Rwanda waanza kutoa chanjo ya COVID19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Chanjo dhidi ya Covid-19 imeanza kutolewa nchini Rwanda kwa wahudumu wa afya, wizara ya afya imetangaza.

Afisa wa wizara ya afya ameiambia BBC kuwa chanjo dhidi ya corona inaanza kutolewa mapema wiki hii, chanjo ya Pfizer inaanza kutolewa kwa baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali za mjini Kigali.

Katika tangazo lililoandikwa Twitter, wizara ya afya imesema chanjo hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa kimataifa na kwa kiasi kidogo.

Misri, Equatorial Guinea, Mauritius, Morocco na Seychelles ndio mataifa ambayo yanaanza kutumia chanjo.

Maofisa nchini Rwanda wamesema awamu hii ya kwanza itafuatiwa na usambazaji wa vifaa vinavyotarajiwa kutoka kwenye mradi wa Covax na Umoja wa Afrika kwa kipindi cha muda wa mwezi mzima.

Mataifa mengi yanasubiri chanjo ya Oxford ya AstraZeneca kusambazwa kupitia mpango wa Covax.

Zaidi ya wagonjwa 17,000 wameripotiwa kupata Corona na vifo 236 vimeripotiwa na wizara ya afya ya Rwanda.
 
214a5c1fdf5f420c8d851ed410322871.png

Hii ndo chanjo inayoaminika kwa sasa.
 
Kuna siku nilimsikiliza Bill Gate anahojiwa na BBC, alisema katika nchi za Afrika anazotoa misaada, Rwanda anaona value for his money.
ni kweli ,kwa sababu Rwanda ni sehemu ambayo anatarajia kufanya majaribio ya chip zake zile za kumonitor will ya binadamu.. wanyarwanda hawana namna mkuu wao anapiga dollars tu kutoka kwa gates.
 
Back
Top Bottom