Sababu mbili kwanini bado upo single

Radium

JF-Expert Member
Aug 5, 2022
478
847
Kwa akili timamu tatizo la usingle kwa muda mrefu, hupeleka lawama nje na kulifanya tatizo katika mfumo wa mechanics. Nipo single kwa sababu pamoja na kuishi mjini na sehemu yenye watu wengi, sijaalikwa kwenda sehemu zenye mikusanyiko muda wa free.

Au jukumu la kikazi linalonifanya nisafiri mikoani kila mara linanifanya nikose muda wa kusocialize. Au kwa sababu nipo huku kijijini ndani kabisa milimani ambapo kuna basi moja tu la kunifikisha mjini nalo si la uhakika, sio rahisi kwangu kukutana na mtu sahihi. Hizi zinaweza kuwa sababu imara kabisa LAKINI tatizo hili la usingle linapokuwepo kwa muda mrefu uwezo wetu wakujitetea unadhoofika.

Sasa hapa ndipo inabidi mtu utoke kwenye kulitazama tatizo lako katika mechanical na kulipeleka katika psychological perspective. Tatizo lipo katika akili zetu na sio kwa watu wengine. Na katika ubongo huu wa mtu aliyeko single kwa muda mrefu, issue mbili tofauti ila zanazoendana ni lazima zitagundulika.

1. Yupo single kwa sababu anajichukia sana(Self Hatred)
2. Yupo single kwa sababu anajipenda kupitiliza(Excessive Self Love)

1. SELF HATRED.

Hii ya kujichukia ndiyo case kubwa zaidi kwa jamii ya sasa.
Pamoja na kufuatwa na kuchombezwa na mtu wa jinsia nyingine(Hii ni haswa kwa wanawake) au pamoja na kumtongoza na kuona nafasi ya kuwa na mahusiano(Hii kwa wanaume), ijapokuwa ana mvuto na kama nilivyosema tunaona kabisa nafasi ya mahusiano, tunaanza kujiuliza tena kwa mshangao tukijaa maswali kichwani
" Kwanini awe waajabu, mjinga, mdhaifu, na kipofu mpaka hata ampende mtu kama MIMI"

Tunapokuwa na mashaka na kupendeka kwetu tu, attention ya mtu mwingine kwetu huwa tunaiona ya kukera na tunathubutu kuwaita ving'ang'anizi na hata anapopiga simu tunjisikia kukereka tukijiaminisha kuwa hatuwapendi, kumbe tusiyempenda ni sisi na tunaamini hatustahili upendo wa mtu kama huyo. Hivyo tunawaona wajinga wasio na machaguo mengine.

Mapenzi yanageuka kuwa kama zawadi ambayo bado hatujaishinda, na haitustahili, kwahiyo tunakuwa makini na hatimaye tunaitupia mbali.

Inaweza kuonekana maajabu lakini ni wanaume wengi waliweza kufuatwa au kutongozwa na wanawake wazuri na wanaojiheshimu lakini waliwakataa na kubaki kujiuliza ni kwa nini hawavutiwi na wanawake hao.

Na ni wanawake wengi wametongozwa mara 100 na wanaume wanaowaota na kuwa fantasize kila mara lakini wakawakataa.

Hii ndiyo "MENTAL ILLNESS" iitafunayo jamii yetu.

Kwahiyo kwakuwa hakuna mtu anayetujua kiundani kuliko sisi wenyewe, tunachokifanya ni kuwakimbia mapema sana hawa wanaotupenda kabla hawajatukimbia watakapo gungua undani wetu.
Pamoja na matamanio yetu na mapenzi yetu tunaona hakuna sababu nzuri na zakudumu za kumfanya mtu mwingine atupende.

Anapotuma jumbe, anapotununulia zawadi au anapotukumbatia tunakuwa na hisia fulani ya hasira isiyoelezeka kwa sababu tunaona ni king'ang'anizi kwa kiwango cha juu na wanatutaka kupitiliza. Ila yote ni kwasababu tunaona hatufai kuhitajika kwa namna yoyote. Tunaukataa upendo unaotegemea kwetu kwa sababu tunajua ndani kabisa ya mifupa yetu, sisi si wakutegemea.

Mtu anayetupenda sio kwamba ni mpuuzi asiyeweza kuchagua, bila shaka yoyote wanatuona kwa jinsi tulivyo na wanajua kabisa ni katika point zipi tunatatiza na tunakera, lakini wanajua kuwa kila mtu yupo hivyo haijalishi anamuonekano gani. Wanajua kuwa hakuna aliyeko sawa na hilo sio kikwazo cha kuwa na mahusiano ya kiutu uzima.

Mbele yetu wanajua kabisa mtu anaweza kuwa si mkamilifu na bado akawa na haki ya kupewa mapenzi yasiyo na mipaka.

2.EXCESSIVE SELF LOVE.

KISHA katika upande mwingine wa spectrum ndipo inakuja wale wanaojipenda kupitiliza.

Hapa sasa mtu anasita au wala hajaribu kujiuliza na kutambua kuwa Je Ni kwa namna gani yeye ni kikwazo kiasi gani na ni kwa kiasi gani yeye sio mkamilifu.

Na kwasababu hiyo hafikirii ni kwa namna gani anapaswa ashukuru pale ambapo mtu mwingine yeyote yule anaangalia upande wetu ,specifically kwa kuvutiwa na sisi.

Tunaoperate kwa mawazo yaliyokosa msaada wa kuona ni jinsi gani mtu atakuwa mwenye bahati kuishia mikononi mwetu. Baada ya kuwa pekeyetu kwa muda mrefu kuna uwezekano mkubwa wa part ya emotions kwenye ubongo kukosa nguvu hivyo tunashimdwa kuona jinsi tulivyo wadhaifu na wenye uhitaji wa kuwa na mtu.

Bila kuwa na mtu wa kutushikia kioo, tumesahau kutua uzito majuto, malalamiko, wasiwasi, na nyakati za taabu tulizoficha ndani yetu. Kwa wakati huohuo tunasafiri dunia huku tumezima IMAGINATION.

IMAGINATION ya kuwa uwezo wa kuzingatia uso na uwepo na upendo wa mtu, ili kutafuta ninini kinaweza kuwa cha thamani na cha kuvutia ndani yake.

Ni nini kinatokea tunapoangalia bila IMAGINATION;
#- Tunakutana na mtu anatuchombeza, yuko poa lakini pua yake ni kubwa sana. (Mmmh NO!)
#- Oh ni injinia, lakini mainjinia hawana mahaba( NNO!)
#- Labda ni tajiri, na matajiri wana radharu na kashfa.(Mimi Hapana)
#- Inaonekana nywele zake zinakuwa nyembamba, na wanaume wenye walaza sio vitu vyetu. (Hapana pia)
#- Ana shape kubwa sana, sitaki mwanamke atakaye kuwa mnene sana( Huyu Noo)
#- Ana shape ndogo havutii(No thanks)
#- Ana lafudhi mbaya sana( Noo!)

"Imagination is the sensitivity to the less obvious things"
Yani hapa mtu ana scan ndani ya mtu mwingine na kutafuta ninini kinaweza kuwa cha thamani ndani yake, mtu ambaye ilikuwa rahisi kabisa kum criticize.

Nini kinatokea kama tukiangalia kwa imagination
#- Ana pua kubwa lakini mdomo wake ni mzuri na wa tofauti
#- Hana shape nzuri sana lakini labda yeye anauwezo mkubwa wa kuishi na watoto na kuvumilia.
#- Hana pesa lakini uaminifu wake na ucheshi unaweza kuwa wa kiwango kingine.

Kuamsha uwezo wetu wa IMAGINATION tunaweza kwa kujaribu kuangalia kwa undani mtu yoyote tukiwa kwenye basi au daladala ambaye kwa haraka haraka tusingeweza kutoka naye, na tujiulize ninini kizuri ndani ya mtu huyu.

Kama tutadeal na chuki zetu kwetu au upendo wetu kwetu , kukosa nafasi mara kwa mara, kuwa bize au kuwa kijijini hakutakuwa sababu ya u single kwa muda mrefu.
 
Nipo single sababu najipenda mimi zaidi, najionea wivu kumkabidhi mtu moyo na mwili wangu...
Umeelezea vizuri sana, nimekuelewa na hiyo ya pili ni kama umenielezea mimi. Asante kwa maneno haya nayafanyia kazi...
 
Nipo single sababu najipenda mimi zaidi, najionea wivu kumkabidhi mtu moyo na mwili wangu...
Umeelezea vizuri sana, nimekuelewa na hiyo ya pili ni kama umenielezea mimi. Asante kwa maneno haya nayafanyia kazi...
Njoo pm
 
Nipo single kwasababu tuliyeshindwana amenifanya niogope kuingia kwenye mahusiano though watu wengi wanataman kuwa na mm sijui muonekano wangu unashawishi nn
 
Nzuri sana hii, ndo nagundua kua sababu za kuwa single ni mbili tu, kujichukia sana au kujipenda sana. Ukweli usiopingika.
 
"Thou shalt marry" amri hii haipo kwenye Biblia Takatifu. Nadhani msipende kulazimisha watu wasio kwenye mahusiano kuwepo kwenye mahusiano kwa nadharia za kutungwa........

Wamekuwepo watu mashuhuri ambao hawakuwahi kuoa wala kuolewa, na walikuwa hawana tatizo lolote kama unavyosema hapa. Kikubwa zaidi ni kwamba waliifanyia dunia makubwa mno kuliko hata waoaji/waolewaji.......

Tuwaache watu waishi maisha yao.....
 
"Thou shalt marry" amri hii haipo kwenye Biblia Takatifu. Nadhani msipende kulazimisha watu wasio kwenye mahusiano kuwepo kwenye mahusiano kwa nadharia za kutungwa........

Wamekuwepo watu mashuhuri ambao hawakuwahi kuoa wala kuolewa, na walikuwa hawana tatizo lolote kama unavyosema hapa. Kikubwa zaidi ni kwamba waliifanyia dunia makubwa mno kuliko hata waoaji/waolewaji.......

Tuwaache watu waishi maisha yao.....
Ubaya ni kuwa jamii kubwa duniani hasa hasa kwetu huku Afrika hiki ulicho andika hawa fahamu na wala hawataki kufahamu.
 
Uhuru binafsi unao tengeneza focus iliyo bora katika jambo/mambo fulani hii pia inapaswa kuzingatiwa kama sababu ya msingi kwa nini mtu hajihusishi na mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote.
 
Uhuru binafsi unao tengeneza focus iliyo bora katika jambo/mambo fulani hii pia inapaswa kuzingatiwa kama sababu ya msingi kwa nini mtu hajihusishi na mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote.
Self love
 
Back
Top Bottom