Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Hello! JF mi naona hapa tunatwanga maji kwenye kinu, mafisadi wamekula hela za bandari hazijawatosha wanataka kuhamia kwenye vitengo vingine, Hanspope anasema vikwazo ni ving atwambie ni nani mwenye jukumu la kumaliza matatizo hayo, ili tumpe taarifa kuhusu malalamiko yake, Wamelikoroga lazima walinywe
 
wewe kweli ni krapu

hebu niambie unalinganishaje matumizi ya bandari ya watu wa rwanda na wilaya ya ilala au temeke??

if we lose DRC, then tutaumia zaidi, ila si rwanda (kama unavyodhani

Uganda sio watumiaji wakubwa wa Dar, they have been using Mombasa for ages

fanya homework yako wewe imbechili kwanza... hatuangalii bendera tunaangalia numbers

nalaabuk wahed

habari zako za vujiwe vya kahawa sijui kama itakusaidia sana....matokeo yake unaonesha ulivokuwa hujui mambo...kinachokudanganya ni ramani tu....huna data acha watu wenye data wadiscuss....ilala/temeke?well nakupotezea utaniboa....peace bro/sister
 
aisee noma sana
matatizo bandarini yapo
ila kutakuwa na hidden agenda
haka ka urafiki ka udanga na rwanda jaka
tukachek kwa jicho la tatu
kenya kunguru anafurahia vita vya panzi
 
Bandari yetu ingekuwa inafanya kazi inavyopaswa, wala hamna mtu angeondoka, with or without ugomvi.


Halafu bila haya kiongozi anasema haoni mantiki!
 
[JFMP3]http://mp3.com/2012/12/17/free-mp3-grace-danger-love-me-like-its-the-end-of-the-world/[/JFMP3]
 
Khaa!! wewe vipi? Sisi ndiyo wa kuliwa kwenye ajira na ardhi tuingie au tusiingie kwenye shirikisho

Hii ni mbinu ya hizi nchi triple K kujaribu kuishinikiza TZ ikubaliane na mapendekezo yao hasa upande wa ardhi.
2. Kaguta na Kenyata wanautumia mgogoro wa Tz na Rwanda kwa maslai ya nchi zao.
Kwa sasa Tanzania tunakosa kiongozi/viongozi wenye mipango mjalabu ja ku boost uchumi, Tz siyo nchi ya kutegeme bandari tu kiasi kwamba tuone ndiyo mwisho wa uchumi wetu.
 
Mkuu naona unajisumbua bure kumuelimisha huyo mtu. Sisi tunahitaji DRC kuliko hivyo vinchi vidogo, nadhani wakishajiondoa kuna haja ya kusaini mkataba wa makubaliano yaushilikiano na DRC kama USA alivyofanya kwa Saudia Arabia ili DRC watutegemee kwa kila kitu.

sawa bwana elimu ni yangu niliitolea ada usitake kuichukua bure
 
Nchi ya bora liende kama kawaida ila kwa hili tutarajie matatizo zaidina zaidi
 
this is the most serious of all........... nadhan ndio maaan huyo chambo katolewa kwenye hii wizara maana anaongea pumba tu!!! kero za kutoa mizigo bandarini zinaeleweka na suala la mizani pia kua mingi linaeleweka lakini si suala la mizani tu ila mizani imwefanywa kama kitega uchumi cha ndugu za watu... mizani inaongezwa kila cku ili kutoa ajira kwa ndugu za watu.... kero za polisi barabarani nani hajui... madereva wa lori inabidi wawe na kama laki 2 na wanaiomba ofisini kihalali kabisa kua ni hela ya njiani vinginevyo watakua wanasumbuliwa na kupotezewa muda bila sababu!!! tunaingizwa ktk matatizo na serikali dhaifu.....
 
Sasa kama mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ni Andrew Chenge unategemea watu wako serious kweli na serikali hii?
Yaani ktk watu wote mzee wa vijisent ndio amepewa uenyekiti?
Kazi tunayo

aha tujiendeage hivyohivyo mkuu hii nhi inakatisha tamaa kweli
 
Hii ni mbinu ya hizi nchi triple K kujaribu kuishinikiza TZ ikubaliane na mapendekezo yao hasa upande wa ardhi.
2. Kaguta na Kenyata wanautumia mgogoro wa Tz na Rwanda kwa maslai ya nchi zao.
Kwa sasa Tanzania tunakosa kiongozi/viongozi wenye mipango mjalabu ja ku boost uchumi, Tz siyo nchi ya kutegeme bandari tu kiasi kwamba tuone ndiyo mwisho wa uchumi wetu.
UDHAIFU WA dhaifu
 
let them Go nothing to worry! kuendelea kulialia na RWANDA&UGANDA kutumia bandari yetu au lah kwetu ni changamoto lakini pia tujue kua ni muda mrefu hawakupenda kufanya hivyo ila kwa sasa ndo wamejidhiirisha roho zao zikoje! Tumshukuru Mungu kwakua na bahari cha msingi apa ndo iwe chachu ya kusimamia na kuanzisha vyanzo vya mapato vingine..leo tunalaumiana lakini tujiulize je nchi ambazo hazina BAHARI chumi zao zinaendeshwaje? Tuwekeje kwenye GAS na italipa tu acha watuondolee Jams na usumbufu

Hayo ni maneno ya Mkosaji.watu tusitafute excuse ya matatizo yetu.Tumekua na serikali ambayo haiko serious kabisa.Suala la bandari na usafirishaji kwa ujumla limekua la kisiasa zaidi kuliko kiuchumi.Kama tungekua serious tungeongeza ufanisi katika bandari zetu,lakini pia tungehakikisha reli inajengwa ya kwenda uganda na rwanda ili kufanikisha wao kupata mizigo kwa haraka na pia,kupunguza gharama za uharibifu wa barabara zetu.Lakini kwa kua viongozi wetu wa serikali wanachaguliwa kutokana na siasa ,yaani chama wanachotoka tuendelee ,kuona madudu na huku uchumi wetu ukiporomokaq,na wao kusaini mikataba feki,ya kuzimilikisha familia zao mali lukuki ,huku watz wakizidi kuteseka,ilhali wana rasilimali za kutosha.Nchi hii bila CCM kuondoka madarakani hali itaendelea kuwa hivi hivi na pengine zaidi ya hivi.
 
Hivi Uganda wameshalipa deni letu (lililotokana na vita vya kagera)
au tumewasamehe!!! "japo ni nje ya mada"
 
Pamoja na agenda ya siri aliyonayo PK hasa ya ugomvi wake na mkuu lakini ukweli unabaki palepale,vikwazo/ukiritimba,urasimu wa uitishwaji wa mizigo mwanzio Bandarini hadi mpakani ni mkubwa sana na unatisha,hebu fikiri kutoka Dar hadi Rusumo kuna mizani ngapi? kwanini gari la mafuta lililopima Kibaha apime mizani mingine ya yoote wakati imefungwa sili?
Police wa ugaguzi kila kona wapo yoote hayo ni vichochoro vya kuchukulia rushwa tu.miye naona nisawa kabisa wacha watafute njia nyingine ya kuharakisha uchumi wao sisi acha tuendelea kumwagiana Tindikali!!!
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
It sound good......that is economical principle....and always it govern the political idea
 
Jamani nchi inanuka nilikuwa Blantyre wk iliyopita Nilitafuta gari ya kupakia mzigo kuleta dar walikataa katakata wanasema hajawahi kuona Trafic wengi barabarani namna hiyo na walarushwa wakubwa,anasema ukimyima pesa unalimwa fine, wao sasa wanaenda msumbiji na south africa, Tujiulize tumepotoka wapi?
 
ujenzi wa barabara ni kitu ghali sana,usipoweka mizani za kutosha njiani itakula kwako tu kwa sababu wenye malori wana tabia ya kuongeza mizigo njiani,jawabu ya hilo ni kuimarisha reli ya kati!!!!
 
Back
Top Bottom