Saa imetimia - madaktari waonyesha njia

Saa imetimia - madaktari waonyesha njia

Yani hawa madaktari wamenikosha kweli mwenyewe naumwa hapa lakini niko na vidonge vyangu tu hapa!Mmefanya la maana sana na mna support ya wengi.Tumechoshwa na serikali ya udhalimu na ya waovu
 
Hii filamu haina mwisho mzuri kwa mustakabali wa taifa hili...ngoja tuione itavyoingia sura mpya hapo kesho kama sio leo jioni
 
upumbavu mwingine..bado migomo ya chuo kikuu cha dar es salaam ndio yenye tija hadi sasa..
Madactari walimu on the same chaine
 
Pinda alipopeleka barua ya wito kuwataka wakutane jana karimjee c alipeleka kwa uongozi huo wa Dr Ulimboka?wakati huo hakujua kama sio Dr (hakumaliza)? how come anaibuka na kusema Ulimboka c Dr?
 
Acha siasa mtoa mada, hayo ni sawa na maneno wanayoyasema Wagunge kuwa wanapiga vita Ufisadi kumbe wenyewe ndio mafisadi. Sasa unataka Madaktari wafungue Account watanzania wawachangie wakati hawataki kuwahudumia na wanakufa, Wachangiwe kwa lipi hasa. Hivi umekurupuka au umefikiria? Hivi unaweza kumchangia mtu ambaye hakutimizii matakwa yako? ningekusifia sana laiti ungesesma Madaktari warudi kazini kisha ukaitisha mwito kama huu kwa Watanzania kuwa tuwachangia madaktari na wauguzi ili kuwaongezea kipato. Kuliko unaposema wagome alafu tuwachangie.
 
Ubatili mtupu kwa dr. Kurejea kazini kwa kutii agizo walilolikataa tangu mwanzo,...kama wametii basi mgomo wa kuleta mabadiliko ya sekta ya afya utafanywa na ma dr wa india watakapo goma!
 
Endapo madaktari watakuwa wameamua kurudi kazini, .......nawaonea huruma wagonjwa!! Wataona bora mgomo ungeendelea!
DC ni kweli kabisa, wakirudi kwa mtindo huu wa mabavu na sio kwa mioyo yao basi tusubiri disaster. Yale mambo ya mgonjwa wa goti kufanyiwa upasuaji wa kichwa sasa yatakuwa ya kawaida.
Waweza kumlazimisha Punda kubeba mzigo wako ila huwezi kumlazimisha kunywa maji.
 
Bdo polisi na wenyewe wanawavutia kasi tu,wanasema wamechoka kukaa nyumba za fulu suti!!Sasa hao wakigoma japo siku moja tu sipati picha traffic jam na vitendo vya uhalifu vitakavyokywa aisee!!
 
gadafi alikuwa hivi hivi mwishowe yakamtokea puani sasa kazi kwako pinda na kauli zako za kilevi ...hao sio akina mgaya mnaowatisha wanatishika wewe mwenyewe unajua unaumwa afu anaanza ujeuri na madokta ..watu wengine bana
 
Inapendeza kusikia wapo kazini. Ila vyema tuseme tuwachangie sasa ili kuwaongezea kipato kuliko hiyo njia uliyosema tuwaunge mkono. mchemko mkubwa sana
 
Appolo siyo ya viongozi wa CCM tu, hata Mh Zitto aliposumbuliwa na kipanda USO, Mh Spika alisema tutampeleka Appolo. Sisi tu ndio tunaodanganyika eti viongozi lazima wawe wa CCM. Ndio watibiwe nje ya nchi
 
Madactor hawana uzalendo hawa. Kwanza kodi zetu zinawasomesha alafu wanaenda kufanya kazi nje, mkopo wanaurudisha kweli? Nafikiri wakati umefika kwa serikali kuweka mkataba na kila anayetaka kusoma fani ya udaktari kuwa atafanya kazi kwa muda wa miaka mitano ndipo aruhusiwe kwenda atakako ili kuondoa uonevu unaofanywa na madoctor dhidi ya serikali kwa kusomeshwa kisha kukumbilia nje au kugoma kutoa huduma. Kama maisha magumu ni kwa wote hata wanasheria pia, mnajiona nyie wa muhimu kupita fani zingine ilhali hakuna asiyemtgemea mwingine. uruma hivyo hamsitTunahitaji better life lakin si kwa kuuwa wagonjwa, hamna huruma hivyo hamstahili kazi hiyo ya wito. Shame on you Doctors. Tena huwa mnasoma kwa kudesa ndo mana hamjui mnachofanya inapokuja muda wa kupratice.:shock:
 
Kama huu mgomo sio wa Appolo Hospital basi serikali ya CCM hauwahusu maana wo wanatibiwa India.

Halafu wanadanganya watu kama watoto. Wao mtu akikohoa tu, anaenda Apollo! Sie kina sisi tunaenda wapi?
 
Madactor hawana uzalendo hawa. Kwanza kodi zetu zinawasomesha alafu wanaenda kufanya kazi nje, mkopo wanaurudisha kweli? Nafikiri wakati umefika kwa serikali kuweka mkataba na kila anayetaka kusoma fani ya udaktari kuwa atafanya kazi kwa muda wa miaka mitano ndipo aruhusiwe kwenda atakako ili kuondoa uonevu unaofanywa na madoctor dhidi ya serikali kwa kusomeshwa kisha kukumbilia nje au kugoma kutoa huduma. Kama maisha magumu ni kwa wote hata wanasheria pia, mnajiona nyie wa muhimu kupita fani zingine ilhali hakuna asiyemtgemea mwingine.Tunahitaji better life lakin si kwa kuuwa wagonjwa, hamna huruma hivyo hamstahili kazi hiyo ya wito. Shame on you Doctors. Tena huwa wengi wenu mnasoma kwa kudesa ndo mana hamjui mnachofanya inapokuja muda wa kupratice.:shock:
 
Back
Top Bottom