Rwanda na Burudi wanapashwa kufanya kitu Tanzania baada ya kuwaonesha wema wakati wa mauaji ya Kimbari

Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
783
525
Leo ni siku ninayokumbuka ndugu zetu na majirani zetu Wa Rwanda na Burundi walipopata jinamizi la mauaji ya kimbali, na wale waliobahatika kukimbilia Tanzania kwa idadi kubwa.

Tuliwapokea na wengine tukawapa hifadhi kabla ya wote kuhamishiwa makambini, wale tuliowapokea walimuua Mama yangu wakatoweka, wapo raia wengi katika maeneo ya Ngara na Biharamulo waliouawa,
kwa miaka sasa takriban miaka 18 sijasikia viongozi wa Nchi hizo wakija kutupa pole, UNHCR kutufidia au Serikali kufanya lolote kwa ajiri ya familia zilizopata madhira mbalimbali.

Tusingeweza kusema lolote katika hali mbaya iliyokuwa inawakabili lakini hata sana hatusemi chochote ila tunawakumbusha tu.

Wakati mwingine wanalewa sifa hata kuanza kutubeza kana kwamba wao wana uwezo mkubwa wa maendeleo kutuzidi wanasahau kwamba kwa miongo mingi tumekuwa makimbilio yao.

Hii inanipa hasira ninapokumbuka kwamba tuliwatunza wakimbizi wa nchi kadhaa za Afrika hasa Afrika ya Kusini, ukienda kwao wanatubagua hata kutuua Waafrika wenzao kana kwamba wanasahau mzigo tulioubeba kwa ajiri yao., wengine tulowachangia damu lakini wamejisahaulisha.

Kama so kitu, moja ya setback ya uchumi wetu inatokana na wema kuwasaidia wenzetu Uganda, Zimbabwe, Mozambique, Congo Swaziland Angora Zambia Rwanda &Burundi Malawi Botswana na South Africa, kama wote hao wakisema aksante itatulia moyo sana.

Namshauri Mh. Kagame na wenzake wajipambanue ktk hili.

Namlilia Mama yangu aliyekufa bila sababu nyumbani kwake tarehe 16/6/1994 Mungu amkumbuke kwa wema wake.
 
Pole sana ndugu yangu kwa yaliokupata. Mungu amlaze mam yako mahali pema. Kuhusu swala la kufidiwa au kuombwa msamaha, hilo sidhani kama litawezekana kwa binadam wa sasa ambao wengi wamejaa roho mbaya na chuki zisizokuwa na msingi.

Kama warundi na wanyarwanda wameshindwa kuwafidia au kuwasaidia ndugu zao wenyewe walipatwa na majanga kama hayo ya kwako, watawezaje kuwasaidia nyie mliopo mbali na mipaka ya nchi zao. Kuna ule msemo unaosema "tenda wema uende zako, usingoje shukurani". Nadhani umenielewa mleta mada.
 
Pole sana kwa msiba. Ningependa kukukumbusha kuwa; kila kizazi huwa kina priorities zake, zamani wazee walisoma kusoma hadithi za uhuru nadhani sasa hatuna hizo hadithi.
Sishangai nikienda SA au Uganda kizazi kipya kisijue kuhusu utanzania wangu.

Namna nyingine nzuri ya kupewa heshima ya kile ulichofanya ni kuwa well financially hakika wale wote ulowasaidia watakumbuka mchango wako (mfano)
 
Back
Top Bottom