Saba Saba 2008 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Saba Saba 2008

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Jul 1, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Assalam alaikum wanaJF,

  Hivi kweli jamani kuna haja yoyote ya mtu kuchoma mafuta yake kwenda sabasaba?Nimejiuliza maswali mengi sana nakosa majibu nimeona ni bora niwaulize na nyie wenzangu pengine mtanipa mwangaza,
  Nienende saba saba kununua plastic products kama watu wengi wananvyofanya?niende sabasaba kufanya nini hasa?nitafaidika na kitu gani?nini kipya kupita miaka yote ya nyuma?

  Nimeimiss sana sabasaba ile ya enzi zile wakati ule ilikuwa sikukuu ya wakulima.Nimemiss kuona mabanda ya wakulima na wafugaji. Nimemiss kuona jinsi wakulima wa wakati ule walivyo kuwa mahodari kwenye kazi zao.

  Pengine baada ya wakulima kugundua wamekuwa mayatima serikali ikaona ibadilishe maudhui ya sabasaba? sina majibu naombeni kutoka kwenu wazee,

  Sokomoko.
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..hivyo ulipokuwa ukienda ulikuwa unaona cheap plastic products tu?

  ..usiwe mvivu,tembelea banda la maliasili,ttcl,bot,bunge na hata yale ya kina mama. ukichoka kakae sehemu ule nyama choma au kuku pale steers.

  ..hata mi nime-miss kale ka treni na zile bembea. but what's the point? siku hizi si kuna 88,au haujui?

  ..hamna yatima katika hilo,serikali itafanya mangapi?
   
 3. green29

  green29 JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Kungekuwa na banda ambalo wananchi wangepata kuwaona live kina RA, Karamagi, Chenge, Vithlani, Mkapa na pia kuuliza maswali mbalimbali labda 7-7 ingekuwa na mvuto wa hali ya juu!
   
 4. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #4
  Jul 2, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hahahahaha!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi haiwezekani kuwa na mabanda ya vyama vya siasa????
   
 6. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  i used to feel the same way too ... niende kuchezea vumbi halafu nizunguke kama pia ... nikaona no.. but one time kunamtu aliniambia there's some iranian nice stuff pale for decoration ... i decided to go .. nikavutiwa nikafika mpaka kwenye mabanda ya wanyama pori ... that year there was a big gorilla on display ... nikaenda pale ... i heard a small child asking the mother ... mama yule nani (pointing to the gorilla) ... the mama answered ... babaako .. wonder what the hubby did wrong that day???

  There is always fun
   
 7. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Maonyesho Ya 77 Yanamambo Mengi Kuna Mabanda Kma Ya Wajerumani Mara Nyingi Huwa Wanaleta Vifaa Vinavyofaa (mashine) Kwa Kilimo (umwagiliaji),viwanda Kutengeneza Vitu Mbali Mbali Na Hawa Maranyingi Huwa Wanakuja Kwa Aajili Ya Maonyesho Tu Haya Ya 77 Na Kuondoka Hawana Ofisi Bongo,

  Ukienda Sido Unakuta Wajasiria Mali Wadogo Na Mashine Zao Walizotengeneza Hapahapa Kwetu, Magereza Wanaongoza Kwa Kilimo Na Ufugaji Wa Kisasa

  Si Lazima Ukanunue Plastiki Yapo Mataifa Mengine Yanakuja Kwa Ajili Ya Kutangaza Mashine Zao Zinzofaa Kwa Kilimo Na Viwandani
   
 8. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Kinachokosekana ni ubunifu kwa waandaaji wa maonyesho na kuendelea kung'ang'ania mazoea wakati mazingira yanabadilika kwa kasi kubwa sana. Siku hizi kuna maduka makubwa mazuri na yanafikika kwa urahisi lakini sabasaba ni ile ile, kama una gari wanakucharge kwa kupaki na usumbufu mkubwa sana kufika huko.

  Binafsi ninamashaka na faida inyopatikana kutokana na maonyesho hayo zaidi ya kuwa mtego wa wajanja na mafisadi kuendelea kunyonya watanzania. Cha kustajaabisha ni taasisi za umma kushika chati ya ushiriki na kuongoza katika tuzo na si kama wakati ule IPP inaongoza, Taasisi ambazo zinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi ndio vinara wa sabasaba siku hizi. Ukiangalia kwa undani utaona nafasi kwa wafanyabiashara na wakulima wadogo wadogo ni finyu sana hasaha gharama za maonyesho ni kubwa kwa mkulima au mjasiriamali wa kawaida.

  Zaidi naona kama ni jukwaa la wanasiasa kuuzia sura, jana nilimwona Mh. Pinda anatoa longolongo katika luninga kuhusiana kuona haja ya kuunda chombo kitakacho shirikiana na BET. Wakati BET wenyewe wanasubiri sabasaba kila mwaka na hakuna faida ya BET ambao kwao biashara ni Korosho, Chai, Kahawa, Pamba na katani na nje kwao ni ulaya na marekani. Yaani fursa zilizopo Kongo, Malawi, Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi n.k hawazioni. Shida yote hii ya chakula duniani wabongo bado tunasoma mchezo na ardhi kubwa haina kazi. Pinda na wenzake bado wanaangalia mkakati badala ya kuchukua hatua.

  India inaendelea kwa kutoa wafanyakazi ktk nchi mbali mbali bongo tumelala na vijana wetu wanaendelea kuwa mateja kwa kukosa kazi.
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..for this,you are not innocent!
   
 10. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Dar si Lamu ... am tena kweli kweli vile ..
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  That's wht I wanted to hear, sio kwenda kule kula vumbi tu kuzunguka bila mpango! Kuna mchangiaji amesema kuna decorations nzuri sana kutoka Iran ningemshauri aende kwenye duka la wachina samra/morogoro road au lile la wapalestina derma pale kisutu au lile la mtaa wa samora kelvin house!

  Kila mwaka tumekuwa tukishuhudia maonyesho yale yale kama ku copy and paste! alie enda mwaka jana hana tofauti na alieenda mwaka huu.

  Hivi niende saba saba kuangalia golira?au banda la wanyama?for what for? si bora niende national parks nikajionee wanyama wakiwa free waki browse na ku graze? varaties of animals!

  Last year july I was in ngorongoro I real enjoyd Wallahi! the landscaping and views! this country is so rich rich mond haki ya Mungu!

  Anyway what I can say Saba saba akuna jipya! ni kama vile mtaa wa congo machinga type of business tofauti hii ya saba saba inafanywa na wenye pesa! ile ya congo inafanywa na masikini wenye mitaji midogo!

  Naomba kuwakilisha
   
 12. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180

  ..tembea ujionee! usingoje kuambiwa!
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Maonyesho ya biashara ni sehemu inayokutanisha wafanyabiashara mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya nchi yetu na kutoka mataifa mbalimbali, wanaokuja na bidhaa zao au catalogy za bidhaa zao, kwa ajili ya kutafuta soko. Kwa maana nyingine maonyesho ni sawasawa na ofisi, utulivu unahitajika, mawasiliano yanahitajika. Ukiingia lango kubwa utapokelewa na kelele za music kutoka ndani ya ofisi za BET, kila kona kuna kelele za ajabu, mabaa yamezagaa kila kona ya uwanja kila mmoja akijaribu kufungua music kwa sauti kubwa kushinda wenzake. Vikundi vya ngoma vipo, bendi za muziki zipo nyingi. Inaonekana hawa jamaa wa BET hawako makini wanachojali ni idadi kubwa ya watu waiingie wapate pesa. Jambo hili limepigiwa kelele sana na shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI), lakini BET hawaoni, hawaambiki na hawasikii. Ndiyo maala CTI walijiondoa kushiriki kwao kwenye maonyesho yanayoandaliwa na BET kwa muda mrefu sasa. Ni lazima BET sasa wabadilike, maonyesho ya biashara ya sabasaba yawe ni maonyesho ya biashara hasa na waachane na biashara za umachinga zinazofanyika ndani ya uwanja kwa fujo za makelele.
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2008
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ....you definitely have a point there, mkuu...!!:D
   
Loading...