Sababu ya UKAWA kuwa vibaraka wa wazungu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
UKAWA kila kukitokea tatizo wamekuwa wakikimbilia kuwaomba wazungu wasitishe misaada nk nikatafiti nikajua ni kwa nini UKAWA wako hivyo nikagundua yafuatayo.

Nilipotazama UKAWA nikagundua kuwa UKAWA wana nguvu zaidi mikoa ya kaskazini na Zanzibar ambayo yote inategemea wazungu.Sehemu ambazo ni tegemezi kwa wazungu kwa asilimia kubwa kwa uchumi wao ni hayo maeneo.

Mikoa ya kilimanjaro ,Arusha na Zanzibar tegemeo lao ni utalii.Na watalii wengi ni wazungu ambao hutembelea Zanzibar ,Mlima kilimanjaro na Mbuga zilizoko Arusha.Kwa hiyo wazungu kwa akina Mbowe,Lowasa,Mbatia,na akina Seif SHARRIF Hamad wanawaona kama miungu kwao wa kuwaabudu maana kutwa ndio wateja wao wa kuwaletea pesa.Kwa hiyo kitu kidogo utasikia tumewaandikia mabalozi wa jumuiya ya ULAYA kuhusu hili swala na tumemwambia mzungu Bill GATES wa MCC asimamishe misaada!!!!!!

Ndio maana usione SEIF Sharrif Hamad akimwona mzungu awe balozi wa Norway au wapi anajisikia hata kumwabudu kwani wazungu ndio watalii wakubwa wa mji mkongwe na wakaa hoteli za mji mkongwe ambazo waswahili huwa hawakai.

Mwingiliano mkubwa na wazungu watalii umewafanya kuwa vibaraka
 
Wazungu wamewapa sana Fedha Ukawa za kuing'oa CCM tatizo jamaa Mafisadi pesa wanaenda kujengea mahekalu Dubai.
Mwisho wazungu Wamehemewa wamemuomba Jk asaidie kupumzisha CCM na hilo kabainisha Robert Mugabe kwny hadhara kuu ya umoja wa Mataifa hivi karibuni.
 
we mwenyewe siku nzima umeishi kwa hisani ya watu wamarekani

Marekani kuna wamarekani weusi mimi nimeongelea wazungu.
Ona Lowassa wa UKAWA anavyopenda Wazungu hata ndege aliyokuwa akitumia wakati wa kampeni ilikuwa ikiendeshwa na wazungu.Wazungu ndio walimbeba Lowasa

upload_2016-2-17_9-44-14.jpeg
 
Kwa walioajiriwa watanielewa; ukiwa umeajiriwa kampuni na IDARA moja na watu wenye majungu ya uongo kama wewe, ukweli hua ni SHIDAAA! Unaandika vitu vinavyo onekana kama ni vya kweli kwa wazembe wa kufikiri tena mbele za watu wanaoitwa great thinkers!
 
?JE, Wale WAZUNGU Wanaoendelea Kwenda SELOUS, MIKUMI, KITURO, GOMBE, MAHALE AMBONI, SAADANI N.k. Wanaabudiwa Na CCM!!!!!!!????? KWELI CHOKO, HAACHI UCHOKO, HATA AKIWA MZEE!!!!

Huko ulikotaja Utalii ni sehemu ndogo mno ya tegemeo lao la uchumi.Wana njia zao zingine kubwa za kiuchumi hawategemei watalii wazungu .Zanzibar na kaskazini pato lao kubwa la kodi,ajira nk linategemea zaidi utalii.Sehemu ulizotaja wazungu wala hawajaathiri akili zao kama huko kaskazini na Zanzibar waliko UKAWA.
 
Ukibaraka ni nini? Kuna mtu alileta mada humu akasema UKAWA inaungwa mkono na vyama vya siasa vinavyounga mkono Ushoga huko Ulaya na Marekani. Nilipomuuliza imekuwaje Serikali chini ya CCM imeruhusu Ushoga Tanzania, mpaka leo hajajibu!! Huyu naye ambaye yumo kwenye "List of 46" anakuja na hoja ya namna hii.

Na kwa kweli CCM ubaguzi umo kwenye mishipa ya damu zao na fahamu zao. YEHODAYA anadai marekani wako waamerika weusi na wazungu kwa lengo la kuonesha eti misaada inayoletwa Tanzania inatokana na mchango wa Waamerika weusi na si wazungu. Nyie CCM ni MAKABURU!!
 
Sasa shida iko wapi ?

Kwa taarifa yako kila muafrica anamtegemea mzungu.

Tangu ukoloni . Walioanzisha miundo mbinu ni wao. Hata ukatae vipi na wewe unamtegemea mzungu . Hiyo simu au lap top unayotumia kuwa sema hapa ni wao walibuni.

Acha papara.
 
anadai marekani wako waamerika weusi na wazungu kwa lengo la kuonesha eti misaada inayoletwa Tanzania inatokana na mchango wa Waamerika weusi na si wazungu. Nyie CCM ni MAKABURU!!

PRESIDENT OBAMA IS A BLACK MAN WHO LIKES TO HELP BLACK MEN IN AFRICA. TANZANIA IKIWEMO
 
Unaandika vitu vinavyo onekana kama ni vya kweli kwa wazembe wa kufikiri tena mbele za watu wanaoitwa great thinkers!

Tatizo wewe Mwana UKAWA hata siri ya kuanzishwa UKAWA hujiui ngoja nikupe.

Wengi wanajiuliza hivi wazo la kuanzisha UKAWA lilitokea wapi?

Nianze historia kidogo.Wayahudi walikuwa ni watu wasiopenda siasa kabisa.Walijikita tu kwenye biashara.Walikuwa ni wafanyabiashara wakubwa mno nchi za Ulaya hasa ujerumani.Hitler mwanasiasa katili alipoibuka na kuwaua zaidi ya milioni 60 wakaamua kujitosa kwenye siasa wao na wakawa ndio waasisi wa mfumo ambao unasema anayemiliki njia kuu za uchumi ndiye anatakiwa ashike dola (utawala wa wachache wenye pesa kutawala walio wengi wasio na pesa)

Tanzania kuna makabila mawili makubwa ya wafanyabiashara.Makabila hayo ni ya Wachaga na wapemba.Na hawa ndio makabila ambayo sehemu kubwa za biashara za wazawa zimeshikwa na wao katika nchi.Na wengi wao mfano wachaga chama chao ni CHADEMA na Wapemba chama chao ni CUF.

Kwa hiyo viongozi wakubwa wa vyama hivyo walikaa wenyewe kwa siri wakaona sasa ni wakati muafaka wa nchi kushikwa na wafanyabiashara walioshika njia kuu za uchumi ili washike vyote uchumi na utawala.Ndio wakaamua kuanzisha UKAWA.Waliupa jina la UKAWA kuzuga kujificha mbele ya macho ya watanzania wasione nia ovu iliyokuwa nyuma ya mpango wao.Tuvyama twingine twa akina Mbatia na makaidi tuliingizwa tu kama bendera fuata upepo maana tulikubaliana mwishoni kwa kupewa tusenti twa kujikimu.

Baada ya kuuanzisha UKAWA wakaona watafute mfanyabiashara mkubwa LOWASA agombee uraisi lakini uamuzi huo ulikuwa wa siri watu wasio wafanyabiashara walio vyumba vya ndani (inner circle) kama Lipumba na Dr.SLAA hawakushirikishwa kwenye vikao vya siri mwanzoni wakaja tu kusitukizwa matajiri wafanyabiashara wa kichaga na kipemba walishamaliza yote kuwa mgombea ni LOWASA asiyetaka aondoke.Slaa na lipumba ambao hawana hata mradi wa kuuza nyanya chungu ikabidi watupwe nje ya mfumo wa matajiri wa UKAWA .

UKAWA wangefanikiwa nchi ingekuwa chini ya wafanyabiashara matajiri wanaojiamulia walipe kodi au wasilipe na hakuna jipu hata moja lingetumbuliwa na wasio kuwa nacho wangekiona cha mtema kuni.Na hiki chama walitaka washinde ili wawe wanaongea lugha moja na matajiri wezi wa kizungu.Nchi ingeuzwa hadi nyayo za watu kwa wazungu.

Mungu MKUBWA kaepusha nchi na UKAWA.

UKAWA ilianzishwa kwa ajili ya matajiri na mabwanyenye wa kichaga na kipemba wengine akina yahe mnafuata mkumbo tu na kutumiwa tu.
 
Kwani matajiri kuwa wanasiasa ni tatizo? Hivi kipi ni kizuri, Mwanasiasa kujitajirisha kwa kupitia siasa au tajiri kuwa mwanasiasa? Nyie "List of 46" bure Kabisa!!
 
Kiufupi mleta mada ameathirika kwa mazoea ya kujitoa ufahamu,sasa anaona ni hali ya kawaida!
 
ile ni saccos, ili vyanzo vya mapato viongezeke lazima nyumbu waongezeke, na ili nyumbu waongezeke lazima maigizo yafanyike, kama ulivyoona wakati wa uchaguzi ulifanyika usajili murua kabisa ili kuongeza nyumbu, kwa kiasi flani ni biashara na pato la saccos lazima likue.
 
umesa
UKAWA kila kukitokea tatizo wamekuwa wakikimbilia kuwaomba wazungu wasitishe misaada nk nikatafiti nikajua ni kwa nini UKAWA wako hivyo nikagundua yafuatayo.

Nilipotazama UKAWA nikagundua kuwa UKAWA wana nguvu zaidi mikoa ya kaskazini na Zanzibar ambayo yote inategemea wazungu.Sehemu ambazo ni tegemezi kwa wazungu kwa asilimia kubwa kwa uchumi wao ni hayo maeneo.

Mikoa ya kilimanjaro ,Arusha na Zanzibar tegemeo lao ni utalii.Na watalii wengi ni wazungu ambao hutembelea Zanzibar ,Mlima kilimanjaro na Mbuga zilizoko Arusha.Kwa hiyo wazungu kwa akina Mbowe,Lowasa,Mbatia,na akina Seif SHARRIF Hamad wanawaona kama miungu kwao wa kuwaabudu maana kutwa ndio wateja wao wa kuwaletea pesa.Kwa hiyo kitu kidogo utasikia tumewaandikia mabalozi wa jumuiya ya ULAYA kuhusu hili swala na tumemwambia mzungu Bill GATES wa MCC asimamishe misaada!!!!!!

Ndio maana usione SEIF Sharrif Hamad akimwona mzungu awe balozi wa Norway au wapi anajisikia hata kumwabudu kwani wazungu ndio watalii wakubwa wa mji mkongwe na wakaa hoteli za mji mkongwe ambazo waswahili huwa hawakai.

Mwingiliano mkubwa na wazungu watalii umewafanya kuwa vibaraka
umesahau kila siku kutishia watapeleka watu icc. mara zec icc kwa kufuta uchaguzi. lissu mwanasheria anajua kesi gani zinapelekwa icc lakini wameishiwa wanafanya mzaha. mwisho watataka speaker icc kwa kukataa mwongozo.
 
Wazungu wamewapa sana Fedha Ukawa za kuing'oa CCM tatizo jamaa Mafisadi pesa wanaenda kujengea mahekalu Dubai.
Mwisho wazungu Wamehemewa wamemuomba Jk asaidie kupumzisha CCM na hilo kabainisha Robert Mugabe kwny hadhara kuu ya umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Hahaha chezea DJ wewe
 
UKIWA hawatokuja kufanikiwa na hawa viongozi wao VILAZA
Siasa za kuto kukoselewa
Siasa za UMUNGU MTU
Siasa za UNYUMBU
Siasa za MATUKIO
Ngoja La Zanzibar liishe
Waanze kuuza sura hovyo hakuna hoja tena
Zaidi ya Zanzibar
 
Kwani matajiri kuwa wanasiasa ni tatizo? Hivi kipi ni kizuri, Mwanasiasa kujitajirisha kwa kupitia siasa au tajiri kuwa mwanasiasa? Nyie "List of 46" bure Kabisa!!
Unatetea lisilo tetewa
Tuliwai kuwa ambia Lowassa hasafishiki mkabisha
sasa mliangukia pua
leo mmsalia na ajenda moja ya Zanzibar kama Taa ya Treni
 
Hapa pia unaonekana kukiri kuwa zanzibar ni ukawa kama ilivyo kilimanjaro na Arusha,kwa maana nyingine unakiri kuwa ccm ilipigwa chini zanzibar kama ilivyoangushwa kilimanjaro na Arusha!Wanaccm mnatambua kuwa ccm ilishindwa zanzibar,ndio maana mnasema zanzibar ni ukawa kama mleta mada anavyokiri!

Nimeandika UKAWA wana nguvu sijaandika kuwa wao ndio wenye hayo maeneo.Zanzibar CHADEMA na NCCR haina nguvu kabisa haina hata diwani mmoja.Nikisema UKAWA ina nguvu haina maana CHADEMA ina nguvu wala NCCR ina nguvu
Huwezi sema CUF walishinda au CCM ilishinda wakati matokeo hayakutangazwa na tume !!!!!!!!
 
Matumizi sahihi ya viungo yanahitajika hapa. Makalio kazi yake si kufikiria... Tutumie kiungo kingine.
 
Back
Top Bottom