SDP_TZ_Mpya
Senior Member
- Jun 21, 2013
- 166
- 77
Swali lako ni sawa na kuuliza 'kwa nini tunajenga daraja la Kigamboni pale kurasini hali kuna kivuko pale ferry na pia barabara ya Kongowe' jibu ni 'Congestion'
Eneo la bandari limekuwa dogo, unalazimika kubomoa nyumba za wananchi kupanua bandari imeshindikana, tufungua Bandari kavu kibao ambazo ni usumbufu na gharama kubwa kwa mteja. ukiachilia mbali msongamano wa malori ya kuhamisha mizigo bandarini kupeleka bandari kavu.
Haya ni matokeo ya kikao kilichofanyika kigali kati ya mseven,kagame na uhuru,,,na watakaa kikao kingine tena hivi karibuni,,sijui watakuja na lipi jipya ,,swala la ushuru na forodha sio sababu yawao kutoitumia bandari ya dar,,bali wanataka kujijenga kiuchumi bila kumshirikisha tanzania ,,maana wanampango wakujenga reli itakayopita uganda,kenya na rwanda
Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.Mnachanganya mambo, someni vizuri mada. Uamuzi wa kupitisha mizigo Kenya si wa Serikali ni wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili. ambao hapa wanasemewa na mtanzania mfanyabiashara wa kusafirisha mafuta, ambaye anajaribukuibana serikali ihararishe uharamia kupitisha ktk barabara zetu magari yake yakiwa na uzito usioruhusiwa kisheria.
Wadanganyika kutokujua tunashabikia maharamia ambao miaka yote ndio wanapenyeza hela zao chafu kwa watendaji serikalini kuchelewesha mipango ya matumizi ya reli ktk usafirishaji mizigo mizito.
Hawahawapaswi kuchekewa!!!
Hii serikali mie sisemi kitu.. we are doomed..
hello! Jf mi naona hapa tunatwanga maji kwenye kinu, mafisadi wamekula hela za bandari hazijawatosha wanataka kuhamia kwenye vitengo vingine, hanspope anasema vikwazo ni ving atwambie ni nani mwenye jukumu la kumaliza matatizo hayo, ili tumpe taarifa kuhusu malalamiko yake, wamelikoroga lazima walinywe
let them Go nothing to worry! kuendelea kulialia na RWANDA&UGANDA kutumia bandari yetu au lah kwetu ni changamoto lakini pia tujue kua ni muda mrefu hawakupenda kufanya hivyo ila kwa sasa ndo wamejidhiirisha roho zao zikoje! Tumshukuru Mungu kwakua na bahari cha msingi apa ndo iwe chachu ya kusimamia na kuanzisha vyanzo vya mapato vingine..leo tunalaumiana lakini tujiulize je nchi ambazo hazina BAHARI chumi zao zinaendeshwaje? Tuwekeje kwenye GAS na italipa tu acha watuondolee Jams na usumbufu
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....
1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?
Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???
Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!
Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....
1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?
Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???
Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!
Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
wasiwasi wangu wasije wakaunda millitary alliance tu hapo ndipo hali itakapokuwa mbayakisha mniambie kuwa EAC itarejea kwenye utengamano wake ! THUBUTU, upo mgogoro mkubwa unafukuta, na tusipokuwa waangalifu TUTAUMIA, tutafute marafiki wapya kusini mwa Afrika,
tatizo hawakuwepo mawaziri wenye uchungu na nchi boara sasa jembe mwakyembe alivyokuwepo ila wasiwasi wangu ni kwamba hapati support ya kutosha kutoka serikali kuuMkuu ule mkutano uliofanyika Uganda kati ya Museveni, Uhuru na Kagame ndio unaelekea kuiua bandari ya Dar Es Salaam. Uhuru kwa kujua kwamba serikali yake soon inawezekana ikawekewa vikwazo vya kiuchumi endapo hatashirikiana na Mahakama ya ICC, alianza mapema kuangalia jinsi ya kuongeza pato la ndani litakaloweza kuziba pengo endapo wahisani watajitoa kuisaidia Kenya. Kumbuka Uhuru aliitembelea bandari ya Mombasa kabla hata ya kuapishwa kuwa Raisi. Pamoja na kukubaliana kujenga reli, Uhuru ameondoa mizani kwa mizigo inayokwenda Uganda na Rwanda, pia amewapa ofisi maafisa wa Uganda na Rwanda kushughulikia mizigo yao wenyewe pale Mombasa. Hii deal iliwafurahisha Museveni na Kagame na sasa tayari wametangaza kuacha kuitumia bandari ya Dar Es Salaam kuanzia Septemba Mosi.
Sisi kama Watanzania lazima tukubali kwamba tumekosa viongozi wenye ubunifu na wanaoweza kuona mbali kitu ambacho sasa inaelekea kitaugharimu uchumi wetu. Ni kelele ngapi zimepigwa na importers juu ya tabia ya wizi pale bandarini lakini hakuna hatua madhubuti iliyochukuliwa. Mtu unaagiza kagari kako lakini by time hilo gari linatoka bandarini, power window hakuna, radio hakuna, wheel cover hakuna, list ni ndefu. Wakati tukishangaa Uganda na Rwanda kuacha kuitumia bandari yetu, hata sisi Watanzania wengi tayari waliisha ikimbia bandari ya Dar Es Salaam na sasa wanaitumia bandari ya Mombasa kwa sababu hakuna wizi wa bila mpangilio wa mizigo, hakuna urasimu usio kuwa na tija wakati wa kutoa mizigo na hakuna kudaiwa rushwa ovyo ovyo.
Tujifunze.
Tiba