Saa imetimia - madaktari waonyesha njia

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
Huko nyuma nilisha wahi kusema, siku ambayo watanzania walalahoi watakapoamua kuingia barabarani, sijui watawala hawa watakimbilia wapi kujificha. Sasa wakati umefika, na wakati wenyewe ni leo Jumatatu tarehe 30/1/2012. Siku ambayo Serikali iliyochaguliwa na Wananchi wake wenyewe, imewageuka na kuamua kufanya mauaji ya halaiki kwa kuwanyima huduma muhimu ya afya.

Nafahamu, Madaktari leo hawawezi kurudi kazini, na nafahamu Manesi na wahudumu wengine wa afya kuanzia kesho watoa matamko yanayofanana na hili la Madaktari, Madaktari Bingwa nao, muda si mrefu watatoa tamko linalofanana na hili la madaktari, na kitakachofuata hapo ni kilio na kusaga meno. Kwa sababu watakao athirika ni watanzania wote wa kawaida bila kujali itikadi zao au kazi zao, tutasikia na chama cha waongoza ndege nao wanagoma, Dawasco nao watagoma, Tanesco nao watagoma, kwasababu hakuna atakayepona kwa hili.

Kwa vile Madaktari wameonyesha njia, tuwaunge mkono watanzania wote wenye mapenzi na nchi hii, na kupigana na serikali dharimu. Hatuna silaha, kama wao walivyo na majeshi, lakini umoja wetu ni silaha tosha. Napendekeza kwa kupitia kamati maalum ya madaktari, wafungue account huru, ambayo sisi wapenda mabadiliko tutawachangia na pesa hizo zitawasaidia kujikimu ktk kipindi hiki kigumu. Tunafahamu hawa wenzetu wana familia na ndugu wanaowahusu na kuwategemea. na kwavile vita hii si ya kwao peke yao, hatuna budi kusaidia kwa hali na mali kuendeleza mapambano. Nina uhakika watu wengi watajitoa kuchangia account hiyo ya Madaktari, na wao wakipata pesa hizo watajua namna ya kuzigawanya. Shime MaDoctor wa ukweli, Shime JF na Watanzani wapenda mabadiliko, muda wa kulalamika umeisha, tufanye kwa vitendo. Dr. Ulimboka, tuwekee hiyo account details leo hii hii, au kama kuna njia nyingine ya mbadala tujuze. Tupo pamoja.
 
Mie nitatoa, na wala si moja ya kumi ya kila ninachoweza kupata bali kwa kadri ya uwezo wangu wote.

Bila jitihada kama hizi, Watanzania tutaendelea kuishi kama houseboys au house girls wa watawala!!
 
Kama huu mgomo sio wa Appolo Hospital basi serikali ya CCM hauwahusu maana wo wanatibiwa India.
 
Na sisi wamachinga tuna mpango wa kuanza kutundika nguo kwenye ukuta wa nyumba nyeupe pale magogoni..uswazi ata leso azitoki.
 
taarifa zilizopatikana asubuhi hii ni kwamba katika hospitali nyingi madaktari wapo kazini.
 
Madaktari twawapenda sana watanzania, tunawapa pongezi kwa kukaidi agizo la Dr. Ulimboka aliyetaka kuwaingiza motoni.
 
Hakuna cha njia walioonesha. Walianza magwanda, wakaja wanafunzi, sasa madaktari. Magwanda vipi? wanafunzi vipi? Na hawa madakatari ni hali kadhalika, kwa huu upuuzi wao, hata walipoitwa na waziri mkuu kuongea walimdharau, wanaounga mkono ni wachache wasio na muono.

umelala nje nini?
 
Huko nyuma nilisha wahi kusema, siku ambayo watanzania walalahoi watakapoamua kuingia barabarani, sijui watawala hawa watakimbilia wapi kujificha. Sasa wakati umefika, na wakati wenyewe ni leo Jumatatu tarehe 30/1/2012. Siku ambayo Serikali iliyochaguliwa na Wananchi wake wenyewe, imewageuka na kuamua kufanya mauaji ya halaiki kwa kuwanyima huduma muhimu ya afya.

Nafahamu, Madaktari leo hawawezi kurudi kazini, na nafahamu Manesi na wahudumu wengine wa afya kuanzia kesho watoa matamko yanayofanana na hili la Madaktari, Madaktari Bingwa nao, muda si mrefu watatoa tamko linalofanana na hili la madaktari, na kitakachofuata hapo ni kilio na kusaga meno. Kwa sababu watakao athirika ni watanzania wote wa kawaida bila kujali itikadi zao au kazi zao, tutasikia na chama cha waongoza ndege nao wanagoma, Dawasco nao watagoma, Tanesco nao watagoma, kwasababu hakuna atakayepona kwa hili.

Kwa vile Madaktari wameonyesha njia, tuwaunge mkono watanzania wote wenye mapenzi na nchi hii, na kupigana na serikali dharimu. Hatuna silaha, kama wao walivyo na majeshi, lakini umoja wetu ni silaha tosha. Napendekeza kwa kupitia kamati maalum ya madaktari, wafungue account huru, ambayo sisi wapenda mabadiliko tutawachangia na pesa hizo zitawasaidia kujikimu ktk kipindi hiki kigumu. Tunafahamu hawa wenzetu wana familia na ndugu wanaowahusu na kuwategemea. na kwavile vita hii si ya kwao peke yao, hatuna budi kusaidia kwa hali na mali kuendeleza mapambano. Nina uhakika watu wengi watajitoa kuchangia account hiyo ya Madaktari, na wao wakipata pesa hizo watajua namna ya kuzigawanya. Shime MaDoctor wa ukweli, Shime JF na Watanzani wapenda mabadiliko, muda wa kulalamika umeisha, tufanye kwa vitendo. Dr. Ulimboka, tuwekee hiyo account details leo hii hii, au kama kuna njia nyingine ya mbadala tujuze. Tupo pamoja.

Daktari anapoanza kazi tu mshahara ni 957,500/= je wewe unayetaka kuwachangia utaweza kuwapa wanavyohitaji? Lakini pia uhamasishaji wako hauna maana kwa kuwa wananchi hawezi kuwaunga mkono huku ndugu zao wanakufa kwa mgomo wao.
 
Hakuna cha njia walioonesha. Walianza magwanda, wakaja wanafunzi, sasa madaktari. Magwanda vipi? wanafunzi vipi? Na hawa madakatari ni hali kadhalika, kwa huu upuuzi wao, hata walipoitwa na waziri mkuu kuongea walimdharau, wanaounga mkono ni wachache wasio na muono.

Unajulikana kwa hoja sisizo na tija hapa JF...KE_GE mkubwa wewe!!
 
Viongozi wenye busara tanzania wanakwisha sasa?............, hivi kwa nini watawala wanaogopa kuongea na wasomi?...... hapo ingekuwa JK angewaita wazee wa Dar............., na angewaponda sana hao maDR kama kawaida yake.... lakini huwezi kutatua tatizo kwa vitisho.............., hata mtoto unamtisha anapokuwa ndogo, akikua mnaleweshana na kujadiliana sio kwa vitish tena....
 
Madaktari twawapenda sana watanzania, tunawapa pongezi kwa kukaidi agizo la Dr. Ulimboka aliyetaka kuwaingiza motoni.

Wengi wametambua kuwa ULIMBOKA siyo Daktari wa serikali hana cheti cha udaktari kwa kuwa hakumaliza Internship.... Ni muhuni tu!
 
duh, kumbe bado ndogo sana, Mh mbunge analipwa Fuel Allowance kwa mwezi Tshs, 2,500,000/=

Daktari anapoanza kazi tu mshahara ni 957,500/= je wewe unayetaka kuwachangia utaweza kuwapa wanavyohitaji? Lakini pia uhamasishaji wako hauna maana kwa kuwa wananchi hawezi kuwaunga mkono huku ndugu zao wanakufa kwa mgomo wao.
 
Viongozi wenye busara tanzania wanakwisha sasa?............, hivi kwa nini watawala wanaogopa kuongea na wasomi?...... hapo ingekuwa JK angewaita wazee wa Dar............., na angewaponda sana hao maDR kama kawaida yake.... lakini huwezi kutatua tatizo kwa vitisho.............., hata mtoto unamtisha anapokuwa ndogo, akikua mnaleweshana na kujadiliana sio kwa vitish tena....

Kwa wewe unayeona kuwa Waziri Mkuu katoa vitisho subiri uone kama hao watakaoendelea na mgomo hawatajifukuzisha kazi.
 
Kama huu mgomo sio wa Appolo Hospital basi serikali ya CCM hauwahusu maana wo wanatibiwa India.

Umesahau Aga Khan, Hospitali za dini, Mindu Mandal etc. Wakigoma hao, Nyoni mwenyewe atasalimu amri.
 
Back
Top Bottom