Klabu ya Azam FC imethibitisha kupokea barua kutoka kwa mshambuliaji Prince Dube akiomba kuvunja mkataba

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,732
Klabu ya Azam FC imethibitisha kupokea barua kutoka kwa mshambuliaji Prince Dube akiomba kuvunja mkataba wa kuwatumikia Waoka Mikate hao ambao amewatumikia tangu mwaka 2020.

Mkataba wa nyota huyo raia wa Zimbabwe aliosaini mwaka 2023 utamuweka klabuni hapo mpaka 2026. Hivyo sasa amebakisha miaka miwili na nusu mkataba wake kufikia ukomo.

Azam FC imemjibu Dube (27) kwamba kama anataka kuondoka kama ambavyo amewasilisha ombi lake, klabu haina kipingamizi chochote na imemruhusu kuondoka lakini matakwa ya mkataba yanatakiwa kutekelezwa.

Maoni Yangu: Huyu dogo ni bonge la chezaji kwa hivi Sasa ubora alionao timu za Kariakoo zinamfaa huyu sema majeruhi yanamsumbua.

1709572489937.jpg
 
Anatakiwa alipe kiasi gani..?
Za ndaaniii kabsa Azam FC wanataka 765M ili wamwachie Dube. Lakini najua watamwachia kwa pesa chini ya hiyo maana Azam hawana tabia ya kung'ang'ania wachezaji na hawapendi makelele na migogoro, zaidi ya yote hawana njaa.

Sioni timu gani ya Kariakoo itaweza/itakubali kutoa hiyo pesa kwa Dube ambae mimi namuona sio mchezaji wa kutegemea sana kutokana na rekodi yake mbaya ya injuries za mara kwa mara. Lakini pia sio mchezaji wa daraja la juu na wa kutisha sana. Kama Azam itamwachia Dube halafu imsajili Mayele basi watakuwa wamenufaika zaidi kuliko watakaomchukua Dube
 
Za ndaaniii kabsa Azam FC wanataka 765M ili wamwachie Dube. Lakini najua watamwachia kwa pesa chini ya hiyo maana Azam hawana tabia ya kung'ang'ania wachezaji na hawapendi makelele na migogoro, zaidi ya yote hawana njaa. Sioni timu gani ya Kariakoo itaweza/itakubali kutoa hiyo pesa kwa Dube ambae mimi namuona sio mchezaji wa kutegemea sana kutokana na rekodi yake mbaya ya injuries za mara kwa mara. Lakini pia sio mchezaji wa daraja la juu na wa kutisha sana. Kama Azam itamwachia Dube halafu imsajili Mayele basi watakua wamenufaika zaidi kuliko watakaomchukua Dube
Mzee Mayele stats zinaonyesha hata akiwa Yanga hakuwa striker tishio kiasi hicho hapa Tanzania. Dube is a monster bhn. Mayele ni kuimbwa tu aliimbwa sana ila hamna kitu pale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom