Rwanda wamezuia kutoka na kuingia Mji Mkuu wa Kigali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Rwanda imezuia usafiri wa umma na kibinafsi kati ya wilaya na Mji Mkuu Kigali.

Serikali ya nchi hiyo imetangaza kwamba ni kutokana na hali ya kutisha ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Katika wiki moja tu Rwanda ilirekodi watu 30 waliokufa kutokana na ugonjwa huo.

Kulingana na kikao cha baraza la mawaziri hatua ya kupiga marufuku usafiri wa umma na kibinafsi kati ya wilaya na mji mkuu Kigali inaanza kutekelezwa leo.

Ni moja wapo ya mikakati iliyochukuliwa kudhibiti wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona nchini Rwanda.

Serikali ya nchi hiyo imesema hali imekuwa mbaya na ya kutisha kutokana na kuongezeka sana kwa visa vya maambukizi pamoja na vifo vya watu.

Takwimu zinazotolewa na maafisa wa afya wa Rwanda zinaonyesha kwamba jumla ya watu 105 wameshafariki dunia kutokana na Covid 19 ambapo nusu yao walipoteza maisha mnamo Desemba tu.

Akizungumza na Radio ya taifa ,Daktari Tharcisse Mpunga anayesimamia huduma ya msingi ya afya alieleza kwamba "katika kiwango hiki nchi inapaswa kutekeleza sheria ya kutotoka nyumbani kote nchini " lakini ‘’hatukupenda maisha yasimame kabisa’’.

Dr Mpunga ameongeza kwamba hali ilivyo sasa wagonjwa mahututi wanakufa haraka sana watu wa rika mbali mbali wakiwemo pia vijana.

Katika hatua mpya zilizotangazwa jana usiku wa manane, biashara zote ziliamriwa kufungwa saa kumi na mbili jioni, "mikusanyiko yote ya kijamii na hafla" ni marufuku, na amri ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri imebaki.

Kadhalika imetangazwa kwamba watalii wa ndani na wa kimataifa wanaweza kusafiri kote nchini lakini baada ya kupima covid 19 na kuthibitisha kuwa hawana maambukizi ya ugonjwa huo.

Maafisa wa Afya wa Rwanda wanaamini kuwa ongezeko la maambukizi huenda lilichangiwa na sikukuu za Chrismass na mwaka mpya ambapo watu walisafiri sana kwenda maeneo yao asilia.

Katika siku saba zilizopita Rwanda imerekodi idadi isiyo ya kawaida ya visa 820 na vifo 30.Athari za hatua mpya tayari zimeanza kujitokeza ikiwa watu waliosafiri kwenda katika maeneo yao asilia kwa ajili ya sikukuu wamekosa jinsi ya kurejea mjini Kigali ili kuendelea na shughuli zao za kawaida.
 
Toleo jingine tena au ndo lile lile la mwanzo,na sisi huku tuwe makin maana na majirani kabisa.
 
Back
Top Bottom