Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

.....Mimi nafikiri ili kuweza kutatua migogoro hii serikali ya tz inapaswa kwanza kuangalia athari mapema kabla ya kuruhusu kujitoa kwa nchi hizi tegemezi kwa matumizi ya bandari yetu.
ni jambo la kushangaza serikali inapoweza kupigia kelele suala la ziwa malawi wakati hakuna tunachoingiza pale zaidi ya wananchi tu kujitafutia riziki zao kwenye hilo ziwa malawi.
... serikali ijaribu kuonyesha sasa nguvu kama ilizoonyesha kwenye mgogoro wa ziwa malawi ambalo kiuhakika sio letu. na inachotakiwa isikilize kero za watumiaji wakuu wa bandari hii kwa faida ya nchi na si kukaa kimya kwa maslahi ya vijitu vichache tena viroho vyenye uchu wa kutafuna uchumi wetu.
TAFAKARI CHUKUENI HATUA..
 
Hata wale watanzania waliokuwa wanapeleka biashara zao nchini Rwanda nao wameathiriwa na fukuto hilo. Wamepewa masharti magumu ya kupeleka bidhaa nchini humo pia wamepandishiwa ushuru maradufu..

Bakharesa ni mmoja wa waathirika kibiashara maana Rwanda ilikuwa kama familia yake analisha kila kitu sembe, jui, maandazi yaani ni kwamba wanyarwanda walikuwa watoto wa kambo wa AZAM, kumbuka wakenya wanavizia opportunity hiyo.Rwanda hawataathirika na kuondoka kwa AZAM kwani wakenya wanakodolea macho na ndicho kenyata is EYEING FOR.Kifupi swala hili watanzania mlishabikia bila ku-assess impact na the multiplier effects.Dr.slaa mlimpuuza yeye alishauri badala ya mipasho wangekaa kwanza wawili at round table, that is hiow conflicts are always addressed.BIG UP DR.SLAAAA lastly the got the message from u
 
kwli ni land-locked if u really are learned huwezi argue hivo economically imekula kwetu...na ndo maana umeona bwana PK anatafuta mbadala kabla hakijanuka zaidi...politics is killing us

wewe kweli ni krapu

hebu niambie unalinganishaje matumizi ya bandari ya watu wa rwanda na wilaya ya ilala au temeke??

if we lose DRC, then tutaumia zaidi, ila si rwanda (kama unavyodhani

Uganda sio watumiaji wakubwa wa Dar, they have been using Mombasa for ages

fanya homework yako wewe imbechili kwanza... hatuangalii bendera tunaangalia numbers

nalaabuk wahed
 
.....Mimi nafikiri ili kuweza kutatua migogoro hii serikali ya tz inapaswa kwanza kuangalia athari mapema kabla ya kuruhusu kujitoa kwa nchi hizi tegemezi kwa matumizi ya bandari yetu.
ni jambo la kushangaza serikali inapoweza kupigia kelele suala la ziwa malawi wakati hakuna tunachoingiza pale zaidi ya wananchi tu kujitafutia riziki zao kwenye hilo ziwa malawi.
... serikali ijaribu kuonyesha sasa nguvu kama ilizoonyesha kwenye mgogoro wa ziwa malawi ambalo kiuhakika sio letu. na inachotakiwa isikilize kero za watumiaji wakuu wa bandari hii kwa faida ya nchi na si kukaa kimya kwa maslahi ya vijitu vichache tena viroho vyenye uchu wa kutafuna uchumi wetu.
TAFAKARI CHUKUENI HATUA..

PK said clearly that I will hit him at the right place, hakumaanisha vita, jamaaa alimaanisha this is real the right place.Nchi inayotegemea kodi ya bandari pekee, kagame kuna wakati aliwahi kusema TZ wanipe mimi bandari niendeshe waone kazi yake.Anajua fika the potentiality of DAR PORT
 
.....Mimi nafikiri ili kuweza kutatua migogoro hii serikali ya tz inapaswa kwanza kuangalia athari mapema kabla ya kuruhusu kujitoa kwa nchi hizi tegemezi kwa matumizi ya bandari yetu.
ni jambo la kushangaza serikali inapoweza kupigia kelele suala la ziwa malawi wakati hakuna tunachoingiza pale zaidi ya wananchi tu kujitafutia riziki zao kwenye hilo ziwa malawi.
... serikali ijaribu kuonyesha sasa nguvu kama ilizoonyesha kwenye mgogoro wa ziwa malawi ambalo kiuhakika sio letu. na inachotakiwa isikilize kero za watumiaji wakuu wa bandari hii kwa faida ya nchi na si kukaa kimya kwa maslahi ya vijitu vichache tena viroho vyenye uchu wa kutafuna uchumi wetu.
TAFAKARI CHUKUENI HATUA..

Mkuu athari watakazopata wananchi waliozunguka Ziwa Nyasaendapo hawataruhusiwa hata kuchota glasi ya maji kwenye hilo ziwa?
 
Sisi porojo,rushwa,majungu,propaganda ndio tumeweka mbele sana kuliko ufanisi!ni ngumu kumeza ila huo ndio ukweli kwa sisi Watanzania!wenzetu wanasonga mbele kwa kujadili mambo ya msingi kwa maendeleo na ustawi wa uchumi wa mataifa yao,sisi tumebaki na porojo za mara tindikali,mara magari ya cdm yaonekana bar,mara sheikh ponda,mara uchochezi na ugaidi,mara ukabila na udini!nonsense,bad enough mpaka kuna baadì ya viongozi wa kisiasa tena wakijinasibu kua wao ni wasomi nao wanasimama majukwaani kuongea porojo hizo badala ya kutoa hoja zenye tija kwa taifa ili
 
chenge.jpg

Na Raymond Kaminyoge,

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.

Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

“Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi,” alisema.

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

“Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo,” alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.

Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.

Nimesikia mara nyingi wawekezaji wa migodi wakipewa upendeleo kwa mfano hata kodi yao ni ndogo wanayolipa. Kwann bandari ambayo ingeweza kutuingizia kipato kikubwa sana hawakuweza kupunguza urasimi na malalamiko ya miaka nenda rudi? Pia hata majibu tu ya malalamiko yangesaidia lkn kimya! Sasa hii maana yake nn.? Naona Serikali inajitafutia majanga yenyewe!
 
Hakuna haja ya kulalamika,cha msingi bandari ipanuliwe,vinunuliwe vifaa vya kisasa kufacilitate utendaji wa kazi,urasimu na kodi kodi ziangaliwe upya.kwa kufanya hivyo wenyewe watakuja
Khaa!! point kuu ya kujitoa ni hii nanukuu " Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

"Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi," alisema."
sasa pima mwenyewe kama sababu hizi zina sense (Chande was right (RIP)):bored:

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.
 
wewe kweli ni krapu

hebu niambie unalinganishaje matumizi ya bandari ya watu wa rwanda na wilaya ya ilala au temeke??

if we lose DRC, then tutaumia zaidi, ila si rwanda (kama unavyodhani

Uganda sio watumiaji wakubwa wa Dar, they have been using Mombasa for ages

fanya homework yako wewe imbechili kwanza... hatuangalii bendera tunaangalia numbers

nalaabuk wahed

Mkuu naona unajisumbua bure kumuelimisha huyo mtu. Sisi tunahitaji DRC kuliko hivyo vinchi vidogo, nadhani wakishajiondoa kuna haja ya kusaini mkataba wa makubaliano yaushilikiano na DRC kama USA alivyofanya kwa Saudia Arabia ili DRC watutegemee kwa kila kitu.
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!

Mkuu hoja yako imekaa vizuri hasa kuhusu uimarishaji wa Reli ya kati.

Bila usafiri mathubuti wa reli tusitegemee ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam kuongezeka!

Kwa mfano treni moja inaweza kubeba hadi tani 1200 kwa wakati mmoja, ambao ni mzigo wa lori 30 zenye uwezo wa kubeba tani 40. Mzigo wa treni 5 tu kwa siku ni sawa na lori 150.

Bandari inaweza kuhudumia malori mengi kiasi hicho kwa siku? Na barabara zinaweza kuhimili malori mengi kiasi hicho kwa siku bila usumbufu kwa watumiaji wengine wa bara bara?
 
Back
Top Bottom