Rwanda: Shule zitaendelea kufungwa hadi Septemba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Rwanda imetangaza kufungulia biashara lakini imewataka wafanyabiashara kufuata hatua mambo yote ya kujilinda. Aidha masoko yatafunguliwa kwa 50% tu ya wafanya biashara waliosajiliwa. Na kusisitiza malipo ya kielektorinic kila inapowezekana

Usafiri wa umma utapakia watu watakaovaa barakoa tu. Bodaboda hawataruhusiwa kubeba abiria bali kuendelea na usambazaji. Mazishi yatahudhuriwa na watu 30

Pia wataendelea kuwapima raia wote nchini humo. Huku swala la kuvaa barakoa katika maeneo ya watu wengi likiwa ni lazima. Na watu hawaruhusiwi kutembea kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na moja alfajiri

Lakini wameendelea kufunga shule zote hadi Septemba. Pia nyumba za ibada zitaendelea kufungwa hadi itakapotangazwa tofauti. Mipaka yote itafungwa isipokuwa kwa kupokea mizigo au wanyarwanda wanaorudi kwao, ambao watatakuwa kujitenga kwa siku 14

1588353792090.png

1588353815131.png
 
Back
Top Bottom