Rwanda Vs Uganda nani atashinda Vita?

😄😄😄 Basi tufanye US ilishinda Vita ya Vietnam,Russia iliwashinda Muhajidina huku USA ikiwashinda Taliban 😄😄
 
Huyu anayesema Tz vs Rwanda jasho litatutoka hivi haya si matusi mkuu kwa tpdf?

Au tunajioverrate bure?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya Rwanda na Uganda, watajuana wenyewe. Ila ikitokea Rwanda wakajichanganya kwa TZ, wataenda kusimuliana huko Jehanam.

Tutapeleka vifaa kadhaa hapo Kigoma, then tunawaachia ndugu zetu "Waha" kazi ya kumnyoosha Kagame, huku mikoa yetu mingine ikiendelea na shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa!

Na tunavyozitamani pisi zao, wajichanganye tu!
 
Wanajeshi wa tangu 1980s ndio unasema wanajulikana na siri zao zinajulikana. Ukishajua Uganda wana Su-30 fighters na Mil Mi-24 attack helicopters ndio unashinda vita bure?

Rwanda sio wazembe ila hii sio point. Ni sawa na kusema Tanzania itaishinda Angola kwa kuwa tuliwahi toa support kwenye vita yao na makaburu
 
Safi..kumbe hata Kenya ni kelele tu sio na KDF yao..

No wonder operations nyingi za kimataifa mkono wa tpdf unakuwa na umuhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza Kenya ktk majeshi yako very indiscipline kwa East Africa nadhani la kwanza Ni Jeshi la Burundi then linafuata La Kenya,hata wapewe vifaa gani pale Ni bure kabisa.

TPDF Ina mizizi mirefu tena Sana tu.
 
Point yako ni Nini?
 
Hizo Bairaktar TB2 zinauzwa bei ndogo sijui kama Turkey hawatazipandia bei maradufu. Zina bei ndogo kiasi kwamba vichaa wa procurement kama Egypt wakinunua wanaweza chukua units hata 200 kwenye planned budget ileile. Na hazina masharti magumu kwa wanunuzi, unless supplier wa components kama Canada waweke vizuizi
 
Point yako ni Nini?
Rwanda haiifahamu Uganda kisa Kagame aliwahi kuwa CMI. Mambo mengi yamebadilika tangu miaka Kagame yuko Uganda. Hapo kuna seniors kibao wamestaafu na wamebadilishwa majukumu. Hata hivyo ukijua taarifa na huna namna ya kuzichakata hazikufai kitu. Rwanda itajua airbase za Uganda zilipo, ishambulie sasa kwa kutumia nini?
 
Jua hivi Kampala ilikamatwa na 1st, 7th, 11th, 13th, 19th, and 35th battalions ambazo hizo zote zilikua chini ya wanyarwanda, Sasa hapo sijui location ya Kampala itakua imebadilika?BTW Kampala ilikamatwa na hao wkt M7 akiwa zake Sweden ilikokua familia yake.

Wanyarwanda kwny jeshi la Uganda wameondoka officially 1995,baada ya hapo Hali ikawa tete huko Entebbe, Jinja na Kampala ikabidi M7 awaombe wanajeshi wa Rwanda(RPA) warudi kumsaidia kutuliza Hali,ikabidi vikosi vitumwe chini ya Maj. Alex Kagame(usimchanganye na Paul Kagame) akiwa na kikosi cha artillery na anti-aircraft wakapigana na kuikamata Entebbe airport,eneo lenye rada la Nsamizi,Owen Falls Dam, Kule Lugazi kwny Viwanda vya sukari etc wakashikilia hayo maeneo kwa miezi 12 Hali ilipotulia wakayakabidhi kwa serikali ya Uganda.

Hata kikosi Cha ulinzi Cha M7 kulikua chini ya wanyarwanda wakina Captain Charles Muhire(OPTO) and Captain Charles Ngoga, the PPU Commander (OC).

Kifupi tu,nimetaka nikuonyeshe RDF Wanaijua Uganda nje ndani.
 
So far Morocco wanazo 13,Ethiopia nao wameagiza kadhaa,Rwanda wameagiza 12 etc hizi nyingine Ni story za kanyabazongo.
 
Wale magaidi kule Msumbiji hawakutoka hadi Rwanda walipotia timu. Kutokana na hilo, kuna haja ya kuichamnua vizuri na kiundani hii mada kuliko suala la population na ukubwa au udogo wa geographical location
 
'waha' wenyewe Red tabara inawatoa jasho kila Mara mabomu ya hapa na pale hayaishi Mara yanarushwa mtaani,kwny airport,kwny vituo vya mabus 😁😁 wako dhoofu bin Khali.
 
Unaongea pumba.
Kwanza Rwanda hawezi kuchapana na baba yake M7.
Pili huku kwetu anajua shughuli iliyopo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…