Azam yathibitisha kupokea ofa kutoka vilabu viwili vikimuhitaji Dube, Simba sc ikiwemo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
IMG_20240314_201106_442.jpg

Azam FC inathibitisha kwamba imepokea ofa kutoka vilabu viwili tofauti vikimhitaji mchezaji wetu, Prince Dube, raia wa Zimbabwe.

Ofa hizo zimetoka katika vilabu vya Simba SC ya Tanzania na Al Hilal SC ya Sudan.

Uongozi unazifanyia tathmini ofa hizo ili kuona ipi inafaa.

Aidha, Azam FC inavikaribisha vilabu vingine kuleta ofa zao kwani milango bado iko wazi.

Imetolewa na Menejimenti,
Azam Football Club,
Machi 14, 2024.

Pia soma: Klabu ya Azam FC imethibitisha kupokea barua kutoka kwa mshambuliaji Prince Dube akiomba kuvunja mkataba
 
Binafsi sidhani kama Simba ihangaike na Dube. Huyu uchezaji wake hana tofauti na Mbangula ambaye wanaweza kumpata kwa bei chee zaidi. Jobe ana nafasi ya kuisaidia Simba zaidi mbele ya safari kama ataongeza nguvu na kucheza kwa akili zaidi.

Simba inahitaji kusaka na kutengeneza striker mashine moja ya magoli, bwa mdogo wa miaka kama 20 hivi umri sahihi, mrefu wa kimo aliye mzawa watakayemkuza kwa malengo ya muda mrefu.
 
Tanzania mchezaji kama huyo kazi sana kuwepo kwani mashabiki sio wavumilivu kumwacha dogo ajifunze kwa kupatia na kukosea,,,mashabiki wabongo na wachambuzi wamejengeka kwa matokeo Chanya tuu kwa wachezaji wao
 
Wamtafute hata ligi daraja la pili huko na wamsajili bila mbwembwe wala kelele ili kusiwe na pressure. Wakishampoint ni kumjenga tu taratibu katika misingi sahihi, kimwili, kiakili na kimbinu.

Nilichogundua kuna uhaba wa washambuliaji wazuri ndani ya Afrika ambao tayari wanacheza level za ligi kuu. Angalia takwimu za mashindano ya CAF, hauoni mtu anayesumbua miaka 2-3 mfululizo. Na hili tatizo limekuja kwa sababu wajanja wamekuwa nawabeba wachezaji wengi wazuri wangali wadogo sana, wengi kabla hawajacheza hata CL au CC sembuse ligi zao kuu za ndani, wanakuja kuibukia nje huko. Angalia yule dogo wa ASEC, baada ya kuonyesha potential kauzwa nje kabla hata hatua ya makundi haijaisha.
 
Kiyombo,Salamba,Mzize ,KiBu D Ngushi hawa ni mifano tuu ambao tulikua tunawazomea na kuwaua kisaikolojia badala yakuwasapoti na kuwapa Moyo wapandishe soksi waendelee kupambana! !!!
 
Ni kweli ila hizo klabu zao zilikuwa zina program special za kuwakuza na kuwaendeleza ili wafikie level wanayoweza kufikia?

Kibu inaonyesha kama Robertinho ndiyo alimuokoa. Kyombo inaonyesha alishakata tamaa au aliridhika, hakuonyesha muendelezo wa upambanaji. Haitakiwi kuwa mapenzi binafsi ya kocha au kiongozi bali maono ya klabu kwa mchezaji husika.
 
Back
Top Bottom