Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Kijoigraphia...nchi za EA zinaifanya iwe tegemezi kwa Tanzania....
 

ufinyu na umbumbumbu wa watanzania na wewe unaongoza kwa kusema maneno haya.
 
Una mawazo finyu sana ya kuona mambo kwa mapana yake, kama Rwanda wa njia mbadala wa kuingiza mizigo yao hatuna jinsi la ni kufuata yale madai yao ya msingi katika kufanya nao biashara ama tutegemee kuathirika kibiashara wakienda bandari ya Mombasa.

we ndo nakuona una mawazo mgando tena yaliyovunda kwa kumbwera mbwera na ka mkwara ka huyo "mrembo rwanda",
jikomboe kifikra we choko kwani bila rwanda umeambiwa bandari ya dar itakufa ??
 
Jamani naombeni msaada. Binafsi ninfahamu umuhimu wa bandari za Dar na Tanga. Kwa sababu hiyo zikipanuliwa nitaelewa. Sasa bandari ya Bagamoyo itakuwa ina-serve maeneo gani na umuhimu wake ni upi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums


Bandari ya Bagamoyo nikwa ajili ya usafirisahji wa nekel kutoka Burundi na Kabanga.
 
Huyu Bwana Zacharia Hanspope atakuwa amechemka kwa kutaka kuzitumia nchi za Uganda na Rwanda ili kupata unafuu kwa TATOA.
Ninaamini kuwa private sector inajitegemea hata sisi kama nchi hatuwezi kumieleza mtu anayeagiza bidhaa kupitia sehemu furani bali ana option ya kupitia sehemu yenye unafuu kwake.
Haya mambo hayana siasa.
 


Huyu jamaa japo sikupenda kauli aliyoitoa ila ni kichwa.
 
Kijoigraphia...nchi za EA zinaifanya iwe tegemezi kwa Tanzania....
nijuavyo mimi ni importer (mmiliki wa mzigo) ndiye anaamua mzigo wake upitie bandari gani lakini hii haiondoi ukweli kuwa mlengo wa sera za nchi husika unachangia katika kuwashawishi wananchi wake waamua nini kuhusu mizigo yao. Na pia haina maana kuwa kama nchi iko strategical positioned au advantages zingine basi haina haja ya kufanya bidii kuvutia wateje kwa kuamini kuwa 'watakuja tu'.
Nchi yoyote duniani hata iwe na utajiri au rasilimali za vipi kama watu wake hawana akili (tusitafune maneno hapa) haiwezi kupiga hatua. Kikubwa ni kuwa hizo rasilimali zitaishia mikononi mwa watu wengine maana tusisahau kuwa dunia hasa kwa sasa ni nchi moja na binadamu wote ni raia wake.
 

Kama ni msafiri wa barabara ungekuwa ushajiuliza swali hili siku nyingi... ,Kuna msururu mrefu kwenye mizani ukianzia kibaha, michese, morogoro, dodoma, shinyanga, katika mizani zote hizi lazina lori ipoteze zaid ya dakika arobaini na tano.. (muda unaopotea kwenye mizani tuu ni zaid ya masaa matatu kwa gari moja) ni masaa na bado kuna trafiki katika mkoa mmoja tuu kuna trafiki check poin zaidi ya sita na kila moja ina poteza muda wa dakika kumi (muda unaopotea kwenye hiz check point ni zaidi ya saa moja kwa gari)..

Total time cost per year goes up to billions of money... Kiukweli hatuko kibiashara na viongozi wetu wamekosa vision labda kwa sababu hawayaoni haya na waliochini yao wanafaidika na huu urasimu.. na rushwa..

Hii ni moja kati ya maeneo ambayo wachumi wetu wangefanya utafiti na bila shaka hukosi PHD katika eneo hilii...
Badala ya kuwa objetive na kujiuliza kwanini Rwanda na Burundi wanakimbia bandari zetuu sisi tunachukulia kila kitu personal and subjective.. kwa akili hizi hatuwezi kutoka hapo tuliopo tutakuwa nchi ya laana kina mtu analalamika, hakuna mwenye majibu wote ni lawama na kujihamii tuuu
 

naanza kuhisi harufu ya njaa njaa hapa,ili kuziba pengo usishangae kodi za sim card zikapanda na kuwa buku 5 kwa mwezi........ngoja tuone.
 


Ni mara kumi sisi tufunge mkanda kuliko kuwaandalia wajuku zetu M23. Kama DRC wangewafukuza miaka ile leo kusingekua ni kikundi kinachoitwa M23 kikidai kumegewa sehemu ya DRC. Kwanza siku zijazo tunategemea kuanza kusafirisha nikel tani milion tisa kwa mwaka kitu ambacho bandari ya Mombasa haiwezi kufikia.
 
acha waende zao,hawa kitu kinacho wauma sana wamekuta sivyo ambavyo wametegemea wangepata tanzania kama mnakumbu siku za mwanzo wamepig sana wakitaka ardhi iwe katika jumuiya,huko makwao ukianza na kenya hawana tena ardhi wamegawana siku nyingi imekwisha hata sehemu ya kufugia kuku nikazi kupata, wengi huko ni maskwota,hata ulaya kuna nchi zingine zinazungumzia kujitowa kwenye muungano sembuse uganda na rwanda acha waende zao hawatunyimi usingizi,serikali yetu kama itakuwa makini kukusanya kodi vizuri na kufuta misamaha yote ya kodi na huko kwenye madini wasimamie vizuri tunaweza kupata pesa nyingi sana za kuendesha nchi hata hiyo bandari tunaweza kuwaachia wauza mitumba wa manzese waitumie wao,acha waende zao wafike salama huko waendako
 
Yaani sasa tutaitegemea zaidi Zambia labda na Burundi tu katika kuitumia bandari ya Dar es Salaam.
Malawi nao huitumia bandari hiyo lakini nadhani itafifia sana.

Malawi wanakimbilia msumbiji, Zambia wanakimbilia Walvis Bay Namibia (mzigo unatolewa ndani ya masaa 24), mtabaki na Burundi na Azam. Subirini
 
Maajabu eti Nchi yetu itayumba kwa àjili ya RWANDA na UGANDA (landlocked) acheni zijitoe hata EAC kwahiyo Ntuzu kutufananisha na wezi wa madini huko DRC ni utoto na ngoma hiyo haikeshi na za mwizi ni 40, hebu tuambie ni kwanini mpaka leo Wakimbizi wao hawajarudi kwao? na bado leo wanarudi tena Tanzania, Uganda tu Byesige na wengineo wapinzani wa Museveni ni kufungwa je Tanzania ipo ? Ipo siku mtakuwa na kujua adui akikuingilia chumbani ni kosa kumpa siri za Baba au Mume kuwa àna udhaifu gani kwanza ni kumfukuza adui
 
Last edited by a moderator:

Dreaming is good.
 
Wala msiwe na wasiwasi. Wanaotumia bandari kwa asilimia kubwa ni wafanyabiashara binafsi na taasisi mbalimbali,si serikali za Uganda na Rwanda. Faida kibiashara inakuja kwa fomula ndogo sana ambayo inasema FAIDA=MAPATO-GHARAMA. (PROFIT=REVENUE-COST).Mfanyabiashara yeyote duniani anachokihitaji ni kukuza faida yake hivyo huwa anajitahidi kukuza mapato huku akitafuta gharama ndogo. Serikali inachotakiwa ni kupitia gharama mbalimbali wanazoingia wafanyabiashara kuanzia pale bandarini,barabarani mpaka kufika huko Rwanda na Uganda. Kisha iangalie/ipeleleze gharama za kama hao watu watatumia bandari za Mombasa au Beira. Baada ya hapo sisi gharama zetu tuzishushe kidogo na tuondoe aina mbalimbali za urasimu.Reli ya kati na TAZARA ziboreshwe haraka iwezekanavyo tena kama inawezekana TAZARA wapewe wachina na reli ya kati wapewe wajerumani waziendeshe kwa ubia na serikali(nilisikia China walishaomba hilo serikali iligoma). Hizo nchi zote landlocked lazima watatumia Bandari za Tanzania kwani biashara si blah blah za SIASA bali ni utafutaji wa faida kwa gharama ndogo iwezekanavyo, SIMPLE!. North Korea na South Korea hawapatani na toka miaka mingi nyuma wanatunishiana misuri lakini kuna miradi kadhaa ya ki teknologia na kibiashara wanashirikiana itakuwa hawa Uganda naRwanda kwa Tanzania. Serikali iache utani ifanye kazi!
 

Trafiki barabarani ni kero na mizani zetu ni keroo kila mizani inajaza jam ya malori na mabasi serikali inashindwa nini kuzipanua hizo mizani ziweze kuhudumia gari nyingi kwa wakati mmoja. tatizo letu Watanzania tukiambiwa ukweli tunakimbia ku-attact personal affairs badala ya ku-act objectively.. mkoa mmoja una trafiki check point sita na kila moja wanakusimamisha na kukuuliza vitu vile vile au kukutafutia makosa wanayoona wao yatakuongezea usumbufu ili utoe kitu kidogooo.. rushwa uwajibikaji na utendaji kazi wetu hauna ufanisii... bahati mbaya tunaona tulipoangukia ila hatujiulizi tumejikwaa wapiii??!!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…