wao wa kuwawezesha ruzuku kupatikana ni Tundu Lisu ndio maana anatumia pesa za makao makuu kuendesha kampeni akikodiwa ndege helikopta nk

Majimboni wagombea ni wabunge na madiwani hao ni kama wagombea binafsi pesa ya ruzuku ya makao makuu ya Chadema haiendi kwao kuwasaidia kukodi hata baiskeli sababu wao sio wagombea wa kusaka ruzuku wa makao makuu
 
Mwambieni kuungwa mkono Safari hii kumegoma kura za kufikia ruzuku hazifikiki Safari hii

Anatafuta asikimie 20 ya kura chama kipate ruzuku lakini Ni ndoto 2015 iliwezekana sababu ya UKAWA Chadema waliowatapeli pesa zao

Katika vitu vilivyotukwaza wanacdm wengi ni huo muungano wa vyama. 2015 cdm ilikuwa inajimudu bila muungano na chama chochote. Hata kujiunga walijiunga kama fashion tu na haikuwa lazima sana.

Na kitendo cha kutokuungana hivi sasa, na ile mijizee miwili ya ccm Lowassa na Sumaye kurudi huko huko chama chakavu kumetupa faraja sana. Kwa mfano sasa hivi cdm wangekosea kisha wajiunge na Membe ingetukera vibaya sana.

Hivyo vyama vilivyojiunga na ccm ni bora viendeleze muungano wao na ccm, maana vitapewa chochote. Cdm haihitaji kujiunga na mchepuko wowote wa ccm, maana ina mtaji wa kutosha wa watu.
 
Back
Top Bottom