Mambo mengine fanyeni utafiti kwanza, je, unajua kuna version ngapi za S-300? Nani kawambieni kwamba export version ya S-300 ni sawa sawa na inayo tumiwa na jeshi la Urusi!! FYI Warusi si wajinga kama unavyo wafikiria wewe, walijua wakiwauzia Wagiriki Air Defence System type S-300 bila shaka Israel na Amerika watakuwa na shahuku kubwa ya kujua inavyo fanya kazi ili wabuni mbinu za kui-defeat.
Soma taarifa za Israel na marafiki zake wanasema nini kuhusu uwezo wa S-300 iliyo nunuliwa na Wagiriki kutoka Urusi, Israel imejaribu mara lukuki kui-jam lakini walishindwa - wanakiri kwa kauli yao kwamba walikuwa wanawazuga Wagiriki kwa kujidai wafanye mazoezi ya kijeshi kwa pamoja kumbe lengo lao ni kutafuta mbinu za kutumia ECM zao ku-blind S-300, Waisrael wanasema mbinu zote walizotumia bado radar za S-300 zilikuwa zinatrack ndege zao hivyo zingekuwa rahisi kutunguliwa na missile za S-300.
Kumbuka S-300 waliyo wauzia Wagiriki ni export version i.e a watered down Defence System, kama Wayahudi na Uncle SAM hawajapata jibu la ku-defeat export version ya S-300, je, version inayotumiwa na jeshi la Urusi ndiyo wataiweza? labda watumie mbinu za kupora system nzima nzima kutoka kwa Wagiriki kama walivyo fanya wakati wa vita 1973 kwa kupora SAM-6 iliyo kuwa inatumiwa na Waarabu, licha ya kufanikisha uporaji huo yet it took Israel and US six years kuelewa SAM-6 inavyo fanya kazi - je,wakifanikiwa kupora S-300 itawachukua miaka mingapi kupata dawa yake - jibu unalo. Hata Turkey ikinunua S-400 mambo yatakuwa yale yale - watauziwa a watered down version ambazo hazitumiwi na jeshi la Urusi, hata Uturuki ikirubuniwa na Uncle SAM na Israel kwamba wastrip S-400 to bare bones ili waichunguze inavyo fanya kazi, Russians won't mind watabaki wanawacheka tu kwa kutapa tapa kwao.
Ukweli wa mambo Warusi wanajiamini ndiyo maana uwezi kusikia hata siku moja wanangahika kuiba au kununua ndege za kivita za Uncle SAM au silaha zao zingine na kwenda kufanya reverse engineering - tafuteni historia inayo eleza mbinu zilizo tumiwa na Amerika kuiba ndege za Warusi na kuzisafirisha kwa meli mpaka USA na ushahidi hupo - mfano: MiG-15, MiG-17, MiG-19, MiG-21 mwaka 1976 MiG-25 - Miaka ya hivi karibuni walinunua MiG-29 karibu 26 walinunua tena ndege za vita 19 aina ya Sukhoi-27 - ndege zote tajwa hapo juu zilinunuliwa kutoka katika nchi za Ulaya ya mashariki zilizo kuwa zinahunda SOVIET za zamani - Taifa linalo jiamini aliwezi kuangahika kupora pora ndege na silaha nyingine za washindani wako kwenda kuzichunguza zinavo fanya kazi na kuishia ku-copy copy tu na mbwembwe chungu mzima.